Oct 11, 2016
Aina 5 Za Mafanikio Ambazo Ni Muhimu Kuzifahamu Na Kuziishi.
Hongera sana kwa kuchukua uamuzi huu
kuweza kusoma makala haya. Kimsingi ni kwamba siri kubwa ya mafanikio yako
ambayo unayahitaji ipo katika maandishi, unashangaa! Usishangae huo ndio ukweli.
Kila kitu ambacho unataka katika
dunia ya leo kipo katika maandishi, ndiyo maana mwanzoni nimesema hongera kwa
kuchukua uamuzi huu ambao umeufanya katika kusoma makala hii.
Hivyo nakusihi uendelee kusoma makala
haya mwanzo mpaka mwisho naamini utajifunza kitu ambacho kitakusaidia sana siku
ya leo endapo utaamua kuchukua hatua kwa kile ambacho utajifunza katika safu
hii.
Ukweli ambao hautaji mifano kutoka
kwa wazungu, ni kwamba mwanadamu yeyote ambaye anahitaji kufikia kilele cha
mafanikio yake anahitaji aina kumi za mafanikio ile kwa kuanza, nitaeleza aina
tano tu.
Nimeamua kuleta maada hii kwa sababu
wengi huamini ya kwamba kuwa na pesa ndio kufikia ndoto zao, lakini ukweli
halisi haupo hivyo. Kwa msingi huo, leo nitakuongeza kitu katika kujua ukweli
wa aina nyingine za mafanikio ambao mwanadamu yeyote yule ni lazima azifahamu.
Zifuatazo ndizo aina tano (5) za mafanikio ambazo ni lazima
uziishi;
1. Mafanikio ya kiroho.
Haya ni mafanikio nambari moja kwa
mwanadamu, watu wengi huwa wanasahanu ya kwamba mwanadamu yeyote yule ni lazima
awe na malengo ya kiroho ili kukamilisha aina hii ya mafanikio. Watu wengi
wamekuwa hawana ukaribu na aina hii ya mafanikio kwa sababu ambazo mimi ziwezi
kuzielezea ila wao watakuwa wanafahamu kwa undani zaidi.
Na endapo utafanya uchunguzi katika
kundi fulani la watu juu ya malengo yao ni asilimia chache sana ambao
watakwambia kuhusu malengo yao hasa katika upande wa masuala ya kidini na
kumuweka mwenyezi Mungu mbele, wengi tumekuwa tukiishi kama vile tumejiumba
wenyewe.
Ni muhimu pia kujenga mafanikio ya kiroho. |
Ewe usomaye makala haya Maisha yako
yanahitaji uwepo wa aina hii ya mafanikio ambao utakuweka karibu baina yako na Mungu.
Kwani kuwepo na ukaribu na mahusiano bora baina ya mtu na Mungu humfanya mtu
aweze kufikia ndoto zake.
Hivyo kama ufanyavyo katika kupanga
malengo mengine ya mafanikio yako, vivyo hivyo ni lazima upange malengo yako
juu ya aina hii ya mafanikio ya kiroho, hapa haijalishi itakadi yeyote ya
kidini uliyonayo ila anachotakiwa ni kuamini ya kwamba Mungu ana nafasi kubwa
sana katika maisha yako.
Mwingine anaweza akaniuliza afisa
mipango labda nawezaje kufikia aina hii ya mafanikio? Laa! Usipate tabu
unachotakiwa kufanya ni; katika utaratibu wa mzunguko wa dunia katika
kulizunguka jua kuna masaa 24 katika mzunguko huo kwa siku.
Sasa ili uweze kufanikiwa katika aina
hii ya mafanikio ni lazima uyatenge masaa ya kumuomba Mungu. Lakini wengi tupo
vizuri katika kumuomba mwenyezi Mungu pasipo kushukuru, lakinu nikwambie kuwa
siri kubwa ya kupewa ipo katika kushukuru pia.
Hivyo basi kama ufanyavyo katika
suala la kutenga masaa kumuomba Mungu, pia fanya hivyo hata katika
kutenga muda kwa ajili ya kumshukuru Mungu . Pia yakumbuke yale maneno matumu
yenye hamasa ambayo yanasema ombeni bila kuchoka, lakini na mimi naongezea ya
kwamba shukuruni bila kukoma.
Wakati huo pasipo kumung'unya maneno,
wala kukuna kichwa huna budi kuhudhurua kwenye nyumba za ibada kila wakati,
makongamano ya kidini na kama ulivyo na ukaribu na simu yako kuliko kitu
kingine kile.
Mazingira hayohayo yajenge pia katika
vitabu vya kidini. Kufanya hivyo kutakufanya uwe na dira na mwanga mpya kila
mara na hatimaye kufikia aina nyingine za mafanikio zilizosalia.
2. Mafanikio ya mahusiano.
Aina ya pili ambayo unatakiwa kuwa
nayo ni aina ya mahusiano baina yako na watu wengine. Hakuna siri ambayo ipo
katika maisha haya kama hautakuwaa na mahusiano bora na watu wengine.
Je unajua wewe ni daraja la mtu mwingine
kuweza kufanikiwa, kama haujui basi nikwambie ya kwamba bila wewe kuna mtu
hawezi kufanikiwa, kama wewe ambavyo unamtegemea mtu fulani ili uweze kukufikisha
lengo fulani wapo baadhi ya watu ambao wanakutegemea sana watu.
Kuwa na mahusiano bora na watu
wengine ni mbinu bora ya kupata taarifa, taarifa ambazo zitakufanya uweze
kufika kule unapopataka. Hii ni aina muhimu sana ya mafanikio ambayo ni lazima
unahitajika uwe nayo bila kuikosa.
Je, ni aina zipi nyingine za
mafanikio unatakiwa kuendelea kuwa nazo, usikose kusoma wiki ijayo siku kama
hii mwendelezo wa makala haya, ili ujue aina nyingine za mafanikio ambazo
unatakiwa kuwa nazo katika ulimwengu huu.
Badili maisha yako sasa kwa kuwa na
fikra sahihi, endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda pia kuchukua fursa
hii kukukaribisha kwenye kundi la Whats
App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na
namba yako kwenda 0713 04 80 35 ili
uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI
KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako Afisa mipango,
BENSON
CHONYA,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.