Oct 28, 2016
Jinsi Ya Kudumisha Afya Njema Na Kuishi Maisha Marefu.
Katika
hali ya kawaida, hakuna mtu ambaye ana uhakika mkubwa wa maisha yake kwamba ni
lazima afike kesho. Muda na dakika yoyote ile unaweza kuachana na mwili wako na ukafa. Swala
la kufika kesho au kutofika huwa mara nyingi linabaki mikononi mwa Mungu
mwenyewe.
Pamoja
na kwamba binadamu huyo hana uwezo wa kujua kesho yupo au hayupo, lakini upo
uwezo wa kutambua kama binadamu huyo ataishi maisha marefu au mafupi.
Inawezekana unaanza kujiuliza maswali hilo linawezekana vipi? Tulia usiwe na wasiwasi nitakwambia.
Kwa
mujibu wa wataalamu wa afya wanadai kwamba, ikiwa binadamu ataishi maisha yake
ya kawaida bila kupata changamoto
nyingine za nje yake kama kugongwa na gari au
namna yoyote ile ya kukatisha uhai wake upo uwezo wa kujua maisha yake
yataishia wapi.
Vyakula vyenye mafuta sana ni hatari kwa afya yako. |
Wataalamu
hao wanatuonyesha viashiria ambavyo vinaonyesha kama ukiishi hivyo ni lazima
uishi maisha marefu. Mambo hayo au viashiria hivyo walivyotoa, ni matokeo ya
utafiti yaliyofanywa hasa kwa watu walioishi miaka 100 na kuendelea.
Kwa
mfano utafiti huo ulionyesha, watu wanaokula vyakula vyenye mafuta kidogo, watu
hawa wao waliishi maisha ya muda mrefu. Mara nyingi ni kweli unapokula vyakula
vya mafuta kidogo hiyo inakusaidia sana katika swala zima la mwili wako
kutopata magonjwa hovyo.
Pia
utafiti huo uliendelea na kuonyesha kwamba, watu wanaokula vyakula vyenye wingi
wa protini pia afya zao ziliimarika zaidi na kupelekea kuwa na maisha marefu. Vyakula
hivyo ni kama samaki, dagaa, maharage,
nyama ana vinginevyo.
Hata
hivyo pia watu wanaofanya mazoezi kila siku nao pia walionyeshwa kwamba
wanauwezo wa kuishi maisha ya muda mrefu kutokana na mazoezi huweza kuimarisha
afya na kupunguza baadhi ya magonjwa na hali za kunenepeana hovyo.
Hivyo
utaona, vyakula visivyo na mafuta sana, vyakula vyenye protini na kufanya
mazoezi ni mambo ambayo yametajwa na wataalamu yanaweza kuboresha afya yako na
kupelekea kuwa na uwezekano mkubwa sana wa kuishi maisha marefu.
Kumbuka
siku zote, afya ni kitu cha muhimu sana katika maisha yako na safari yako ya
mafanikio kwa ujumla. Kama ukiwa huna afya njema hakuna utakachokifanikisha
kwenye hii dunia. Ni muhimu sana kutunza afya yako kwa ajili ya mafanikio yako.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Pia
napenda kukukaribisha rafiki kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza
pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO
YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.