Nov 5, 2015
Huu Ndiyo Ufunguo Wa Lazima Unaotakiwa Kuwa Nao Ili Kufanikiwa.
Moja
ya changamoto kubwa inayopelekea malengo ya wengi kutokutumia, ni ile hali ya
kukosa hamasa yakuendelea kwenye hayo malengo. Hamasa hii inapokosekana kwa
malengo yoyote yale iwe kuamka asubuhi na mapema, kubadili tabia fulani au
kubadili tabia ya matumizi mabaya ya pesa ni dhahiri malengo hayo hayawezi
kutimia.
Hamasa
ni kitu kikubwa sana kinachofanya wengi kushindwa kuendelea na malengo hayo
hasa pale wanapoikosa. Hiyo yote inatuonyesha kwamba hamasa ni ufunguo
mmojawapo wa mafanikio muhimu, ambao kila mtu mwenye nia ya mafanikio hatakiwi
kuukosa. Kama utakosa jambo hili kila wakati, ni wazi hutaweza kufanikiwa.
Uzoefu
unaonyesha hakuna kitu kitu chochote ambacho mtu anaweza kukifanisha ikiwa
atakosa hamasa. Kwa hiyo kama unataka kujua kama uko kwenye njia sahihi ya kufanikisha
malengo yako, angalia hamasa uliyo ndani yako. Una hamasa kubwa kiasi gani ya
kukusukuma kwenye mafanikio?
Unaweza
ukawa unaanza kujiuliza kazi kubwa ya hamasa nini na inafanya kazi vipi? Sikiliza,
siku zote hamasa inasimama kwetu kama msukumo, au kitu cha kutusukuma kila siku
kwenye kufanya malengo yetu tuliyojiwekea. Na hamasa hizi huwa zipo za aina
mbili yaani hamasa hasi na hamasa chanya.
Unapokuwa
una hamasa chanya hapa unakuwa unajisukuma mwenyewe, hakuna anayekwambia fanya
hivi au vile kwa sababu unakuwa unajua faida ya jambo unalolifanya. Lakini unapokuwa
na hamasa hasi, hii tunasema ni hamasa kama ya kusukumwa, unakuwa unafanya
jambo pengine kwa sababu unaogopa kufukuzwa kazi. Tuchukulie upo kazini na bosi
wako anataka mambo yaende vizuri ni lazima ufanye kazi kwa bidii na kwa hamasa,
maana ukifanya kinyume na hapo utafukuzwa kazi.
Hivyo,
hamasa yoyote ile iwe chanya au hasi ni muhimu sana kwetu lakini ingawa ile
chanya ndiyo unayotakiwa kuwa nayo kwa sababu utafanya kazi zako bila kuchukia.
Wengi wanaofanya kazi zao kwa hamasa hasi, mara nyingi hujikuta wakichukia kazi
zao na kuziona mbaya. Mpaka hapo unaweza ukaona hamasa ni kama kipimo cha kujua
tupo wapi na tuna hali gani kuelekea kwenye malengo yetu.
Kwa
hiyo, hamasa ni kitu cha lazima kukuwezesha wewe kufanya jambo lolote bila kuchoka.
Inapotokea umekata tamaa unaona huwezi kubadili tena tabia zako mbaya zinazokuzuia
kwenye mafanikio kitu pekee kitakacho kunyaua hapo ni hamasa uliyonayo. Msukumo
huu ni muhimu sana kwa wewe kuwa nao kwa jambo lolote hasa pale mambo
yanapokuwa magumu.
Kama
ni hivyo, ni lazima kila siku na kila wakati katika safari yako ya mafanikio
hakikisha unayohamasa ya kutosha kukuwezesha kuendelea mbele. Ni lazima uwe na hamasa hii itakayokufanya
ufanye mambo hata yale unayohisi wakati mingine huwezi kuyafanya. Hilo ni lazima.
Hamasa hiyo unaipataje kila siku? Ni rahisi tu:-
Kwanza, anza kwa kidogo.
Utajenga
hamasa kubwa sana ikiwa utakuwa utaanza malengo yako kwa kidogo. Acha kutaka
kubadili mambo makubwa kwa pamoja utakuwa unakosea. Kama umejiwekea malengo ya
kukimbia anza kwa kidogo tu. Kama umejiwekea malengo ya kujisomea sana anza pia
kwa kidogo.
Kumbuka
katika kila eneo anza kwa kidogo hiyo itakupa nguvu ya kuendelea mbele na
utajikuta umejenga hamasa ya kutosha kila siku. Wengi wanaofanikiwa kujijengea
hamasa kubwa kila siku, kila kitu wanachokifaya huwa wanaanza nacho kwa kidogo
na kisha huchukua uzoefu na kusonga mbele zaidi ya pale walipo.
HAMASA NI LAZIMA KWA MAFANIKIO YAKO. |
Pili, jiwekee malengo machache.
Siri
ya mafanikio ipo kwenye kutekeleza malengo machache kwanza. Ikiwezekana jiwekee
lengo moja tu kwanza ambalo utaamua kulifatilia usiku na mchana mpaka litimie. Lakini
kitendo cha kuwa na malengo mengi inaweza ikawa ni sababu mojawapo ya kukatisha
tamaa na kukosa hamasa.
Unapokuwa
na malengo machache hiyo inakuwa inakupa nguvu na hamasa ya kutaka kuendelea
kufanya siku hadi siku kwa sababu unakuwa unaona mendeleo ya malengo yako
mapema. Hivi ndivyo hamasa kubwa inavyopotikana kila siku.
Tatu, jifunze kwa wengine.
Ni
muhimu kujifunza kwa wengine kwa kile unachokifanya. Unaweza ukaangalia
waliofanikiwa zaidi yako. Ama unaweza ukajifunza kupitia vitabu. Ikiwezekana unaweza
ukakaa nao ili wakueleze nini kilichowasukuma na kufika hapo walipo.
Watu
hawa utakaojifunza kwao ni lazima watakupa nguvu fulani ya kukuchochoa kuweza
kusonga mbele na kukupa hamasa ya ajabu kwa kile unachokifanya. Hamasa hiyo utakayoipata itakusadia kusimama
katika nyakati zote za maisha iwe za kawaida au kukatisha tamaa.
Nne, weka wazi jambo unalolifanya.
Ili
uweze kufanikiwa ni vyema ukaweka wazi jambo unalolitaka kulifanya. Kama umeamua
kukimbia basi, unaweza ukaliweka lengo lako hilo kwenye mandishi au picha na
likaonekana kwa uzuri kabisa. Kwa kufanya hivyo litakupa hamasa ya kufatilia
malengo yako hayo mara kwa mara.
Kwa
kufanya mambo hayo manne yatakusaidia sana kukupa hamasa ambayo utakuwa nayo karibu
kila siku. Na kumbuka huu ndio ufunguo muhimu unaotakiwa kuwa nao kwa ajili ya
mafanikio yako ya leo na kesho.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari yako ya mafanikio iwe ya ushindi na endelea
kuwashirikisha wengine kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila
siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.