Nov 3, 2015
Kama Unafikiri Ili Ufanikiwe Ni Lazima Uwe Na Elimu Kubwa, Unajidanganya Mwenyewe.
Ni
rahisi sana kuweza kuwaza kwamba hujafanikiwa pengine kwa sababu hukusoma, au hujafanikiwa
kwa sababu huna elimu kubwa sana ambayo ingeweza kukupa mafanikio. Haya ni
mawazo ambayo wengi wanakuwa nayo na kufikiri, elimu ni kila kitu bila elimu
maisha hayawezekani. Ni fikra hizi hizi ambazo zimekuwa zikiwadanganya wengi na
kuwarudisha nyuma kila wakati.
Ukweli
wa mambo ulivyo ni hivi, elimu isiwe kisingizio kikubwa kwako cha kukufanya
ukashidwa kufanikiwa. Mafanikio utayapata tu wewe mwenyewe ukiamua iwe hivyo
kwako kwa kuchukua hatua huku ukiwa na nia dhabiti. Wapo wengi waliofanya
mafanikio makubwa kwa kuwa na elimu za kawaida tu ambazo waliamua kuzitumia
vizuri. Hiki ndicho kitu unachotakiwa kuwa nacho.
Je,
unajua hawa na akina nani, waliopata mafanikio makubwa bila kuwa na elimu kubwa
ya kutosha, na unaweza ukapata kitu cha kujifunza kutoka kwao?
1. Richard Braison.
Huyu
ni mfanyabiashara na mwekezaji mkubwa Duniani. Yeye ni mwanzilishi wa makampuni
ya Virginia ambaye chini yake yapo
makumpuni mengine 400. Historia yake ya kuwa mjasiriamali ilianzia mbali hasa
pale alipoacha shule akiwa na umri wa miaka 16 na kuanza biashara ya kuuza
magazeti. Alifanya vizuri na kuendelea kusonga mbele na kuzidi kuwekeza katika
maeneo mengine. Hadi sasa anakadiriwa kuwa utajiri alionao Braison unafikia zaidi
ya dola bilioni 5 za kimarekani.
Lakini,
ukiangalia maisha ya Richard Braison kwa ujumla, kilichomfanikisha na
kumfikisha hapo si elimu kubwa aliyonayo bali ni nia na hamasa yake kufanikiwa.
Yeye kwa kifupi hakusoma sana aliacha shule mapema na kuanza kujihusisha na
ujasiriamali mapema. Safari yake hiyo ya ujsiriamali imemfikisha hapo na si
elimu kama unavyoweza kufikiria. Hivyo elimu kwake haikumpa na mafanikio
makubwa.
UNAWEZA KUFANIKIWA KWA ELIMU YAKO YA KAWAIDA. |
2. Mark Zuckerberg.
Pia
huyu naye ni mfanyabiashara kijana na ni tajiri ambaye anamiliki mtandao wa facebook. Kwa mara ya kwanza alianzisha facebook akiwa chumbani kwake akiwa anasoma
chuo. Kutokana na mafanikio aliyoanza kuyaona ya kujitokeza kwenye biashara
hiyo ya mtandao aliacha chuo alichokuwa anasoma na kuamua kujihusisha na biashara
kikamilifu.
Leo
hii tunapoongea facebook ni moja ya mtandao mkubwa sana wa kijamii uliopo
duniani. Kutokana wa wingi wa watumiaji umemfanya Mark Zuckerberg kuwa moja ya mabilionea wakubwa duniani tena akiwa kijana, ambapo
utajiri wake unakadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 36 za kimarekani.
Mafanikio yote hayo pia aliyapata kutokana na kujituma kwake wala si elimu
kubwa.
3. Michael Dell.
Bila
sha wengi tunafaham au tunatumia kabisa
kompyuta inayofahamika kama Dell. Huyu ndiye mwanzilishi wake. Historia
yake ya madiliko ilianza mwaka 1992 pale
alipoamua kuacha chuo kikuu cha Texas na kuanza kujihusisha moja kwa moja na
biashara ya kompyuta. Kwa muda mfupi tu alijikuta akitajwa na gazeti la Forbes linalojihusisha na habari za watu
matajiri, kuwa ni miongoni mwa vijana matajiri.
Wakati huo Michael Dell alikuwa
na miaka 27.
Kwa
sasa utajiri wake unakadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 19 za kimarekani.
Kitu cha kujiuliza kwake je angebaki kule angeweza kupata mafanikio hayo
makubwa? Yeye aliamua kutafuta njia ambayo aliiona ni sahihi kwake na ikamfikisha
hapo alipo. Leo hii dunia nzima inafurahia ugunduzi wake huo alioufanya na
kufaidi matunda yake.
4. John Mackey.
Hakuna
ambaye aliyeweza kufikiri kwamba biashara chakula na matunda kwa wakati ule ingeweza ikamfanya mtu akawa
tajiri? Hiki ndicho kilichotoke kwa John Mackey na mchumba wake. Watu hawa walijikuta
wakiacha chuo na kuanza kujihusisha na kuuza chakula na matunda kwa asilimia
zote. Biashara yao ilikuja kukua na kuwa kubwa kiasi cha kwamba kuweza kuuza
Marekani na Kanada.
Ilifika
wakati John Mackey alistaafu kufanya kazi hiyo akiwa tajiri mkubwa kabisa. Pesa
nyingi alikuwa amekusanya na alikuwa akiishi maisha mazuri na bora kabisa ya kisasa. Kilichomfikisha hapo alipo ni
imani ya kuwa ni lazima atafanikiwa na wala siyo elimu yake. Kama ni elimu aliachana
nayo mapema na kuamua kujihusisha na biashara.
Kama
nilivyoanza makala haya, unaweza ukawa umefikia ngazi fulani ya elimu na
kuamiani kabisa kwamba, pengine hupati mafanikio makubwa mpaka ufikie ngazi fulani,
hilo sio kweli kabisa. Itumie elimu kwako kama chachu ya kukufanikisha zaidi,
lakini kama umeikosa isiwe sababu sana ya kukuzuia kwenye mafanikio yako.
Dira ya mafanikio inakutakia siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote.
Na kumbuka endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.