Nov 16, 2016
Ifahamu Mipango Hii, Kabla Ya Kuanzisha Biashara.
Malengo ni lazima yaende sambamba na
mipango ili kuweza kutimiza ndoto zako kibiashara, hata hivyo huenda ukawa
haujanielewa, ipo hivi, mipango ni mtiriko wa namna ya kuyafikia malengo.
Pia malengo ni lazima yaanze katika
ngazi ya chini kabisa, hapa nikiwa na maana ni lazima uanze na malengo madogo
madogo au watalaamu wa masuala ya mafanikio huita (baby step).
Malengo ya kibiashara ni njia sahihi
ya kufanikiwa kwako kibiashara, kuna baadhi ya watu wao hufanya mambo ambayo
hayana mipango na mikakati ambayo itawasababisha kuweza kutimiza ndoto zao
ambazo wamejipangia katika masuala mazima ya kibiashara.
Na kufanya hivyo ni sawa na kutwanga
maji kwenye kinu, kwani kila siku utajiona ni mnyonge, huna faida za kuendelea
kuishi, hufai hii ni kutoka na kutoiona faida yeyote katika biashara ambayo
unaifanya.
Yafutayo ni maswali muhimu ambayo ni
muhimu kujiuliza katika upangaji wa malengo ya uanzishaji kibiashara.
1. Eneo kwa ajili ya kufanyia biashara.
Kuanzisha biashara mpya ni sawa na
kununua nguo mpya dukani, kama ndivyo hivyo huna budi kila uwapo dukani ni
lazima uangalie nguo ambayo itakutosha vizuri, kwani kama itakuwa hakitoshi na
ukainunua hautaitumia na mwisho wa siku utajilaamu hata kudiliki kusema
biashara hii nimechezea pesa zangu na meneno mengine mengi kama hayo.
Kama ndivyo hivyo basi kama ilivyo
kwa ununuaji wa nguo, basi hata katika biashara ni lazima ufikirie ni wapi
ambapo unataka kufanya biashara hiyo, baada ya kufikiria kwa umakini katika
kipengele hicho, jambo ambalo ni muhimu ambalo ni vyema ukalizingatia ni kwamba
ni lazima uende eneo hilo kwa ajili ya kufanya utafiti wa kutosha.
Nasisitiza sana suala hili la kufanya
utafiti kwani endapo hautafanya utafiti wa kutosha na ukaanzisha biashara eneo
hilo ni lazima utajikuta unaingia kwenye lile kundi watu walalamikaji ambao
husema wana gundu, wamelogwa, hawana akili za kibiashara na maneno mengine
mengi kama hayo.
Hivyo ili kuepuka na maneno hayo ni
lazima utafiti wa kutosha kuhusu eneo kwa ajili ya kufanya biashara ni lazima
ufanyike mapema na majibu yake yawe ya uhakika.
Zijue vyema gharama za mradi wako, kabla haujauanzisha. |
2. Gharama za mradi.
Sifa kubwa za mfanyabiashara ni
kuendelea kujiuliza maswali kila wakati, kama ndivyo inawezekana kabisa una
mpango wa kuanzisha biashara fulani hapo mbele lakini kutokana na kufanya vitu
vingi kimazoea unajikuta unashindwa kufanya tathimini ya gharama husika
biashara hiyo ambayo unataraji kuifanya.
Kutokana na changamoto hii ya kutojua
thamani ya mradi mzima hapa ndipo ambapo lile kundi kubwa la watu huibuka na
kuhoji eti afisa mipango nina shilingi milioni moja je, naweza kufanya biashara
gani?
Swali kama hili majibu yake yapo wazi
kwamba mtu huyo hana mawazo sahihi ya biashara na pia hajui thamani ya biashara
ambayo anaitaka kuifanya.
Lakini ukweli ni kwamba baada ya
kupata wazo bora la biashara na baada ya kujua ni wapi ambapo utafanya biashara
hivyo jambo tatu ni lazima ujiulize je ni gharama gani ambazo zitatumika
katika kuanzisha na kuendesha mradi mzima?
Kufanya tathimini ya mradi inakufanya
ujue ni wapi ambapo unaelekea. Pia watalamu wa mambo ya kibiashara wanazidi
kutukumbusha kwa kutuambia ya kwamba taswira tuliyonayo ya mafanikio ya
kibiashara hutupekeka pale tunapopataka.
3. Namna ya kupanua mipango ya kijasiriamali.
Katika hili mfanyabiashara yeyote ni
lazima ujihohiji je, anawezaje kupanua mipango ya kijasiriamaili. Hapa nikiwa
na maana ya kwamba upanuaji wa mipango ya kijasiliamali huenda sambamba na
kujifunza vitu vipya ambavyo vitakufanya uweze kukua kibiashara.
Kujifunza mambo hayo utajifunza
kupitia semina, makongamano, mikutano mbalimbali pamoja na kusoma ambapo
kimsingi utajifunza mambo yahusuyo biashara kwa ujumla.
Pia katika hili marafiki sahihi ambao
wanafanya biashara wana mchango mkubwa sana katika kufikia lengo lako. Pia kuna
usemi ambao unasema unaweza ukachagua marafiki ila huwezi kuchagua ndugu, hivyo
chagua marafiki sahihi.
Hivyo niweke nukta kwa kusema ya
kwamba maisha haya ni mazuri endapo utaamua kuchagua kile kilicho chema kwako.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya,
0757 90 99 42,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.