Nov 2, 2015
Kama Ulikuwa Hujui, Huu Ndiyo Ukweli Halisi Wa Maisha Yako.
Kama
ulikuwa hujui, unazo siku za kuishi ambazo hazizidi elfu 30,000 kuanzia sasa,
hiyo ikiwa ni sawa na miaka 82. Nikiwa na maana kuwa baada ya siku hizo kuisha
karibu kila mtu aliyepo hapa duniani atakuwa ameshakufa ikiwemo hata na mtoto
anayezaliwa leo. Kama itatokea binadamu atakuwa hai baada ya siku hizo basi huo
utakuwa ni moja ya muujiza.
Kama
ni hivyo umejipangaje kuishi kwenye siku hizo ambazo naweza nikasema ni chache.
Lengo langu siyo kukukatisha tamaa ya maisha, ila nikukufikirisha na kujua
namna utakavyoweza kujipanga na kuishi maisha yenye hamasa ya kukufanya
ufanikiwe na siyo kujikalia na kubweteka.
Kitu
cha kukumbuka hapa ambacho hutakiwi kusahau ni kwamba unazo siku chache sana za
kuishi duniani. Je, unazitumiaje siku hizo katika maisha yako ya sasa. Je,
umekuwa ukizitumia kwa manufaa au hasara? Kama umekuwa ukizitumia kwa hasara
pole sana, utapoteza mengi na ni lazima utajuta.
Elewa,
maisha yako ni kama dharura. Kama ni hivyo hutakiwi kuishi kiholela kama vile umenunua
muda wote duniani. Inatakiwa tuishi kwa mipango ambayo unaamini ni lazima ilete matokeo chanya na ya haraka kwa
kipindi cha muda mfupi ulionao. Kama kuna mtu anakupotezea muda, achana naye.
Ishi kwa kulinda muda ulionao.
FURAHIA MAISHA YAKO YA SASA. |
Wakati
ulionao ni sasa rafiki yangu. Fikiri jambo hili vizuri, mambo yaliyopita
yamepita na hakuna kesho katika maisha yako hata ufanyaje. Kama ni hivyo, nafasi
pekee uliyonayo kwenye maisha yako ni sasa. Mara nyingi umekuwa ukipanga sana
kwamba nitafanya hiki siku nyingine au mwaka fulani yote hayo ni sawa, lakini
hakuna kesho wakati ulionao ni sasa wa kufanya mabadiliko makubwa kwenye maisha
yako.
Acha
kuendelea kujidanga kila siku kwa kujipa ahadi nyingi ambazo huzifikiki.
Uhalisia wa maisha yako upo sasa. Kama kuna kitu unataka kukifanya kifanye leo,
na wala usingoje kesho. Ikiwa utaendelea kungoja kesho hakuna ambacho utaweza
kufanikisha kwenye maisha yako, sana sana utapoteza muda.
Zaidi
kumbuka kifo, hakikusubiri wewe ukamilishe mipango au mambo yako fulani ili ufe,
kifo kinakuja kwako muda na wakati wowote. Hivyo, hutakiwi kupoteza muda wako
kwa lolote lile. Jipange kuishi maisha yako kwa furaha, amani na mafanikio makubwa
ndani ya muda mfupi ulionao.
Lakini
hata hivyo hiyo haitoshi ni vyema kuishi maisha mazuri na wengine yatakayokupa
furaha wewe na wao kwa siku ulizonazo. Utawazaje kuishi hivyo?
1. Tengeneza orodha yako.
Ni
vyema ukajitengenezea orodha ya mambo yako unayotaka kuyatimza kabla hujafa. Iandike
orodha hiyo vizuri na hakikisha unaifatilia kwa makini kuona kama uliyoandika
unayafatilia na kuyatimiza.
2. Ishi sasa.
Hakuna
kujidanganya ishi maisha yako sasa, usiwaze
sana juu ya kesho, halafu ukajikuta ni mtu wa kuahirisha tu. Kama ni
kuboresha maisha yako, yaboreshe maisha yako sasa. Baada ya muda utakuwa mtu
mwingine wa mafanikio makubwa tofauti na unavyofikiri.
3. Furahia mafaniko unayoyapata.
Kama
kuna kitu umekifanisha ni vyema ukajifunza kukifurahia leo. Acha kusubiri hadi
ufikie mafinikio makubwa ndio uanze kufurahia maisha yako. Kwa kadri utakavyozidi
kufurahia mafanikio haya madogo, utajikuta ndivyo unapiga hatua kubwa ya mafanikio.
4. Weka alama za maisha yako.
Ni
kitu gani ambacho ikiwa utakufa leo utakiacha kama kumbukumbu kubwa kwa kizazi
cha leo na kesho. Kama kitu hicho kipo ni vyema ukaanza kukifanya kwa juhudi
zote. Weka alama ili kizazi kijacho kijue wewe ulikuwa ni nani. Na uliacha kitu
gani cha faida kwao.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.