Sep 13, 2021
Mambo Yakiwa Hivi, Rudi Kwenye Njia Kuu.
Pengine nikuulize, huwa unajisikiaje, hasa pale ambapo mambo yako huwa hayaendi kama unavyotaka au yanapokwenda kinyume na mategemeo yako?
Je, huwa unaanza kulalamika na kujisikia vibaya kwa sababu ya mambo kwenda hovyo? Au huwa unakaa chini, na kuamua kutokufanya kitu chochote, au huwa unafanyaje?
Kama umekuwa ukifanya mambo hasi pale mambo yako yanapokwenda vibaya, hapo umekuwa ni sawa na unajipoteza tu, hakuna kitu ambacho umekuwa ukikijenga.
Kitu cha kipekee unachotakiwa kufanya pale mambo yako yanapokwenda vibaya au hovyo ni kwa wewe kuamua kurudi kwenye njia ya kuu, yaani kwenye jambo ulilokuwa ukilifanya.
Najua umeshawahi kuwa na siku mbaya, wiki baya au mwezi mbaya, hayo yote hayasaidii, zaidi ni kuamua kusonga mbele kwa mbele. Yaliyopita yamepita, na yamekuwa historia isiyorudi.
Haijalishi kama unajiona una bahati mbaya, hiyo sio sababu ya hayo unayoyaona mabaya kwako, yakatawala maisha yako kwa sehemu kubwa na kuharibu kila kitu mbele yako.
Unayo sababu ya wewe kubadili maisha yako, kama hutaruhusu jana yako itawale maisha yako. Acha yaliyopita yapite, wewe kazana na mambo yajayo, hayo mengine sahau.
Ni kweli unaweza kufikia ngazi kubwa ya kimafanikio, ukiamua
kutokuzuiliwa na kile kilichotokea jana. Amua kusonga mbele bila kujali nini
kimetokea kwenye maisha yako ya jana.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.