google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 11, 2015

Kanuni 4 Za Kufikia Mafanikio Makubwa.

No comments :
Maisha tunayoishi yanaongozwa na kanuni. Kanuni hizi zinapotumika zinakuwa zinaleta matokeo makubwa kwetu kwa upande wa maisha yetu. Kanuni hizi kwa bahati mbaya au nzuri zinafanya kazi iwe unajua au hujui. Ikiwa utakuwa unazifanyia kazi kanuni hizi hata kama ni kwa bahati mbaya utake, usitake ni lazima utafanikiwa.
Mara nyingi kanuni au sheria hizi huwa zipo za aina nyingi, lakini ambazo zina manufaa makubwa kwetu. Uwe na uhakika unapoamua kuzitumia, unakuwa upo katika njia sahihi ya kuelekea kutimiza mipango na malengo yako makubwa uliyojiwekea. Kanuni hizi hazina ubaguzi kwa yoyote yule anayeamua kuzitumia ili kufikia mafanikio makubwa.
Kwa bahati mbaya wengi kati yetu tunakuwa hatuzijui kanuni hizi na kuishia kusema maisha hayana ‘fomula’. Kwa kuendelea kwetu kushikiria msimamo huo tusio na uhakika nao, tunajikuta maisha yetu yanakwenda hovyo kila kukicha. Kitu cha kujiuliza je, ni kweli kanuni za mafanikio zipo na zinafanya kazi? Jibu hapa ni NDIYO.
Kwa haraka haraka tuangalie baadhi ya kanuni hizi za kimafanikio ambazo zinawezo wa kututoa pale tulipo na kutupeleka eneo lingine kimafanikio.
1. Weka nguvu za uzingativu katika eneo moja.
Hakuna uchawi katika hili unaoweza kujitokeza hapa. Kama ni kweli umeamua kufanikiwa, weka nguvu zako nyingi katika kile unachokifanya. Kwa kuweka nguvu na uwezo wako wote kwa lile jambo unalolifanya utakuwa unajihakikishia mafanikio makubwa katika maisha yako bila kupingwa na kitu chochote.
Mafanikio yoyote makubwa mara nyingi yanaanza kwa kuweka nguvu zote na uwezo wako wote sehemu moja kwanza. Hii ndiyo kanuni mojawapo rahisi ya kuweza kufikia mafanikio makubwa unayoyataka na kuwa mtu wa tofauti kabisa. Acha kujihusisha na mambo mengi sana. Fanya jambo moja na matokeo yake yatakuwa makubwa kwako.

2. Weka juhudi kila siku bila kuchoka.
Kitu pekee kitakachokuokoa kutoka kwenye shida, matatizo na ugumu wa maisha ulionao ni kujiwekea juhudi endelevu katika maisha yako bila kuchoka. Haijalishi unafanya kitu gani siku zote weka mkazo na juhudi zako nyingi kwenye kile unachokifanya na matunda yake utayaona. Hakuna kitu utakachokipoteza kutokana na wewe kujiwekea juhudi, zaidi utakuwa bora zaidi kila siku.
Watafiti wa masuala ya mafanikio wanadai kuwa ili uweze kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa unahitaji muda wa saa 10, 000 kuwekeza nguvu zako kwa kufanya kitu kilekile. Hiyo yote inaonyesha jitihada za lazima zinahitajika ili kufikia mafanikio ya kweli. Hakuna mchezo, wala hakuna bahati katika mafanikio zaidi ya kuweka juhudi kubwa mpaka kufikia malengo yako.
3. Fanya kazi zako kwa ubora wa hali juu sana.
Kuweka juhudi peke yake haitoshi, lakini unatakiwa kukumbuka pia kwa chochote kile unachokifanya kifanye kwa ubora wa hali juu kuliko kawaida. Acha kuwaza au kufikri kwamba kuna muda wa ziada ambao utaupata kukifanya tena. Utafanikiwa na kupata malipo yako kutokana na uthamani wa kile kitu unachokitoa kwa wale wanaokuzunguka. Acha kujidanganya na kufanya mambo yako kwa kulipua hiyo haitakusaidia kitu.
Wekeza juhudi na maarifa yako yote katika kutoa thamani inayohitaji kufikia mafanikio makubwa. Kama ni biashara ifanye bishara hiyo kwa ubora wa hali juu ukizingatia suala zima la kutoa huduma bora kwa mteja. Na katika maeneo mengine, fanya hivyo hivyo utaona mafanikio makubwa yakijitokeza siku hadi siku kwa upande wako.
4. Pima matokeo ya kile unachokifanya.
Acha kuthubutu kufanya kazi moja kwa moja tu bila kufika sehemu na ukaanza kupima matokeo ya kile unachokifanya. Ni lazima ukafika sehemu na ukatambua umuhimu wa kuangalia kule unakotoka na kule unakokwenda. Hiyo itakuwa ni njia rahisi ya kuweza kukusaidia kutambua wapi ulipo na wapi unapokwenda.
Kama kutakuwa kuna sehemu umekosea itakuwa ni rahisi kwako kuweza kurekebisha makosa hayo na kuweza kusonga mbele. Kwa hiyo kupima matokeo ni kanuni ya muhimu kwako kuitumia kama njia ya kufikia mafanikio yako makubwa. Ni lazima ifike mahali ukapima matokeo iwe kwa siku, juma au mwezi.
5. Andaa akili yako kwa ajili ya mafanikio.
Inaweza ikawa ni kazi ngumu sana kwako kuweza kufikia mafanikio makubwa kama utakuwa ni mtu mtu ambaye unaishi bila kuandaa akili yako kwa ajili ya mafanikio hayo. Katika mchezo wowote ni lazima unakuwa una maandalizi ya kutosha ili kushinda. Pia katika mafanikio maandalizi ni muhimu sana, vinginevyo kushindwa inakuwa rahisi na lazima kwako.
Kitu unachotakiwa kufanya ni kuweza kuiandaa akili yako na kutambua kuwa kuna kukosea hapa na pale, kukabiliana na mawazo hasi au hofu unazokuwa nazo. Ukishajua hayo yote yapo ni lazima kwako kuweza kujifunza kila siku juu ya mafanikio, kama sehemu ya maandalizi ya akili yako ili kufanikiwa kwa kiwango cha juu.
Ni rahisi kujenga mafanikio makubwa unayoyataka ikiwa utazingatia kanuni hizo. Kitu cha kuafanya ziweke kwenye matendo na jipe muda wa kuwezakubadili maisha yako mara moja. Mafanikio yote unayoyahitaji utayapata hatua kwa hatua.
Ninakutakia siku njema na ushindi katika safari yako ya mafanikio. Kwa elimu na maarifa bora endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,
dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.