Nov 3, 2016
Kilimo Cha Papai.
Papai ni moja ya tunda
mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza
kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia
linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.
Uzalishaji wa papai nchini
Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo
inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.
Kijinsia mpapai umegawanyika
katika aina tatu
i) Mpapai wenye maua kiume
tu.
ii) Mpapai wenye maua kike
tu.
iii) Mpapai wenye maua ya
jinsia zote (Hermaphrodite papaya).
Katika uzalishaji kila
aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika
urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua
ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha
wenyewe.
Kutokana na jinsia ya maua
mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa
kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au
yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote
mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI.
Miche ya mpapai Katika
uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika:
1.
Mbegu za Kawaida (Local seeds).
Hizi ni mbegu ambazo
huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu
kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote.
Hivyo itakulazimu kung'oa
baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye
jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya
mipapai yenye maua ya kike.
2.
Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri
kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaja
(Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao
mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1 au MALAIKA F1.
UPANDAJI.
Panda mbegu moja tu kwa
kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha
weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya
kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide &
Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea
wako.
Mbegu ya papai uweza
chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia
maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa
toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.
KITALU
CHA MIPAPAI NA BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI.
Mpapai upendelea zaidi
udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5.
Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye
magadi. Kiasi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa
matunda.
Eneo lenye udongo wenye
unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yaliyoja maji maji na eneo
lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu. Mpapai hawezi
kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.
UANDAAJI
WA SHAMBA.
Njia ya kuandaa shamba
itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia
shamba. Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na
mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.
Andaa mashimo yenye upana
na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya
udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza
udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa
chini wakati wa kuchimba shimo.
Kiasi cha mmea huwa kati
ya 1000 hadi 2000 kwa hekta (400 hadi 800 kwa ekari) Kupanda mimea shambani Baada
ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa
mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia
madhara ya jua kwa mimea.
UWEKAJI
WA MBOLEA.
Zuia matumizi ya mbolea
zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya
kuhamisha miche yako weka mbolea gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye
phosphate kwa kaisi kikubwa.
Mfano; - 12:24:12. (NPK)
Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi
kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK) Potassium
inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi
kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114
cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2
(NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron
kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.
UMWAGILIAJI.
Maji ni sehemu ya muhimu
sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji ni ya muhimu sana katika
kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha
unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.
Magugu Hakikisha unazuia
magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa
virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza
kuathili mazao yako.
HATUA
ZA UKUAJI WA MPAPAI.
i) Kitalu - Wiki 1 - 6
-Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa.
ii)shamba - wiki 7 -16
-Maua na kuweka matunda.
iii) wiki 17 - 21 -Kukua kwa matunda.
iv) wiki 22 - 26 -Mavuno ya kwanza
v)Wiki 37 -kuendelea Week
37 ni miezi tisa au kumi sio kwa hiyo kilimo cha mapapai huchukua miezi 10 kupata
mavuno
GHARAMA
Kununua ekari moja inategemea
na eneo ulipo na bei husika.
Kununua mbegu tsh 50,000-100,000.
Kumwagilizia kila siku
-upandaji -kuhamisha kutoka kwenye vitalu hadi kwenye shamba -machine ya
kumwagilizia 1,500,000/-
Generator tsh lak 6
Mbolea tsh 100,000 kila
mwez -na vibarua shambani -kulima kwa trekta 40,000 Gharama zote kama mil 3-4
hiv mpaka kuvuna.
MAVUNO
NA FAIDA.
Kama umelima ekarI moja
unaweza ukapata matunda 15- 35 kwa mvuno wa Kwanza tu twende kimahesabu EkarI
ina miche 400-800 Tuseme tupate miche 600 kwa ekari, kila mche utoe matunda 20
chini kabisa 600×20=12,000.
Matunda Soko Kwa sasa unaweza ukauza kwa jumla jumla tsh 1500-3000 Tuuze kwa bei ya chini 1500 kwa kila papai 12000×1500=18,000,000/- Ukitoa Gharama za uendeshaji unaweza ukabaki na tsh 14,000,000 au toa 4,000,000 uweke kwenye dharura unaweza ukamake tsh 10 mil kwa ekar moja tu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.