Oct 21, 2016
Usiruhusu Makosa Haya Yawe Sehemu Ya Maisha Yako.
Yapo
makosa ambayo hutakiwi kuyaruhusu mara kwa mara kutokea katika maisha yako. Ni
muhimu kuzingatia hilo kwa sababu maisha tuliyonayo ni mafupi na kila hatua
inatakiwa tuifanye kwa uhakika ili tusipoteze muda sana.
Kumbuka hata
hivyo wengi wetu kuna wakati tunashindwa kufanikiwa sana kutokana na kuruhusu
makosa ya aina fulani yatokee sana katika maisha yetu. Makosa haya ndio yamekuwa
yakipelekea mipango mingine kuweza kukwama.
Je, ni
makosa gani ambayo hutakiwi kuyaruhusu katika maisha yako mara kwa mara ili
uweze kufanikiwa?
1.
Usiruhusu kutawaliwa na watu hasi.
Hata kidogo
usiruhusu kuweza kutawaliwa na watu hasi. Usiwape nafasi kubwa ya kuweza
kuwasikiliza. Ikiwa utafanya hivyo kuwaruhusu watu hasi, watakuharibia maisha
yako sana kwa kukupa ushauri wa kukatisha tamaa na mwisho utaona maisha
hayawezekani tena.
Acha kuruhusu woga utawale maisha yako. |
2.
Usiruhusu woga ukutawale.
Woga ni
sumu kubwa sana ya mafanikio yako. Acha kuruhusu woga ukatawale sana. Kwa wale
ambao huruhusu woga uwatawale kwa kiasi kikubwa hawafanikiwi. Hiyo hutokea hivyo
kwa sababu hata hushindwa kuchukua hatua za kujaribu kufanya jambo jipya kwa
sababu ya woga.
3. Usiruhusu
kuiga sana.
Inapotokea
ukawa unaiga sana kwa kawaida unaua ule ubunifu wako wa ndani. Hivyo kama
unaiga kitu uwe na mipaka, lakini lilokubwa kwako unatakiwa kuwa mbunifu sana
ili iweze kukusaidia kutengeneza mafanikio makubwa.
4.
Usiruhusu kufanya jambo usiloweza.
Kama kuna
kitu hukiwezi ni vyema usikifanye. Kukifanya kitu hicho huku ukiwa huwezi au
huna hakuna na matokeo chanya hiyo itakuharibia sana sifa na maisha yako. Kila
unapotaka kulifanya jambo fulani, hakikisha unalijua vizuri kwa undani ili
likupe mafanikio.
Hivyo ni
vyema ukatambua kwamba hayo ndiyo makosa ambayo hutakiwi kutokuyaruhusu sana yatokee ili uweze
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kama itatokea unaruhusu makosa hayo sana
maishani mwako, basi utakuwa unajitengenezea mazingira ya kushindwa mwenyewe.
Nikutakie
siku njema na ansante sana kwa kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. Kitu cha kufanya kwako, washirikishe
na wengine waweze kupata maarifa haya bora.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.