google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 7, 2016

Ukweli Kuhusu Pesa Utakaokufanya Uwe Tajiri Au Maskini -2

No comments :
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO katika makala iliyopita tuliona umhimu wa kuujua ukweli kuhusu pesa ili uweze kuwa na mafanikio.
Na moja ya kweli muhimu kuhusu pesa ambayo tulijifunza ni kwamba pesa yoyote unayoipata au uliyonayo ni ishara ya thamani unayoitoa kwa kile kitu unachokifanya.
Leo katika makala haya tunaendelea na kweli zingine ambazo ni lazima uzijiue kuhusu pesa. Pengine unajiuliza kwa nini nasisistiza ni lazima uzijue? Usipozijua kweli hizi ni rahisi sana kubaki kwenye  umaskini.

Tumia kanuni za pesa ili upate pesa.
Aina nyingine ya ukweli unaoatakiwa uujee kuhusu pesa ili uwe na mafanikio ni kwamba pesa ina kanuni zake. Katika hili hapa hakuna ubishi ili uweze kupata pesa ni lazima utembee kwenye kanuni za pesa.
Haijalishi mtu unayezitumia kanuni za pesa amesoma au hajasoma, ila ukizitumia kanuni hizo ni lazima zinafanye kazi na ufanikiwe. Na kanuni hizi za pesa mara nyingi huwa si ngumu sana ni rahisi tu.
Kwa mfano mojawapo ya kanuni muhimu ya pesa inasema kwa kiasi chochote cha pesa unachopata ni lazima kwanza ujilipe wewe asilimia kumi kama mtafutaji wake.
Sasa kwa kanuni kama hizi zinakuwa sio ngumu sana kuweza kutekelezeka kama kweli umedhamiria iwe hivyo. Kwa maana hiyo ni muhimu kujua kanuni za pesa ili ufanikiwe, usipozijua umaskini ni wako bila ubishi.
Pia ukweli mwingine unaolazimka kuujua kuhusu pesa ili usije ukaishia kwenye umaskini ni kwamba  thamani ya pesa inakwenda sawa sawa na muda.
Hiyo ikiwa na maana kwamba kama pesa yako unaiweka tu na hata bila kuiweka kwenye mzunguko wa pesa na ikakuzalishia ni rahisi kuweza kupoteza thamani yake.
Kwa kumalizia makala haya kumbuka tumezungumzia pesa ni ishara ya thamani, pesa ina kanuni zake na pia pesa thamani yake inapanda kulingana na muda. Hayo yote ni mambo muhimu sana ya kujua ili uweze kuwa na mafanikio.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.