Feb 8, 2016
Siri Katika Kupata PESA Na MAFANIKIO.
Katika ulimwengu wa leo hakuna binadamu asiyetambua thamani na
umuhimu wa pesa. Pesa inathaminiwa hata na watoto wadogo. Ukimpa mtoto karatasi
na pesa halafu ukamwambie tupa zote atatupa karatasi atabaki na pesa.
Kila mtu anahangaika kuitafuta shilingi. Watu wanahangaika kwa waganga, Usiku na mchana
kuitafuta pesa. Pesa inatafutwa kwa njia ya halali na haramu jamani pesa! Pesa
ni nini? Mbona viko vingi duniani vizuri lakini pesa inaongoza kutafutwa na
kila mtu.
Duuh! pamoja na kutafutwa huku pesa na kila mtu lakini swali la
kujiuliza mbona wengi bado wanahangaika na hawaipati pesa? Mbona wengi wana
elimu lakini pesa hawana? Mbona wengi wana akili lakini pesa hawana? Nauliza
tena kwa nini pesa jamani?
Katika dunia kuna makundi manne ya watu wanaotafuta pesa ila
kundi moja tu ndio lenye mafanikio. Humiliki utajiri na uchumi wa 90% wa dunia.
Kundi hili ni la watu wachache sana ila ni watu pekee waliogundua siri ya pesa
na mafanikio.
TOA THAMANI, UPATE PESA. |
Hawa ni watu wanaoishi ndoto zao na kufuata mbinu za mafanikio
ambazo ziko katika siri za pesa na mafanikio. Nimekwambia Leo nataka kukupa
SIRI YA KUTAFUTA PESA NA MAFANIKIO, nataka nikuzindue kutoka kwenye
usingizi wa umaskini na leo uanze kukimbia mbio zako mwenyewe.
Unashangaa? Usitoe macho ndio ukweli usiopingika mafanikio ya
pesa yana siri yake waliofanikiwa wamezigundua na kuzifanyia kazi siri hizi.
Huwezi kuitafuta pesa kama pesa halafu ukategemea kupata pesa abadani asilani.
Unaweza kusema nawe maneno yako ndio nini kusema huwezi kupata pesa kwa
kuitafuta pesa kama pesa? Wakati watu wanafanya hivyo. Usiwe mbishi tulia
kwanza.
Iko hivi, katika pesa huwezi kupata pesa bila ya kubadilishana
na thamani ya kitu. Hizo zilikuwa zama za mawe na ujima sasa tuko katika karne
ya 21 ya sayansi na teknolojia. Hivyo mambo yamebadilika. Kisaikolojia na
maumbile ya binadamu kamwe huwezi kuwa na pesa nyingi au kumiliki utajiri mpaka
uvitumikie viumbe vya mwenye utajiri wa Mali na dhahabu.
Hapa najua wengi nimewaacha kidogo. Hapa maana yangu ni kuwa
huwezi kupata pesa mpaka utatue changamoto na matatizo ya viumbe wa Mwenyezi
Mungu (Watu). Hapa nadhani umenipata uzuri. Hii ndio siri ndio siri ya kwanza
ya utajiri na pesa. Ni lazima utatue matatizo ya watu ndipo watu hao wakupatie
pesa.Haijalishi ni maskini au ni wanyonge kiasi gani watakulipa pesa tu.
Anza na kutoa huduma watatulie changamoto walizonazo watakupa
pesa tu watake wasitake. Mfano wa kwanza chimba kisima cha maji watakuletea
pesa umekaa, waletee usafiri watakuletea pesa umekaa,Wajengee shule watakuletea
pesa umelala, walimie nyanya,mchicha, kitungu na mengineyo mengi watakuletea
pesa umelala ndani kwako.
Siri ya kwanza ya utajiri ni kutoa huduma watazame matajiri wote
duniani wanatoa huduma, wanatatua matatizo ya watu. Mtazame Bakheresa ameona
unahangaika na kukuna nazi akabuni kukuletea nazi ya pakiti ili umpe pesa. Naona
sasa mpaka hapo tunaenda sawa na siri ya kwanza ya kupata pesa na mafanikio, subiri
nikupe siri zingine bado zinakuja.
Siri ya pili ya pesa na mafanikio ni kuzalisha mali. Hapa
ndipo patamu watu wengi leo hii wanatafua eti pesa kwa kuwa mchuuzi wa biashara
ndogondogo wanaita mtaani kulangua. Unaenda kwa mzalishaji MKUBWA unanunua
kiasi unaenda kuuza ili nawe upate kuwa na pesa na umiliki utajiri.
Mweee hii ni kucheza na nyani shambani utavuna mabua shauri yako usije sema sikukuambia. Mzee wa nyundo kali
napita mie. Mwenye kusikia leo naasikie zalisha mali upate pesa uninunue mali
kupata pesa utachelewa sana na pengine ukaishia kupata za kubadilisha mboga tu.
Matajiri wakubwa wamegundua siri ya pesa ndio maana wanazalisha mali ili wapate
pesa.
Siri ya tatu ya utajiri na pesa ni kuwa na ‘Network’ nzuri ya watu. Watu waliofanikiwa wana marafiki bora katika
ushirikiano wao. Hawako tayari kuwa na marafiki wavivu, wakatisha tamaa na
wasio na ‘vision’ wala malengo na ndoto katika maisha yao. Huchagua watu wa
kwenda nao katika safari ya mafanikio. Naamini tupo pamoja.
Siri ya nne ya utajiri na pesa katika mafanikio ni kujifunza
kila siku. Matajiri na watu wenye pesa wanasiri ya kujifunza kila siku na
kujiendeleza. Wapenda kujua na kujifunza kila kitu hawana kujifanya wajuaji
hata kama kuna kitu wanajua hujifanya hawajui ili wajifunze zaidi.
Siri ya tano ya pesa na mafanikio ni ubunifu katika kuitafuta
pesa ni lazima uwe mbunifu katika kuitafuta pesa. Pesa haipatikani
kirahisi kwa wale wasiotumia ubunifu ila tu kwa wale wabunifu katika
kufikiri na kutenda. Ili upate pesa ni lazima uwe na ubunifu katika kufanya
kile unafanya iwe ni kilimo,biashara au ufugaji.
Kwa haya machache naomba kuishia hapa kwa leo tukutane tena katika
makala nyingine Mungu akipenda. Asanteni
kwa kunifuatilia wako katika kusaka mafanikio na utajiri Shariff H. Kisuda.
Ansante kwa kutembelea na kufatilia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Endelea kuwaalika na wengine wafaidike na makala tunazotoa hapa.
Tupo pamoja;
Shariff Kisuda aka Mzee wa Nyundo Kali,
Simu; 0715 079 993,
Email; kisudashariff@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
UTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
ReplyDelete(KWANINI USUMBUKE)(HACHA KUTANGATANGA)
NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843.
KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE
MIKOSI,
MABALAA,
JINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI. NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote