Nov 8, 2016
Siri Ya Kujua Kanuni Za Asili Za Mafanikio.
Kama
ambavyo mara nyingi tumekuwa tukisema, maisha tunayoishi yanaongozwa na kanuni
zake. Na kwa bahati mbaya au nzuri uwe unazijua au huzijui kanuni hizo,
zinafanya kazi wakati wote katika maisha yako na zitakupa matokeo.
Na
kila mtu ana uhuru wa kuchagua kutumia au kutotumia sheria za asili za mafanikio.
Uchaguzi wowote utakao uchagua ni lazima ukupe matokeo, haijalishi ni chanya au
hasi. Lakini, hakuna mtu ambaye ataweza kukwepa matokeo ya kutumia au kutotumia
kanuni za mafanikio.
Kwa
kujua umuhimu wa kanuni au sheria hizi katika mafanikio, tutaanza kujifunza
baadhi ya kanuni za asili za mafanikio na kuona jinsi ambavyo zinasaidia
kutufanikisha katika maisha yetu.
Watu
wenye mafanikio wanatumia kanuni hizi za asili za mafanikio kuweza
kuwafanikisha. Ni kanuni ambazo hazibagui, ni lazima zikupe matokeo iwe
umezitumia au hujazitumia.
Kanuni
hizi za mafanikio si wengi sana wanaozifahamu, ingawa zipo katika maisha
yetu kila siku na zinatoa matokeo kila kukicha.
Mara
nyingi ikiwa unaishi nje ya kanuni hizi, ni rahisi sana kuanza kuona maisha
yako kama hayasogei kwa kiasi kikubwa. Kunakuwa kuna ugumu fulani hivi kwenye
maisha yako, ambao hata wewe unakuwa hujui unatokana na nini.
Kwa
hiyo, utakapojifunza na kuzijua sheria hizi na kuzitumia, utafurahia jinsi
maisha yako yatakavyokuwa yakieenda kwa wepesi ambao hata hukitarajia mwanzoni.
Mambo
ambayo yalikuwa yakikupa hasira sana, utashangaa hayakupi tena hasira.
Wasiwasi
uliokuwa nao utashangaa ukipungua na kutoweka.
Woga
wa mambo mbalimbali ikiwemo pamoja na kuthubutu pia utakutoka na kuwa mtu wa
vitendo.
Hata
pia utaweza kujihakikishia mafanikio makubwa, ikiwa utazifanya sheria hizi kuwa
sehemu ya maisha yako.
Hayo
yote yatatokea si kwa bahati mbaya wala muujiza, bali ni kwa sababu sheria au
kanuni za mafanikio zinakuwa zipo kazini.
Kanuni
hizi, ambazo tutakwenda kuziangalia moja baada ya nyingine yaani kanuni za
asili za mafanikio, ni vyema tukajua nini maana yake? Yaani Tunapozungumzia
kanuni za asili za mafanikio tunamaanisha nini?
Kanuni
za asili ni mfumo au taratibu unaoendesha maisha bila kufuata taratibu za jamii
yoyote. Mfumo au utaratibu huu upo wakati wote, ni mfumo ambao upo kama kiroho,
ni mfumo ambao hauonekani kwa macho haya, lakini unafanya kazi vizuri tu, ndio
maana zinaitwa kanuni za asili za mafanikio yaani ‘Universal Laws’.
Kwa
hiyo, tutaanza kujifunza kanuni mbambali za mafanikio kadri muda
utakavyoturuhusu. Kati ya kanuni za asili za mafanikio tutakazokwenda
kuzangalia ni pamoja na kanuni ya asili ya karma, kanuni ya asili ya kusamehe,
kanuni ya asili ya uvutano na nyinginezo nyingi.
Kwa
leo tuishie hapa, tukutane wiki lijalo siku kama hii ya leo, kuanza kuangalia
kanuni moja baada ya nyingine ili zikupe msingi mkubwa wa mafanikio yako.
Nakutakia
kila la kheri na ushindi katika kufikia mafanikio yako.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.