Nov 4, 2016
Matatizo Yanayosababishwa Na Kuahirisha Mambo.
Kuahirisha
mambo, ni jambo ambalo hufanywa sana na karibu kila mtu katika maisha yake.
Utakuta kitu ambacho kilitakiwa kifanyike leo, kinasogezwa mbele hadi kesho au
siku nyingine.
Hali
hii huonekana ni kitu cha kawaida na yamekuwa mazoea ya wengi kuahirisha mambo
bila sababu yoyote ile. Kwa bahati mbaya sana, pamoja na wengi kuahirisha mambo
yao, lakini hata hivyo wanakuwa hawajui madhara makubwa yatakanayo na
kuahirisha mambo.
Moja
ya madhara makubwa yanayosababishwa na kuahirisha mambo ni msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unakuja
kutokea hasa pale kazi ambayo ulitakiwa kuikamilisha mapema sasa inakuwa
inahitajika.
Kwa
mfano, unaweza ukawa umeajiriwa na bosi wako akakupa kazi fulani. Ukishindwa
kuifanya kazi hiyo kwa muda na kuahirisha sana, siku ikitakiwa ni lazima
utapata msongo wa mawazo na kujiuliza sana ufanyaje ili kazi hiyo ikamilike.
Mbali
na msongo wa mawazo tatizo lingine ambalo unaweza ukakumbana nalo kwa sababu ya
kuahirisha mambo yako ni kupoteza furaha. Hauwezi kuwa na furaha hata kidogo
kama kitu ulichotakiwa kukamilisha, hakijakamilika na kinatakiwa kwa kwa
haraka.
Ni
lazima ndani yako utakuwa na wasiwasi mwingi kwamba jambo hili au kazi hii
haijakamilika na muda umekwisha sasa hapo nafanyaje fanyaje? Maswali mengi kama
hayo ni lazima yatakupotezea furaha yako ya moja kwa moja.
Pia
ikiwa utakuwa unaahirisha mambo mengi sana, upo uwezekanao mkubwa wa wewe Kutokufanya
kazi zako kwa kwa usahihi. Kazi nyingi ambazo mara nyingi zinafanywa muda ukiwa
umebaki kidogo huwa hazifanyiki vizuri, zinakuwa ni kazi za kulipua lipua.
Kwa
kifupi, hayo ndiyo matatizo yanayosababishwa na kuahirisha mambo mara kwa mara
katika maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri
katika kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.