Oct 14, 2016
Tabia 3 Za Watu Wanaokubalika Sana Na Jamii.
Katika
maisha bila shaka umewahi kuona watu wanaokubalika sana katika jamii yao. Kila ulipofatilia
mienendo yao ulikuja kugundua kwamba watu hao kila wanaloligusa katika maisha
yao ni kama linakubalika sana na wengi.
Pengine
ilifika mahali ukajiuliza mengi kwa kuwaza na kusema “ Mmmh inawezekana watu hawa ni Freemason na sio bure kwa nini wao tu
wanakubalika na sisi hapana?”.
Najua
unayo mifano mingi ya watu kama hawa ambao wanakubalika sana na jamii. Je, ulishawahi
kujiuliza ni kitu gani hasa ambacho kinasababisha watu hao waweze kukubalika
kwa jamii kiasi hicho?
Majibu
ya maswali hayo ya ni nini ambacho kinawafanya hadi wao wawe na mvuto mkubwa
unakwenda kuyapata kwenye makala haya. Je, unataka kujua ni nini kinachofanya
wawe ni watu wa kukubalika au wawe ni watu watu?
Hebu
fuatana nami katika makala haya kujifunza baadhi ya tabia zinazowafanya wawe na
mvuto.
1.
Tabia ya kujenga tabasamu.
Tafiti
nyingi zinaonyesha tabasamu ni kitu muhimu sana katika mahusiano yoyote yale
yawe ya kimapenzi au kawaida. Kwa mfano, tabasamu huwa ni kichocheo cha kuwavuta
wengi kusikiliza au kutambua umuhimu wa mtu anayetoa tabasamu hilo.
Pia
tafiti hizo zinaendelea kuonyesha kila unapotasamu inasaidia kuwasisimua
wengine kujaribu kukusikiliza. Hiyo ikiwa na maana kwamba hakuna mtu ambaye
anapenda kumsikiliza mtu aliyenuna nuna. Ni lazima uwe na tabasamu fulani ili
usikilizwe.
Kampuni
nyingi zenye mafanikio kwa kujua hili, ndio maana zimeajiri watu wenye nyuso za
bashasha au tabasamu pale mapokezi. Hivyo, Kama unataka kukubalika katika
jamii, jifunze namna ya kutengeneza tabasamu zuri litakalo wavuta wengine kwako.
2.
Tabia ya kusaidia wengine.
Mara
nyingi watu wanao kubalika na jamii kwa sehemu kubwa, ukiwachunguza utagundua
ni watu wa kusaidia watu wengine pia. Matatizo au changamto za jamii
huyachukulia kama yao. Hivyo kila wakati hushirikiana na jamii zao kuweza
kutatua yale yaliyo muhimu.
Kutokana
na tabia hiyo ambayo wamejijengea, huwasaidia sana kuweza kuwa watu waliokubalika
katika jamii kwa sehemu kubwa. Ni kitu ambacho hata wewe unaweza ukakifanya ili
kuweza kuvuta mvuto kwa jamii yako hasa unayoishi.
3.
Tabia ya shukrani.
Watu
wanaokubalika na jamii na kupendwa na wengi maisha yao yametawaliwa na shukrani.
Sio watu wazito sana kushukuru. Kila wanachokipata au pale wanaposaidiwa ni
rahisi kwao kuweza kusema ansante mara moja.
Kwa
kawaida shukrani yoyote haina gharama. Anza leo kujifunza kushukuru kwa mambo
madogo madogo. Wape shukrani ndugu zako waliokutembelea au hata yule aliekupigia
simu. Kwa jinsi utakavozidi kufanya hvyo itakusaidia kwako wewe uweze
kukubalika kwa jamii yako.
Zingatia
sana kwa kadri utakavyozidi kufanyia kazi tabia hizo, ndivyo utajikuta unakuwa
ni mtu wa kukubalika na kupendwa na jamii yako kwa sehemu kubwa.
Nikutakie
siku njema na ansante sana kwa kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. Usiache kuwashirikisha wengine waweze kupata maarifa haya bora.
Pia
napenda kukukaribisha rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga
tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha
ikifuatia na namba yako kwenda 0713 04 80
35 ili uanganishwe.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.