Nov 12, 2015
Tiba Bora Ya Mwili Na Afya Yako Ni Hii Hapa.
Kuna
wakati kama binadamu huwa tunapatwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Yapo magonjwa
ambayo huwa tunajua chanzo na tiba yake na mengine huwa hatujui. Kwa kuwa
afya ni muhimu sana kwa binadamu, kila mtu hufanya kila linalowezekana
kuhakikisha mwili wake uko salama kiafya.
Katika
kuhakikisha hili linatimia wapo ambao hutumia dawa za kila aina na wapo pia
wengine ambao huamua kutumia tiba mbadala. Yote haya hufanyika ili kupata tiba
bora ya mwili na afya zetu. Katika makala hii ya leo tutaangalia tiba nyingine
bora ya mwili ambayo haifahamiki na wengi. Tunasema ni bora kwa sababu inatibu
magonjwa mengi. Tiba hii ni tiba ya zabibu.
Ikumbukwe
Zabibu hulimwa sehemu nyingi sana duniani. Matunda ya zabibu ni matamu sana kwa
maana ya ladha nzuri mdomoni. Zabibu ziko za kijani, nyeusi na
urujuani(Violet). Pia ziko katika maumbile na ‘saizi’ mbalimbali. Kuna zile
zenye maumbile madogo na zina mbegu ndogo na nyingi.
TIBA BORA YA MWILI. |
Zabibu
ni nzuri sana kwa matatizo ya koo, nywele, ngozi na matatizo ya macho. Vilevile
zabibu inaleta hamu ya kula. Zabibu zinasaidia kuondoa kiu, homa, pumu, ukoma,
kifua kikuu, matatizo ya sauti na kutapika. Inapunguza gesi tumboni.
Zabibu
zinaharibika upesi baada ya kuiva hivyo zinataka matunzo mazuri kwa kuwekwa
jokofu au penye baridi baada ya kuvuna. Ili zabibi ifanye kazi, huna budi
kuzila nyingi kwa siku. Zabibu hufanya mtu aonekane kijana kwa muda mwingi. Glucose
iliyo kwenye zabibu huyeyuka kwa haraka sana mwilini.
Zabibu
zinasaidia kwenye mambo mengi sana kama unywaji pombe kupita kiasi yaani ‘Alcoholism’. Matatizo ya unywaji pombe
mara kwa mara au kupita kiasi unaweza kuachwa au kupunguzwa kwa kula zabibu kila
siku. Zabibu zenyewe zinatoa pombe mwilini.
Harufu
ya zabibu inaleta ahueni kwenye kwenye matatizo ya pumu na matatizo ya watoto
wadogo. Juisi ya zabibu inasaidia kutibu matatizo ya choo kwa watoto wadogo,
hata kwa wakubwa inasaidia. Zabibu inasaidia kupunguza matatizo ya moyo na
matatizo ya figo.
Zabibu
pia inasaidia matatizo ya ini kwa sababu ina tindikali aina ya Malic, Citric na
Tartaric. Tindikali hizi zinasaidia kusafisha damu, kuamsha ufanyaji kazi wa
tumbo na ini.
Hayo
ndiyo magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa kutumia Zabibu. Hivyo, ni muhimu sana
kwa miili yetu.
Tunakutakia
siku njema na afya bora, ila kama umesoma makala hii mshirikishe na mwingine
ili apate tiba hii bora bila kuikosa.
Endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza zaidi.
Makala hii imeandikwa na Joshua
Labani kwa ushirikiano na Aminiel Richard wa Tanga -Tanzania . Kama una maoni
au ushauri wasiliana na Waandishi wa makala hii kwa email
richardaminiel007@gmail.com/labanjoshua4@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.