Feb 15, 2016
Hatua 6 Za Kuchukua Ili Uwe TAJIRI.
Hivi
umeshawahi kujiuliza kuwa ipo siku
unaweza ukawa na mafanikio makubwa hadi kufikia utajiri? Kama bado hujawahi
kuwaza hivi hata siku moja, leo nataka nikupe habari njema kuwa hata wewe
unaweza ukawa tajiri leo hii endapo utaamua.
Unashangaa!
Ndiyo unaweza. Kwa nini nakwambia unaweza? Sikiliza. Kufikia mafanikio makubwa
na hatimaye kuwa tajiri si bahati wala muujiza kama ambavyo wengi wamekuwa
wakifikiri sana. Bali ili uweze kuwa tajiri
unahitaji kuwa na maandalizi yakutosha na kuchukua hatua muhimu za kukufikisha
huko.
Ikiwa
utakubali kufanyia kazi hatua hizo basi ni wazi unaweza kufikia utajiri mkubwa
ambao upo mbele yako na unaokusubiri. Sasa bila kupoteza muda, naomba twende
pamoja kwenye hatua muhimu ambazo unaweza ukazifuata kila siku na kila wakati
hadi kuufikia UTAJIRI.
1. Tengeneza njia nyingi za
kukuingizia kipato.
Hakuna
njia ya uhakika ambayo inaweza ikakufikisha kwenye utajiri kinyume na kuwa na
vyanzo vingi vya pesa. Huwezi kufanikiwa kama maisha yako yanategemea chanzo
kimoja cha pesa. Kwa hakika hii itakuwa ni ndoto na pia ngumu sana kwako.
Kwa
kuwa umeshalijua lengo lako kubwa unataka kuwa tajiri, hapo sasa unatakiwa
kuweka juhudi zote kwa kutengeneza njia nyingine za kujiingizia kipato chako. Kwa
kufanya hivyo utakuwa umejiweka kwenye nafasi kubwa ya kufikia mafanikio
makubwa na hatimaye kuwa TAJIRI.
MAFANIKIO NI HATUA KWA HATUA. |
2. Jiwekee malengo ya kifedha.
Mbali
na kutengeneza njia nyingi za kukuingizia pesa, lakini ni vizuri ikiwa
utajiwekea malengo yako ya kifedha. Hapa sio suala la kukusanya pesa tu peke
yake, inabidi pia utambue unataka kukusanya pesa kiasi gani baada ya muda
fulani.
Unaweza
ukaanza kujiwekea malengo haya kwa mwezi na hata mwaka. Na unaweza ukaanza
kujiuliza ‘mwaka huu ifikapo disemba ni
lazima niwe na kiasi hiki cha pesa’. Na unapokuwa unajiwekea malengo hayo,
yanakusaidia kukusukuma kufanya kazi kwa juhudi zote ili ufikie malengo yako ya
utajiri kwa haraka.
3. Jifunze kila siku.
Watu
matajiri siku zote si wajuaji. Ni watu wa kujifunza. Kwa kuwa umechagua njia ya
kukufikisha kwenye utajiri, inabidi ukubali kuwa mpole na kujifunza kila siku.
Bila kufanya hivyo utaachwa nyuma sana. Hii ni kwa sababu, kwa sasa tupo kwenye
ulimwengu wa habari. Kama huna habari za kukufanikisha ni sawa na huna
mafanikio kabisa.
Kama
ulikuwa huna utaratibu huu unatakiwa kuunza mara moja. Anza kwa kujisomea
vitabu. Sikiliza mafundisho ya mafanikio au huwezi hilo hudhuria semina au
jifunze kutoka kwa marafiki zako. Naamini ukijifunza utabadilisha maisha yako
sana kuliko unavyodhani na kwenda mbele zaidi.
4. Badili mtazamo wako kuhusu pesa.
Mara
nyingi mitazamo tuliyonayo ndiyo ambayo hutufikisha hapo tulipo. Jaribu kuangalia
hili kwa undani utagundua ukweli huu. Hata kwenye mambo ya pesa na mafanikio ni
hivyo hivyo. Ili uweze kufanikiwa kuna umuhimu wa kubadili sana mitazamo yako
kuhusu pesa.
Kila
unapoifikiria pesa unakuwa una mtazamo upi? Je, unaiona pesa ni adui? Unaiona
pesa kama ni shetani kwako au unaionaje? Kwa vyovyote vile kama una mtazamo
hasi kwenye fedha huwezi kuwa tajiri. Ni lazima uione pesa kama rafiki yako wa
karibu ili ufanikiwe.
5. Tatua changamoto zinazowakabili
watu.
Watu
wenye mafanikio siku zote ni watu wa kutatua changamoto zinazowakabili watu.
Hawa ni watu ambao huwa si walalamikaji sana, ni watu wa kuchukua hatua dhidi
ya maisha yao na ya wengine. Hicho ndicho kitu ambacho huwafanya wapate pesa
na fursa nyingi siku hadi siku.
Kwa
jinsi wanavyotatua matatizo ndivyo ambavyo pesa inazidi kumiminika. Hakuna ubishi
wala mtu atakayekuzuia kupata pesa ikiwa wewe unatatua changamoto
zinazowakabili watu. Ni lazima upate pesa hata iweje. Tena kuna wakati hizo
pesa watakuletea wao wenyewe hata kama umelala.
6. Fanya kitu cha kukutoa kwenye hali ya mazoea.
Kuna
wakati ambapo tunakuwa tunaamka hatujisikii kufanya kile tunachokifanya. Hapa
sasa ndipo ambapo unatakiwa kufanya hivyo hivyo. Unatakiwa kutoka kwenye mazoea
uliyonayo na kujisukuma mpaka kufanya kitu hicho kwa ngvu zote hata kama
unajiona huwezi.
Kwa
kadri utakavyozoea kujisukuma kufanya mambo nje ya yale uliyozea yaani kutoka
kwenye ‘Comfort zone’ kwa mazoea
uliyozea, utazidi kujiweka kwenye mafanikio. Kama unaona mambo yako ni magumu
jisukume vivyo hivyo kuyafanya hadi kufikia mafanikio makubwa.
Hizo
ndizo hatua unaweza kuchukua kwa sasa kufikia utajiri. Jiwekee malengo ya
kufikia utajiri wako bila kuacha. Ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila
wakati. Waalike wengine waweze kujifunza kupitia makala tunazotoa hapa.
Ni
wako rafiki katika kuyasaka mafanikio ya kweli,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Axante xana kwa Elimu
ReplyDeleteAhsante kwa elimu
ReplyDelete