Oct 6, 2016
Ukweli Kuhusu Pesa Utakaokufanya Uwe Tajiri Au Maskini.
Kwa
kawaida, ili uweze kupata pesa, mbali na kanuni za pesa, upo ukweli unaotakiwa
kuujua kuhusu pesa ili ufanikiwe. Kwa kuujua ukweli huu, unao uwezo wa
kukufanya ukawa tajiri au kwa kushindwa kuujua ukweli huu ni rahisi pia kuwa
maskini.
Ukiangalia
watu wanaofanikiwa kipesa kwa namna moja au nyingine wanajua kweli nyingi
kuhusu pesa. kwa upande mwingine, watu wengi wapo katika hali mbaya za kiuchumi
na kukosa pesa kwa sababu ya kushindwa kuijua pesa vizuri na kweli zake jinsi
zinavyofanya kazi.
Sasa
ili uweze kufanikiwa kwenye eneo la pesa zipo kweli tatu ambazo unatakiwa
uzijue na kuzifanyia kazi.
Kwanza,
ili uweze kupata pesa ipo thamani ambayo ni lazima uweze kuitoa. Hautaweza kupata
kiasi chochote cha pesa ikiwa hakuna thamani yoyote unayoitoa. Kwa hiyo kiwango
cha pesa ulichonacho kipo sawasawa na thamani unayoitoa.
Toa thamani kubwa, utapata pesa. |
Hebu
jaribu kufikiri moja ya matajiri wakubwa dunia, ni kitu gani wanachokifanya cha
ziada na ambacho kinawafanya wapate pesa? Ukichunguza utagundua ni thamani
kubwa wanayotoa kwa yale wanayoyafanya kila siku.
Kwa
mfano tukimuangalia kila mmoja wetu anaujua au anatumia mtandao wa ‘facebook’. Sasa, mmiliki wake ambaye ni
Mark Zuckerberg ni moja ya matajiri wakubwa sana duniani akiwa kwenye orodha ya
kumi bora kwa sasa. Ukiangalia ni nini kilichomfikisha hapo ni ile thamani
anayoitoa kwenye biashara yake.
Kila
kukicha watu wanapofurahia na kutumia ‘facebook,’
ndivyo ambavyo Mark Zuckernberg anazidi kuwa tajiri. Hiyo yote inaonyesha kwamba
pesa ni ishara ya thamani fulani inayotolewa. Hivyo ili uweze kupata pesa ni
lazima rafiki, uweze kutoa thamani kubwa kwa namna yoyote ile.
Kama
hujanielewa vizuri ngoja nikuulize swali hili? Hivi ulishawahi kujiuliza kwa
nini wale wote wanaoshinda bahati nasibu mara nyingi huishia kuwa maskini yaani
zile pesa zinakuwa kama hazijawasaidia kitu? Ama wakati mwingine pesa hizo
huonekana kama zina mkosi zimepotea tu kiaina?
Kama
hujawahi kujiuliza hivyo usipate tabu, jibu ni rahisi tu, ni kwa sababu pesa
walizopata haziendani na thamani waliyotoa, hivyo ni lazima zitapotea tu, hata
kwenye mazingira ambayo hayakutegemewa. Ni ngumu sana kuweza kutunza pesa
ambayo haiendani na thamani uliyotoa.
Hili
pia hutokea sana kwenye zile pesa za kupewa ambazo hujafanyia kazi, nazo huisha
sana kwa sababu kama hii. Kama unafikiri natania pita barabarani halafu mtu
akupe shilingi laki moja uone kama utadumu nayo sana, kwa wengi huisha mapema
mno.
Kwa
hiyo kila unapofikiria suala la kuongeza kipato, ili uweze kufanikiwa katika
hilo usianze kufikiria juu ya pesa. Fikiria ni namna gani jinsi unavyoweza
kuongeza thamani kwenye maisha ya watu na yale unayoyafanya. Kwa jinsi
utakavyozidi kuongeza thamani pesa itakuja tu kwako na hilo sio suala la
kuuliza.
Kumbuka
siku zote pesa ni ishara ya thamani. Kama hutoi thamani kubwa utapata pesa
kidogo. Matokeo hayadanganyi, kanuni za mafanikio hazidanganyi, labda wewe
udandanye kwa kukataa ukweli huu. Na ikiwa hautafanya hivyo kwa kutoa thamani
hiyo, itakuwa ni sawa na mtu kukimbia kivuli chake.
Je,
ni ukweli gani mwingine kuuhusu pesa unaotakiwa kuujua ili uwe tajiri? Fuatana
nami katika mwendelezo wa makala haya kwa siku ya kesho bila kukosa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.