Nov 9, 2016
Panda Mbegu Ya Mafanikio Yako Leo.
Inawezekana upo kwenye
wakati mgumu sana kimaisha ukiwa huna pesa, mipango yako inakwenda hovyo na
huna uhakika hata hiyo kesho yako itakuwa vipi yaani ni kipi utakula na kipi
utavaa.
Kila njia unayowaza kwamba
inaweza kukuingizia kipato bado unaona pia nayo kama vile haikusaidii sana. Ukiangalia
kila mlango unaoufahamu wewe wa kukupa pesa kama haupo na hata wale wateja wako
umewapoteza.
Hali kama hizi ni hali
ambazo zinamkuta karibu kila mtu duniani. Kuna mahali katika maisha yako ni
lazima itafika utajikuta upo njia panda kwa sababu ya mambo yako kwenda hovyo hovyo.
Inapotokea hali kama
hiyo mifuko imechacha yaani huna mapesa, kitu kikubwa cha kufanya badala ya
kusikitika, anza kupanda upya mbegu ya mafanikio yako tena. Ni wakati wa
kuhakikisha unapanda mafanikio yako ili kesho uvune.
Kwa jinsi utakavyozidi
kupanda mbegu nyingi za mafanikio leo ndivyo utajikuta unavuna sana kesho. Kama
unalalamikia leo maisha yako ni magumu, hebu jiulize ulipanda nini unachotaka
kuvuna leo.
Tukiangalia hakuna
ulichokipanda. Kama hukupanda kitu, kaa kimya anza kuweka mikakati na mipango
yako upya ya kimaisha itakayokupa mafanikio makubwa kesho. Kila kitu
kinawezekana ukiamua.
Weka
mipango, mikakati yako vizuri leo ili kesho yako iwe ya mafanikio makubwa na
tabasamu. Tumia uwezo wako wote ulionao mpaka kufanikiwa. Ili usitumie njia ya
mkato ya kung’ang’aniza kuvunja ya ili utoe kifaranga nenda kwa taratibu na
UTAFANIKIWA. Usivunje kanuni.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.