Oct 3, 2016
Tabia Tano (5) Za Muhimu Kwa Mjasiriamali Mwenye Mafanikio.
Kwa kawaida siri ya
mafanikio makubwa kwa mjasiriamali
yeyote yule ipo kwenye tabia zake. Tabia hizi ndizo ambazo zinazomtofautisha
mjasiriamali mwenye mafanikio na yule ambaye ana mafanikio ya kusuasua au hana kabisa mafanikio.
Hivyo kwa mantiki
hiyo, ni muhimu sana kwa mjasirimali
mwenye mafanikio makubwa kujijengea tabia bora zitakazo msaidia kuweza kufanikiwa.
Moja kati ya tabia hizo ambazo mjariamali anatakiwa kuwa nazo ili kufanikiwa ni
kama hizi zifuatazo:-
1. Kuamka asubuhi
na mapema.
Wengi
kati ya watu wenye mafanikio makubwa wamefanikiwa sana kujenga tabia hii ya
kuamka asubuhi na mapema. Huu ni muda ambao huwasaidia sana kutekeleza majukumu
yao ya muhimu mapema zaidi wakati watu wengi bado wakiwa wamelala.
Wanafanya
hivyo kwa sababu, hiki ni kipindi ambacho kinakuwa kimetulia na wala kuna kuwa
hakuna makelele ya hapa na pale. Mara nyingi muda ambao watu wenye mafanikio
hupenda sana kuamka ni kati ya saa kumi kamili hadi saa kumi na moja kamili
asubuhi.
Mipnago imara ni muhimu kwa mjasiriamali mwenye mafanikio. |
2. Mahusiano na
wengine (Networking).
Kati ya kitu muhimu
katika safari ya mafanikio ni mahusiano bora na wengine. Kwa kila mjasiriamli
mwenye mahusiano bora na watu wengine, inamsaidia sana katika kujipatia fursa mbalimbali
ambazo zinajitokeza karibu kila siku.
Ikiwa huna tabia ya
kujenga mahusiano mazuri na wengine ni ngumu sana kufanikiwa kama mjasirimali. Hiyo
iko hivyo kwa sababu utashindwa kushirikishwa mambo mengi ambayo ni fursa kwako. Kwa nini
hautashirikishwa? ni kwa sababu huna mahusiano mazuri na watu wengine.
3. Mipango.
Ukifatilia maisha ya watu
wenye mafanikio kwa ukaribu, utagundua ni watu wenye mipango. Si watu wa kuishi
tu kama bendera fuata upepo, bali ni watu ambao mambo yao wamejiwekea kwa
utaratibu na kuhakikisha wanayafanikisha kwa namna yoyote ile.
Hakuna
mtu wenye mafanikio makubwa akaishi kiholela bila kuwa na mipango imara. Jaribu
leo kujiwekea mipngo imara juu ya maisha yako, hiyo itakusaidia sana kuweza
kufika mbali kimafanikio baada ya muda fulani na utatimiza malengo yako.
4. Kusikiliza.
Mbali na kuamka
asubuhi na mapema, kuwa na mahusiano mazuri na wengine na kujiwekea mipango,
pia watu wenye mafanikio wana tabia moja muhimu ya kusikiliza. Hawa ni watu ambao
huwa si waongeaji muda wote bali pia husikiliza sana ili kujifunza.
Kusikiliza ni moja
ya tabia muhimu sana inayowajengea mafanikio. Mengi sana hujifunza kupitia
kusikiliza kuliko kuongeongea tu jambo ambalo lingepelekea kujua yale tu peke
yake wanayoyajua. Hata wewe kama unataka kufanikiwa ni muhimu sana kujijengea
tabia hii ya kusikiliza.
Kwa mjasiriamali
yeyote
mwenye mafanikio, huzingatia sana tabia hizo ambazo kwa sehemu kubwa humsaidia
kumfikisha kwenye kilele cha mafanikio.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI
NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.