Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, November 3, 2015

Kama Unafikiri Ili Ufanikiwe Ni Lazima Uwe Na Elimu Kubwa, Unajidanganya Mwenyewe.

No comments :
Ni rahisi sana kuweza kuwaza kwamba hujafanikiwa pengine kwa sababu hukusoma, au hujafanikiwa kwa sababu huna elimu kubwa sana ambayo ingeweza kukupa mafanikio. Haya ni mawazo ambayo wengi wanakuwa nayo na kufikiri, elimu ni kila kitu bila elimu maisha hayawezekani. Ni fikra hizi hizi ambazo zimekuwa zikiwadanganya wengi na kuwarudisha nyuma kila wakati.
Ukweli wa mambo ulivyo ni hivi, elimu isiwe kisingizio kikubwa kwako cha kukufanya ukashidwa kufanikiwa. Mafanikio utayapata tu wewe mwenyewe ukiamua iwe hivyo kwako kwa kuchukua hatua huku ukiwa na nia dhabiti. Wapo wengi waliofanya mafanikio makubwa kwa kuwa na elimu za kawaida tu ambazo waliamua kuzitumia vizuri. Hiki ndicho kitu unachotakiwa kuwa nacho.
Je, unajua hawa na akina nani, waliopata mafanikio makubwa bila kuwa na elimu kubwa ya kutosha, na unaweza ukapata kitu cha kujifunza kutoka kwao?
1. Richard Braison.
Huyu ni mfanyabiashara na mwekezaji mkubwa Duniani. Yeye ni mwanzilishi wa makampuni ya Virginia ambaye chini yake yapo makumpuni mengine 400. Historia yake ya kuwa mjasiriamali ilianzia mbali hasa pale alipoacha shule akiwa na umri wa miaka 16 na kuanza biashara ya kuuza magazeti. Alifanya vizuri na kuendelea kusonga mbele na kuzidi kuwekeza katika maeneo mengine. Hadi sasa anakadiriwa kuwa utajiri alionao Braison unafikia zaidi ya dola bilioni 5 za kimarekani.
Lakini, ukiangalia maisha ya Richard Braison kwa ujumla, kilichomfanikisha na kumfikisha hapo si elimu kubwa aliyonayo bali ni nia na hamasa yake kufanikiwa. Yeye kwa kifupi hakusoma sana aliacha shule mapema na kuanza kujihusisha na ujasiriamali mapema. Safari yake hiyo ya ujsiriamali imemfikisha hapo na si elimu kama unavyoweza kufikiria. Hivyo elimu kwake haikumpa na mafanikio makubwa.

UNAWEZA KUFANIKIWA KWA ELIMU YAKO YA KAWAIDA.
2. Mark Zuckerberg.
Pia huyu naye ni mfanyabiashara kijana na ni tajiri ambaye anamiliki mtandao wa facebook. Kwa mara ya kwanza alianzisha facebook akiwa chumbani kwake akiwa anasoma chuo. Kutokana na mafanikio aliyoanza kuyaona ya kujitokeza kwenye biashara hiyo ya mtandao aliacha chuo alichokuwa anasoma na kuamua kujihusisha na biashara kikamilifu.
Leo hii tunapoongea facebook ni moja ya mtandao mkubwa sana wa kijamii uliopo duniani. Kutokana wa wingi wa watumiaji umemfanya Mark Zuckerberg kuwa moja ya mabilionea  wakubwa duniani tena akiwa kijana, ambapo utajiri wake unakadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 36 za kimarekani. Mafanikio yote hayo pia aliyapata kutokana na kujituma kwake wala si elimu kubwa.

DIRA YA MAFANIKIO
3. Michael Dell.
Bila sha wengi tunafaham au tunatumia kabisa  kompyuta inayofahamika kama Dell. Huyu ndiye mwanzilishi wake. Historia yake ya madiliko ilianza mwaka 1992  pale alipoamua kuacha chuo kikuu cha Texas na kuanza kujihusisha moja kwa moja na biashara ya kompyuta. Kwa muda mfupi tu alijikuta akitajwa na gazeti la Forbes linalojihusisha na habari za watu matajiri, kuwa ni miongoni mwa vijana matajiri.  Wakati huo Michael Dell  alikuwa na miaka 27.
Kwa sasa utajiri wake unakadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 19 za kimarekani. Kitu cha kujiuliza kwake je angebaki kule angeweza kupata mafanikio hayo makubwa? Yeye aliamua kutafuta njia ambayo aliiona ni sahihi kwake na ikamfikisha hapo alipo. Leo hii dunia nzima inafurahia ugunduzi wake huo alioufanya na kufaidi matunda yake.

4. John Mackey.
Hakuna ambaye aliyeweza kufikiri kwamba biashara chakula na matunda  kwa wakati ule ingeweza ikamfanya mtu akawa tajiri? Hiki ndicho kilichotoke kwa John Mackey na mchumba wake. Watu hawa walijikuta wakiacha chuo na kuanza kujihusisha na kuuza chakula na matunda kwa asilimia zote. Biashara yao ilikuja kukua na kuwa kubwa kiasi cha kwamba kuweza kuuza Marekani na Kanada.
Ilifika wakati John Mackey alistaafu kufanya kazi hiyo akiwa tajiri mkubwa kabisa. Pesa nyingi alikuwa amekusanya na alikuwa akiishi maisha mazuri na bora kabisa  ya kisasa. Kilichomfikisha hapo alipo ni imani ya kuwa ni lazima atafanikiwa na wala siyo elimu yake. Kama ni elimu aliachana nayo mapema na kuamua kujihusisha na biashara.

Kama nilivyoanza makala haya, unaweza ukawa umefikia ngazi fulani ya elimu na kuamiani kabisa kwamba, pengine hupati mafanikio makubwa mpaka ufikie ngazi fulani, hilo sio kweli kabisa. Itumie elimu kwako kama chachu ya kukufanikisha zaidi, lakini kama umeikosa isiwe sababu sana ya kukuzuia kwenye mafanikio yako.
Dira ya mafanikio inakutakia siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote. Na kumbuka endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment