Oct 26, 2016
Kipindi Muhimu Sana Cha Mafanikio Yako.
Njia
mojawapo kubwa ya uhakika ambayo ukiitumia ni lazima itakupa mafanikio ni
kusubiri. Hakuna kitu au mafanikio ambayo utashindwa kuyapata katika maisha
yako ,ikiwa utakuwa ni mtu wa kufanya kazi na kusubiri.
Wataalamu
mbalimbali wa mafanikio, akiwemo mwandishi wa vitabu wa kimarekani ndugu J.G
Holland amewahi kuthibitisha hili pia kwa kusema“Hakuna mafanikio makubwa duniani ambayo utayapata bila kufanya kazi kwa
bidii na kusubiri”.
Hiyo
ikiwa inaonyesha kuwa upo uhusiano mkubwa sana kati ya kile unachokitaka na
swala zima la uvumilivu wakati unasubiri kufanikisha jambo lako. Ni lazima
ufanye kazi na usubiri mchakato wa kufanikisha jambo lako hilo.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza kuyapata ‘chapuchapu’ na kuamua kukwepa njia hii.
Mchakato wa kusubiri na kuwa mvumulivu kwa kile unachokitaka, upo palepale. Watu
wote wenye mafanikio wanapitia njia hii kufanikiwa na sio kinyume cha hapo.
Vumilia mpaka utimize ndoto zako. |
Kwa
kawaida ile tu kujua kusubiri kitu ambacho una mhemko nacho au mchecheto mkubwa
kukipata ni siri au hatua kubwa sana ya kuweza kukusaidia kufanikiwa. Utulivu utakao
utengeneza wakati unasubiri, ndio utakusaidia ukae sana na kitu hicho tofauti
na ungekipata kwa upesi.
Elewa zipo namna nyingi za kusubiri kile unachokitaka kwenye maisha yako ili ukipate. Kwa mfano, kipo kipindi cha kusubiri wateja kuongezeka pale unapoanza biashara yako. Kipo
kipindi cha kusubiri miezi tisa mtoto, pale mama anapopata ujauzito. Kipo kipindi cha kusubiri kujibiwa majibu yako
pale unapoomba kazi.
Kuwa
na subira, ni kipindi muhimu sana cha mafanikio yako na pia ni kanuni ya asili. Kanuni hii inaweza
ikajitokeza katika yai. Kwa kawaida yai haliwezi kutoa kifaranga mpaka zifike
siku 21.
Si
hivyo pia tunaona kanuni hii inajitokeza pale unapoumia na kupata kidonda. Kwa mfano
tunaona, ukipata kidonda huwa hakiponi mara moja, upo muda wa kusubiri hadi
kidonda chako kipone. Na ndivyo kanuni hii inafanya kazi kwa misingi kama hiyo
kwa mambo mbalimbali.
Kwa
hiyo inapotokea umejiwekea malengo yako na kuanza kuyafanyia kazi, jifunze kuwa
na subira. Acha kuwa na haraka zisizo na msingi kuharakisha matokeo. Kama kila
wakati wewe ni mtu wa haraka haraka hutafika popote. Maisha yanakutaka sana uwe
mvumilivu na mtulivu ili kufanikisha makubwa.
Kipo
kipindi ambacho kinakulazimisha uwe na subira ili mambo yako yatimie. Hiki ni
kipindi au muda ambao unakujenga na kukufanya uweze kufanikiwa. Hichi ndicho
kipindi au wakati muhimu sana wa mafanikio yako. Ukishindwa kuvumilia hapa basi
utaharibu kila kitu.
Hebu
jaribu kufikiria ni wangapi ambao huwa hawana uvumilivu wa kusubiri mafanikio
yao, bila shaka ni wengi tu. Huwa kuna ugumu kwa watu wengi kuvumila kile wanachokitaka,
zaidi ya wengi hutafuta njia za mkato sana ambazo pia huwaangusha.
Kutokana
na kukosa subira, wengi hutaka mipango yao iende upesi sana. kwa mfano, vijana
wa miaka 22 wao hutamani kwa umri huo wawe wana gari, nyumba nzuri, mke mzuri,
miradi ya kutosha na watoto. Haa! Haa! Haa! kama hizo ni ndoto zako umepotea.
Huwezi
kufanikisha maisha yako kwa kwenda kinyume na kanuni za asili au kanuni za
mafanikio. Maisha yanakutaka ufuate kanuni ndogo ndogo ambazo zitakusaida
kupiga hatua kila siku. Mojawapo ya kanuni hizo ni kuwa na subira.
Kama
huna subira ya kutosha unataka mambo kwa upesi sana huwezi kufanikiwa. Anza leo
kwa kujenga msingi wa maisha yako kidogo kidogo. Anza leo kwa kuchapa kazi huku
ukiwa na subira na ndoto zako. Kumbuka ile kusubiria ndoto yako itimie, ni
kipindi muhimu sana cha mafanikio yako.
Endelea
kuwashirikisha wengine waweze kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Pia
napenda kuchukua fursa hii kukaribisha wewe rafiki yangu, kwenye kundi la Whats App ili
uweze kujifunza pamoja nami kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO
YANGU, kisha ikifuatia na namba yako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.