Nov 17, 2018
Kila Wakati Zitumie Kanuni Hizi Muhimu Kwa Ajili Ya Mafanikio Yako.
Leo nitaomba
nichukue walau dakika chache ili niweze kukumbusha kanuni sita za kukupa
mafanikio unayoyahitaji. Hizi ni kanuni ambazo ukizitumia na kuzifanyia kazi ni
lazima zikupe matokeo makubwa kwa ajili ya mafanikio yako.
Wengi wanaozitumia
kanuni hizo zinawasaidia sana kupiga hatua na kuwafanikisha. Kila wakati jaribu
kuzitumia kanuni hizi kwa ajili ya manufaa yako na ya wengine pia. Usitoke hapo
ulipo twende pamoja katika somo letu la leo tujifunze kanuni hizi;-
1. Kanuni ya 1; Chukua hatua
stahiki.
Miongoni
mwa vitu vitakuvyofanya uzidi kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa ni pamoja na
kuendelea kuchukua hatua stahiki kwa hicho unachokifanya au kile unachotaka
kufanya. Kushindwa kuchukua hatua huko ni kuchagua kujiangusha wewe mwenyewe.
2. Kanuni ya 2;Tumia siku yako
vizuri na kwa uhakika.
Mafanikio
siku zote ni matokeo ya vile unavyoitumia siku yako vyema, hivyo ulivyo leo ni
matokeo ya hatua ulizozichukua siku ya jana. Hivyo jifunze kuitumia leo yako
vyema ili uishe kesho yako yenye mafanikio na furaha tele.
3. Kanuni ya 3; Jenga mtazamo sahihi
kila wakati.
Hivyo
ulivyo leo katika suala la mafanikio ni matokeo ya mawazo yako. Kama mawazo
yako ni hasi basi hata maisha yake yatakuwa vivyo hivyo. Kama unataka unataka
kubadili maisha yako, basi badili na mawazo yako na kuwa chanya.
4. Kanuni ya 4; Tafuta njia ya
mafanikio yako.
Kama
tutaamua kutafuta mafanikio ya kweli ni lazima tutafuta njia ya kuyapata
mafanikio hayo, ila kama hatuhitaji mafanikio ni lazima tutafuta visingizio.
Hivyo ili tuweze kufika katika kilele cha mafanikio tunatakiwa kutafuta njia ya
kupata mafanikio hayo.
5. Kanuni ya 5; Jenga uwezo wa kutatua
changamoto;
Katika
maisha haya kila kitu kinawezekana, kama kuna jambo unaliona ni changamoto na
haliwezekani basi mahala hapo ndipo palipo na fursa lukuki zilizojificha, hivyo
jifinze kushughulika na kila changamoto zilipo katika jamii yako kwani hapo
ndipo palipo na fursa.
6. Kanuni ya 6; Toa hofu zako.
Siraha
hatari zaidi duniani si bunduki wala mabomu ya nyuklia kama wengi wadhanivyo,
bali siraha hatari zaidi duniani ni hofu. Hofu ndio chanzo kikubwa cha kuua
ndoto za walio wengi, wengi wetu tunashindwa kuthubutu kufanya jambo fulani eti
kwa sababu ya kwamba tunaogopa kitu fulani.
Hivyo
kama kweli unataka kupiga hatua za kusonga mbele tunatakiwa kuhakikisha ya
kwamba tunaondokana na hofu, kwani hofu ni adui nambari moja wa mafanikio.
Asante
sana kwa kusoma makala haya kupitia mtandao huu wa Dira Ya Mafanikio, nikutakie
siku njema na mafanikio mema.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.