Sep 5, 2021
Maeneo Nane Unayotakiwa Kuyatawala Kiuhakika Ili Ufanikiwe.
Ushindi wowote katika mafanikio unapatikana kwa kutawala. Kwa mfano, Ili uweze kufanikiwa katika biashara unatakiwa kuitawala biashara hiyo katika kila eneo, kwa kuijua biashara hiyo ndani nje tena kwa uhakika.
Hata
katika mafanikio kwa ujumla vipo vitu ambavyo unatakiwa kuvitawala, kwa jinsi
unavyovitawala vitu hivyo unapata uhakika wa mafanikio kwa asilimia kubwa sana.
Je, ni mambo yapi ambayo unatakiwa kuyatawala ili kufanikiwa?
1. Jitawale wewe kwanza.
Kitu
cha kwanza ambacho unatakiwa kukitawala vizuri ili ujijengee mafanikio ni kujua
jinsi ya kujitawala wewe. Tambua jinsi ya kutawala fikra zako, matendo yako,
vitu unavyosoma au kuangalia, imani na mitazamo uliyonayo juu ya maisha ya
mafanikio.
Kwa
kujua jinsi ya kutawala hayo mambo inakusaidia sana wewe kuweza kufanikiwa na
kupiga hatua. Watu wanaofanikiwa wanajua sana jinsi ya kujitawala wao wenyewe
hasa kutokana na kumudu kutawala mambo kama hayo kila wakati.
2. Tawala mihemko yako.
Kujitawala
wewe tu hiyo haitoshi, ni muhimu kujua jinsi ya kutawala mihemko yako. Huwezi
kufanikiwa kama unashindwaa kutawala mihemko yako. Hapa inabidi ujue kutawala
tamaa zako au kujizuia kwa mambo yanayokuangusha kimafanikio.
Kama
ukishindwa kutawala mihemko yako ni wazi utashindwa. Ipo mihemko ya aina
tofauti kama mihemko ya kununua vitu hovyo, au mihemko anasa zisizo na mbele
wala nyuma. Kikubwa jiangalie una mihemko ipi wewe inayokuangusha?
3. Tawala visingizio vyako.
Kila
wakati fanya ufanyalo, lakini hakikisha usiwe tu mtu wa visingizio, tawala visingizio
vyako na kila aina ya visinguio weka pembeni. Usiwe mtu kila unaposhindwa jambo
unasingizia kwamba umeshinsddwa kwa sababu hii au ile.
Kama
jambo umeshindwa kweli ni bora ukaa kimya na uache kusingizia singizia vitu
kwani huwezi kukosa sababu. Ukiweza kutawala sababu zako, ukiweza kutawala
visingizo vyako, basi anza kujihakikishia mafanikio yako.
4. Tawala maono yako.
Najau
zipo ndoto au maono ambayo unayo na kila siku unaomba Mungu hayo maono yako yaje
yatimie. Sasa jifunze jinsi yakutawala maono yako. Maono hayo yaweke kwenye
karatasi au picha na ikiwezekana uwe unayaona mara kwa mara.
Weka
utaratibu wa kujikumbusha kila siku na kwa kujikumbusha huko inakusaidia kutawala
sana maono hayo kwa sehemu kubwa. Wengi wanaoshindwa kufanikiwa, ni watu ambao
kiuhalisia wanashindwa kutawala maono yao kwa sehemu kubwa sana.
5. Tawala sheria za mafanikio.
Hata
kama hujui lakini naomba nikwambie kwamba, zipo sheria zinazotawla mafanikio
unayoyatafuta. Kwa bahati mbaya sana sheria hizo zinafanya kazi eidha uwe
unajua au hujui lakini sheria hizo zipo kazini muda wote.
Wale
wanaoshindwa ni watu ambao wanashindwa sana pia kumudu kutumia sheria za
mafanikio. Unatakiwa kujua jinsi ya kutawala sheria za mafanikio ili ziweze
kukupa mafanikio ya uhakika. Ukishindwa kufanya hivyo ujue utakwama kufikia
ndoto zako.
6. Tawala watu wanaokushauri.
Kila
mtu ana mtu anayemshauri katika jambo fulani hivi liwe la mafanikio au la
kawaida. Wengi sasa kwa bahati mbaya wana washauri wabovu, yaani wanashauriwa
na watu wasio sahihi kwa lugha nyingine watu hao wanawapoteza.
Kwa
hiyo ili kufanikiwa kitu ambacho unatakiwa kukitawala vizuri na kukipe
mafanikio ni kutawala washauri. Tafauta washauri ambao watakusaidia wewe
kufanikiwa na si washauri watakokupoteza wewe na kukufanya uonekane hufai.
7. Tawala muda wako.
Kutawala
muda ni jambo gumu sana kwa watu wengi kulifanya. Watu wengi wanashindwa
kutawala muda wao na matokeo yake muda wanaupoteza sana kwa mambo ya hovyo ili
mradi tu muda huo umepotezwa pasipo malengo.
Kwa
mfano; kuna wanaopoteza muda wao katika soga, kuna wanaopotezea muda wao
kufanya kazi ambazo si zao badala wangefanya kazi zao ambazo zingewapeleka na
kuwapa mafanikio makubwa ya kimaisha kwa sehemu kubwa sana.
8. Tawala mipango yako.
Ile
mipango uliyonayo hautakiwi kuiacha tu hivi hivi hewani, unatakiwa kujua jinsi
ya kuitawala mipango yako na ukapata mafanikio makubwa. Kila wakati jikumbushe
mipango yako ni ipi na utaifatilia vipi hadi ifanikiwe.
Unapokuwa
unajua hatma kama hizi za mipango uliyonayo, hicho ni kichochezi cha kukupa
wewe nguvu ya kuweza kusonga mbele zaidi kwenye mafanikio. Watu wengi wenye
mafanikio wana uwezo wa kutawala pia mipango yao sana na kuimudu.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0687449428, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.