Nov 9, 2015
Hatua Sita Wanazopitia Matajiri Wengi Na Kufanikiwa.
Siri
kubwa ya mafanikio mara nyingi ipo kwenye kujifunza hasa kwa wale watu
waliofanikiwa zaidi. Ikiwa utaweza kuitumia siri hii, ndani ya muda mfupi
utakuwa umeweza kumudu kubadili maisha yako kwa kiasi kikubwa lakini kama utachukua hatua.
Kwa
kulijua hili unalazimka kujifunza kila siku ili kujua mbinu, kanuni na hata
hatua wanazotumia matajiri wengi kufanikiwa. Je, unajua ni kanuni au mbinu zipi zinaweza kukusaidia
na kukufikisha kwenye mafanikio. Najua zipo nyingi, lakini kwa leo tuangalie
hatua hizi wanazopitia matajiri wengi na kufanikiwa.
1.
Hatua ya kujiwekea vipaumbele.
Ninaweza
nikasema hii ndiyo hatua ya kwanza kabisa ya matajiri wote wanayoipitia. Ili
kutimiza malengo yao, kitu cha kwanza wanachokifanya ni kuweka vipaumbele. Hata
ikitokea wana malengo mengi vipi, lakini kwa kuwa wana vipaumbele inawasaidia
kujua ni lengo lipi waanze nalo na lipi waliache.
Vipaumbele
ni msingi mkubwa wa maendeleo yoyote yale. Bila vipaumbele hakuna mafanikio yoyote
yanayaweza kutokea kwa sababu kila kitu kinakuwa kinafanywa kiholela. Unapoweka
vipaumbele inakuwa rahisi kutimiza malengo yako kwa sababu unakuwa unaweka
nguvu nyingi za uzingativu sehemu moja na kuleta matokeo mazuri.
JIWEKEE VIPAUMBELE VYA MAFANIKIO. |
2. Hatua ya kutengeneza pesa.
Matajiri
walio wengi wana njia nyingi za kutengeneza pesa. Hawa sio watu wa kutegemea
njia moja ya kuwaingizia kipato. Na huo ndio ukweli ambao kwa mtu yeyote
anayetaka kuwa tajiri anatakiwa kuujua. Ili uwe tajiri lazima uwe na vitega
uchumi vingi vya kukuingizia kipato. Hata kama ni kimoja lakini lazima kiwe
kimegawanyika sehemu nyingi tofauti.
3. Hatua ya kujifunza kila siku.
Njia
nzuri ya kukufikisha kwenye utajiri ni kuangalia matajiri wanafanya nini na kisha
na wewe kufanya. Matajiri walio wengi wanalijua hili ndio maana ni watu wa
kujifunza kila siku kupitia vitabu na kwa watu waliofanikiwa zaidi yao.
Kujifunza ni njia ya uhakika ya kufikia mafanikio kwa haraka, kwa sababu inakuwa
rahisi kujua mbinu nyingi za mafanikio kwa muda mfupi.
4. Hatua ya kufanya kitu cha ziada.
Watu
wenye mafanikio muda mwingi wanafanya kitu cha ziada cha kuwatoa kwenye hali ya
kawaida au kuridhika. Huwa si wepesi sana kuridhika na kujiona kwamba maisha
ndiyo wameyaweza, hapana. Ni watu wa kutafuta kitu cha kuwatoa kwenye ‘comfort zone’ zao. Kwa hili hufanikiwa
kufikia mafanikio makubwa.
5. Hatua ya kujiwekea malengo ya
kifedha.
Ikiwa
unataka kupata matokeo unayayapata sasa, endelea kufanya mambo ambayo
unayofanya sasa. Hautaweza kubadili maisha yako hata iweje. Huu ndio ukweli
halisi, hasa linapokuja suala la kujiwekea malengo ya kifedha. Ili uwe tajiri
ni lazima kujiwekea malengo ya kifedha na kubadili kipato chako. Matajiri wengi
wanapitia hatua hii muhimu.
6. Hatua ya kutatua matatizo.
Watu
wenye mafanikio, mara nyingi wanatatua matatizo. Wanajua kabisa matatizo ndiyo
yanayosabbisha wao wawe matajiri. Kama hakuna tatizo maanake inakuwa ni ngumu
sana kuweza kufanikiwa. Matatizo yanakuwa yanawapa fursa za kuweza kufanikiwa.
Hii pia ni hatua mojawapo muhimu ambayo inapitiwa na matajiri wengi kabla
hawajaufikia utajiri huo.
Hizo
ndizo hatua za msingi ambazo matajiri wengi wanazipitia. Je, unataka kuwa
miongoni mwa mtajiri wa wakubwa kwa baadae? Kama jibu ni ndiyo, ishi na fanya
yale wanayofanya matajiri wengi. Njia ya mafanikio itakuwa ni wazi kwako.
Nikutakie
ushindi na mafanikio makubwa na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili
ya kujifunza na kuhamasika kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.