Nov 11, 2016
Chanzo Cha Kufa Kwa Biashara Nyingi.
Sababu ya kuanzisha biashara yeyote
ile ni kuifanya biashara hiyo ikue kadri siku zinavyozidi kwenda na si kufeli.
Mitazamo hasi ambayo imekaa katika halmashauri zetu za ubongo ndizo
zinazotufanya biashara zetu kuanza kusua sua na hatimaye kufa kabisa.
Wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao
pindi biashara zao zinavyokwenda kombo, wao huamini ya kwamba wamelogwa na
sababu nyinginezo nyingi kama hizo. Hivi hujawahi kukutana na mfanyabiashara
ambaye anatamka kauli kama "hapa
lazima patakuwa na chuma ulete?”
Au hujawahi kusikia mfanyabiashara
pale ambapo biashara haiendi sawa akisema hapa ni lazima patakuwa na mkono wa
mtu? Bila shaka nadhani utakuwa umewahi kukutana na aina hii ya watu na kama
hujawahi kukutana nao basi huenda ukawa ni wewe mwenyewe.
Lakini nikwambie mfanyabiashara wa
kweli hamini katika nguvu za kishirikiana bali yeye huamini katika uwepo wa
Mungu katika kukamilisha mipango na mikakati ambayo mwanadamu ameipanga. Hata
hivyo kwa kwa kuwa wewe mtazamo wako ni chanya katika biashara nataka kukupasha
mambo ambayo kama utayafanya uwe na uhakika biashara yako itakufa.
Twende sambasamba kwa kuangalia sababu
za kufa kwa biashara nyingi:-
a) Tamaa za kuhamisha biashara kutoka sehemu moja
kwenda sehemu nyingine huku ukiamini kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kukua
kibiashara kumbe kinyume chake biashara hiyo inakwenda kufa kabisa.
Naomba nielewe vizuri juu ya maelezo
haya, si kwamba kuhama kibiashara ni kosa, la hasha si kosa, ila litakuwa kosa
endapo utashindwa kufanya uchunguzi wa kutosha wa kibiashara katika eneo ambalo
unategemea kufanya biashara
Katika kufanya uchunguzi wa eneo
ambalo unataka kufanya biashara ni lazima ujiulize baadhi ya maswali ya msingi
ambayo nitayaekeza kwa uchache hii ni kutoka kalamu yangu siku ya leo kuwa na
wino mchache hivyo nahofia itaisha na nikashindwa kuleta ujumbe wangu kwako.
Naomba nikueleze kwa uchache ni nini
ambacho unatakiwa kufanya kabla ya kuhama eneo moja kwenda jingine kibiashara;-
Fanya uchunguzi wa kutosha kuhusu
wateja wako wanataka nini haswa? Ukipata majibu kutakusaidia kuweza kukata kiu
ya wateja hao na hatimaye kupata fedha.
Chunguza kuhusu washindani ambao wapo
katika eneo hilo ambalo unataka kufanya biashara.
Tambua vyazo vyao vya mapato. Kufanya
hivi kutakusadia kujua, je ni biashara gani ambayo unataka kufanya ambayo
wateja watamudu kununua bidhaa au huduma hiyo.
Hayo ni baadhi ya machache kati ya
mengi ambayo ni vyema akajiuliza kabla ya kuamua kuhama kwenda kufanya biashara
sehemu nyingine.
b) Kukosa soko la uhakika.
Watu hufanya biashara kwa kutokuzingatia
na kujua biashara wataifanya vipi, unakuta mtu analima mazao ya kibiashara
lakini baada ya kuvuna ndo anaanza kutafuta wateja. Hili ni suala ambalo
litakufanya biashara yako ife tu. Kwahiyo ili kuepukana na adhaa hiyo unatakiwa
kuanza kutengeneza mazingira mapema ya kuwatafuta wateja.
Au ili kuweza kupata soko la uhakika
unachotakiwa kufanya ni kusoma alama za nyakati, pale ambapo unaona uhitaji wa
bidhaa au huduma ni mkubwa ndipo na wewe unatakiwa kuanza kufanya biashara
hiyo.
c) Kuongeza kwa washindani kibiashara.
Watu wengi biashara zao hufa kwa
sababu ya kwamba kuna wafanyabiashara wengi ambao wanafanya biashara kama yao.
Hivyo kuna baadhi ya wafanya biashara hukata tamaa na kuona hawewezi kushindana
na wafanyabiashara hao.
Ila nikwambie ya kwamba kuwepo kwa
washindani wengine kusikuumize kichwa na kuanza kufikiria hata kuacha kufanya
biashara, bali unatakiwa kuwaza na kufikiri ni jinsi gani unaweza kuwa bora
zaidi.
Ubunifu unahitajika ili kuwa bora
zaidi. Ongeza thamani katika biashara. Kwa mfano unaweza kuweka hata punguzo
fulani, kufanya hivi kutakufanya wateja wasikuhame, pia kufanya hivyo kutafanya
ongezeko la wateja kwani wateja tuna kasumba ya kuambiana kuhusu uzuri na ubaya
wa mfanyabiashara fulani.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ndimi afisa mipango, Benson Chonya
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.