Oct 12, 2016
Mambo Muhimu Ambayo Hutakiwi Kuyapoteza Kwenye Maisha Yako.
Katika
safari ya mafanikio, kuna mambo ya msingi sana ambayo unatakiwa kuyalinda ili
uweze kufanikiwa. Ikiwa utakuwa unaishi kiholela na kuyapoteza mambo hayo iwe
kwa kujua au kutokujua ni wazi utashindwa kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kwenye
maisha yako.
Je,
wewe binafsi ulishawahi kujiuliza ni
mambo gani unayotakiwa kuyalinda kama mboni ya jicho lako ili yaweze kukusaidia
kufaniwa? Kama hujawahi kujiuliza hivyo, tambua yapo mambo unayotakiwa kuyalinda
sana ili yakusaidie kufanikiwa.
Bila
kupoteza muda fuatana nami hatua kwa hatua katika makala haya ili kuweza
kujifunza mambo muhimu ambayo hutakiwi kuyapoteza kwenye maisha yako kabisa.
1. Hutakiwi kupoteza mwelekeo.
Ili
uweze kuishi maisha ya mafanikio ni lazima uwe na mwelekeo maalumu. Ni lazima
ujue wapi unatoka na wapi unakwenda. Kujua mwelekeo wako sahihi ni jambo la
muhimu sana katika safari ya mafanikio yako.
Watu
wengi huwa ni watu wa kupoteza mwelekeo wa maisha yao hata kwa mambo madogo.
Kwa mfano, wapo ambao hupoteza mwelekeo wao kwa sababu ya kukosolewa, kushindwa
sana au changamoto nyingine za maisha.
Ongeza ushirikiano na wengine ili ufanikiwe. |
Kwa
bahati mbaya, kila unapokosa mwelekeo kumbuka huwezi kukua kimafanikio na
hakuna makubwa utakayoweza kufanya. Kukosa mwelekeo ni moja jambo muhimu sana la
kimafanikio unalolipoteza kwenye maisha yako.
2. Hutakiwa kupoteza ushirikiano na
wengine.
Mafanikio
uliyonayo yanatokana pia na mchango wa wengine. Sasa ili ufanikiwe hiyo
inamaanisha mchango wa wengine kwenye maisha yako ni muhimu sana.
Kama
unaishi peke yako bila ushirikiano mkubwa na wengine sio rahisi sana kufika
mbali kimafanikio. Unaweza kweli ukapata mafanikio lakini hayawezi kuwa makubwa
sana kama ungekuwa na ushirikiano na wengine.
Hivyo,
kati ya kitu ambacho hutakiwi kukipoteza kwenye maisha yako ni ule ushirikiano
mkubwa na wengine. Kila inapoitwa leo jitahidi sana kujenga mahusiano bora na
wengine ili ya kusaidie kujenga mafanikio makubwa.
3. Hutakiwi kupoteza kujitawala
mwenyewe.
Kati
ya kosa kubwa ambalo hutakiwi kulifanya kwenye maisha yako ni kule kupoteza au
kushindwa kujitawala. Kwa vyovyote vile ni lazima ujue namna ya kujitawala wewe mwenyewe iwe uweze kufanikiwa.
Kwa
mfano unatakiwa kutawala matumizi ya muda wako, pesa, tabia na wakati mwingine
hata kutawala nidhamu binafsi. Haya ni mambo ya msingi sana kuweza kuyatawala
ili kujihakikishia ushindi wa mafanikio.
Kwa
wengi wanaoshindwa kujitawala, hujikuta maisha yamewatawala na matokeo yake
huishia kuwa na maisha mabovu sana. Jenga msingi wako wa mafanikio kwa
kuhakikisha ni lazima umeweza kujitawala.
4. Hutakiwi kupoteza matumaini.
Zipo
changamoto nyingi sana ambazo tunakutana nazo kwenye maisha karibu kila siku.
Kuna wakati changamoto hizo hupelekea sisi kukata tamaa kwa yale mambo ambayo
tunayoyafanya.
Inapofika
wakati ukakata tamaa kwa sababu ya changamoto hapo unakuwa upo kwenye wakati
mgumu sana wa kutoka hapo. Kitu ambacho unatakiwa uzingatie, changamoto isiwe
kizuizi kikubwa cha kukufanya ushindwe kufanikiwa.
Na
wala usije ukakata tamaa kwa sababu ya changamoto yoyote ile. Kila wakati
unatakiwa kuwa na tumaini la mafanikio yako, hata wakati unapoona mambo yako
yamekuwa magumu na hayawezekani.
Kumbuka
kama tulivyojifunza ni marufuku kupoteza mwelekeo, ushirikiano, kujitawala na ni marufuku kupoteza matumaini. Hayo ni mambo ambayo hutakiwi kuyapoteza hata kidogo bali unatakiwa uyalinde na kuyakumbatia kila wakati
ili uweze kufanikiwa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda
pia kuchukua fursa hii kukukaribisha kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi.
Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU,
kisha ikifuatia na namba yako kwenda 0713
04 80 35 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.