Nov 17, 2016
Unahitaji Mambo Haya Manne Basi, Ili Kutimiza Malengo Yako.
Siku
zote hakuna uchawi au miujiza mkubwa sana unaotakiwa uwe nao ili uweze kutimiza
ndoto zako. Suala la kutimiza ndoto zako ambazo umejiwekea mara nyingi linakuwa
lipo mikononi mwako.
Ki vipi
hili linawezekana? Na hapo inakuwaje kuwaje? Sikiliza, utaweza kutimiza ndoto
zako ikiwa unajua misingi au mambo ya muhimu yatakayokusaidia kutimiza ndoto
hizo. Hapo ndipo ilipo siri ya kutimiza ndoto zako.
Najua
una hamu na shauku kubwa sana ya kutaka kuona ndoto zako zinatimia na kuwa
kweli. Kama hiyo iko hivyo usiwaze sana na wala hilo lisikupe shida. Je, unajua
ni mambo gani unahitaji ili kutumiza ndoto zako?
Unahitaji
mambo haya manne basi, ili kutimiza malengo yako.
1. Kukijua vizuri kile unachokitaka.
Kuna
wakati wengi wanaanza kutafuta safari ya mafanikio pasipo kujua vizuri hasa,
kile wanachokitaka. Huwezi kufanikiwa kama hukijui vizuri kile kitu unachokitaka.
Kwa
mfano nikiulize, wewe binafsi hapo unakijua vizuri kile unachokitaka katika
maisha yako? Je, unajua baada ya miaka miwili au miaka mitano unatakiwa uwe
wapi kimafanikio? Ni lazima ukijue unachokitaka.
Inapotokea
hata wewe mwenyewe binafsi hukijui vizuri kile unachokitaka, si rahisi sana
kufanikiwa. Siri kubwa ya kufikia ndoto zako na kufanikiwa ipo kwenye kukijua
vizuri kile unachokitaka.
Tekeleza ndoto zako kila siku. |
2. Kuwa na sababu.
Kukijua
tu kile unachokitaka, hiyo pekee haitoshi, ni lazima uwe na sababu. Lazima ujue
kwanini umejiwekea hayo malengo? Kwanini unataka kufanya hicho unachotaka
kufanya?
Unapokuwa
na sababu za kujua kwa nini unafanya hicho unachotaka kufanya hiyo inakuwa ni
motisha na nguvu ya kuweza kukusaidia kuweza kusonga mbele. Kila unapokumbuka
sababu za kufanya hicho unachofanya, hata kama umechoka ni lazima utaamka na
kwenda kupiga kazi.
Wewe
tafuta sababu kwa nini unafanya hicho unachokifanya sasa? Kama huna sababu,
elewa tu ni lazima kwa sehemu utakuwa ni mzembe sana na hutaweza kufikia
malengo yako. Nguvu kubwa ya kufanya zaidi, utaipata ukishakuwa na sababu ya
kufanya hicho unachokifanya.
3. Fanya kila siku.
Ndoto
zako huwezi kuzifikia ikiwa hutaweka juhudi ya kufanya kila siku. Ni lazima
kuweka juhudi na kufanya kila siku hata kama kipo kipindi ambacho unakuwa
umechoka.
Kwa
jinsi unavyofanya kila siku, juhudi zako zitakwenda kuweka matunda. Watu waliofanikiwa,
kila siku wanajitahidi kuweka juhudi zao kila siku hadi kutumiza ndoto zao.
Kitu
unachotakiwa kujiuliza, je, upo tayari kupiga kazi kila siku hata kama kuna
wakati unakuwa umechoka? Ikiwa utafanya hivyo, anza kujijengea uhakika mkubwa
wa kufikia ndoto zako.
4. Tafuta msaada.
Si
vyema sana ukakomaa na ndoto zako peke yako, wakati upo uwezekano wa kutafuta
msaada kwa wale waliofanikiwa kwa hicho unachokifanya. Jifunze kutoka kwao na
waulize nini siri ya mafanikio yao.
Acha
kuwa mbinafsi na kukubali kufa na tai shingoni kama mjerumani. Watu wenye
mafanikio wana hulka na tabia ya kuuliza kwa wale waliowazidi kwa yale
wanayoyafanya bila shida yoyote.
Ukianza
leo kuuliza na kutafuta msaada juu ya ndoto zako, utafika mbali sana
kimafanikio , tofauti na ambavyo ungebaki kimya kimya. Anza kubadili fikra zako
na kuwa na mtazamo wa tofauti ili uweze kutimiza ndoto zako.
Kila
wakati zingatia hivi, kukijua vizuri kile unachokitaka, kuwa na sababu juu ya
ndoto yako, kutekeleza ndoto zako kila siku na kutafuta msada kwa wale
waliofanikiwa, ni nguzo kubwa sana ya kukusaidia kufanikiwa kwa ndoto na
malengo yako.
Nakutakia
ushindi katika kufikia mafanikio yako makubwa.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.