Nov 15, 2016
Sheria Ya Mafanikio; Unapokea Kile Unachotoa.
Maisha
ya binadamu ni matokeo ya kile alichopanda au kukitoa katika maisha yake siku za nyuma.
Haijalishi upo katika hali ya mafanikio au kushindwa, haijalishi pia upo katika
hali ya afya au ugonjwa, yote hayo ni matokeo ya ulichopanda.
Sheria
ambayo inapelekea yale tuliyoyatoa au kuyapanda kurudi kwetu tena, sheria hii
inafahamika kama ‘Karma’ au ‘law of karma’. Ni sheria ya asili,
ambayo inaonyesha wazi kwamba kile unachokitoa, ni lazima utakipata.
Katika
sheria hii ya asili, inasisitiza sana kwamba chochote akipandacho mtu, mfano
wema, ubaya, upendo, ni lazima kitu hicho mtu huyo atakivuna iwe anataka au
hataki.
Mwasayansi
Isack Newton katika moja ya sheria zake aliwahi kusema, ‘every action must have reaction,’ Akiwa na maana kwamba katika
kila tendo/hatua, upo mrejesho wake, haijali ni mbaya au mzuri.
Hapo
utaona Isack Newton alitoa kitu kilekile kinachofanana na sheria ya asili ya ‘karma’ kwamba kwa chochote unachokipanda,
kwa chochote unachokitoa ni lazima ukivune.
Kama
hiyo iko hivyo, ni muhimu sana kwako kutambua mchago wa maneno, vitendo, maamuzi na
chaguzi tunazozifanya kila siku kwenye maisha yetu. Hayo yote kwa mujibu wa
sheria hii ni rahisi kuturudia kama vile tulivyotoa.
Kwa
hiyo kwa chochote kile unachokifanya leo, elewa kabisa unapanda mbegu ambayo utavuna
kesho. Kama hutaki matokeo mabaya na kupata kile ambacho hukipendi, jifunze
kufanya leo yaliyobora sana na ya manufaa.
Hakuna
binadamu ambaye yupo chini ya jua, anaweza kukwepa matokeo ya sheria ya 'karma.' Uwe unajua au hujui sheria hii matokeo ni lazima uyapate, kulingana na kile
ulichokipanda siku za nyuma.
Kanuni
au sheria hii, inatufundisha na kutumbukusha mambo kadhaa kama
ifuatavyo;-
1. Chochote
unachopanda kwenye hii dunia ni lazima utakivuna.
2. Maisha yako hapo hivyo si kwa bahati mbaya, bali ni matokeo ya mchango wako kwa
mambo fulani uliyowahi kuyatoa kipindi cha nyuma.
3.
Kwa mabadiliko yote unayoyataka, ni muhimu kuanza kubadilika wewe.
Usipobadilika wewe hakuna ambacho unaweza kukifanikisha kwenye maisha yako.
4.
Chochote kile ambacho kinakwenda hovyo kwenye maisha yako, chanzo kikubwa ni wewe.
Hapa sheria ya 'karma' inatutaka kuwajibika kwa miasha yetu kwa asilima zote.
5.
Unapata au kufanikiwa kwenye maisha yako kwa kile ambacho umekifanyia kazi au
ambacho unakifanyia kazi katika maisha yako.
Kwa
kujiua sheria hii 'karma,' ni vyema ukawa makini na kile unachofanya kila
wakati, maana kitu hicho ni lazima kikuletee matunda yako, hata kama si leo
utavuna hata siku nyingine.
Kumbuka
sisi ni matokeo ya yale tunayo yafanya kila siku. Hakuna mtu ambaye amekuonea
kwa hicho unachokipata na wala hakijaja kwa bahati mbaya au nzuri, bali chanzo
chake ni wewe.
Endelea
kujifunza kuptia DIRA YA MAFANIKIO kila siku, tukutane wiki ijayo kuweza
kuangalia aina nyingine ya sheria ya asili ya mafanikio ambayo itabadilisha maisha yako.
Nikutakie
siku njema na mafanikio mema.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.