Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, September 30, 2016

Mbinu Za Kukuza Biashara Ndogo.

No comments :
Ni ukweli usiofichika zipo changamoto nyingi sana hasa pale unapukuwa unaanzisha biashara na kuitaka ifike mahali ikue na kujitegemea. Pamoja na changamoto nyingi kama za masoko au ushindani pia huwa ipo changamoto nyingine ya namna ya kukuza biashara yako.
Wafanyabiashara wengi wadogo inakuwa inafika mahali hujikuta wako palepale miaka nenda rudi bila kupiga hatua kubwa mbele. Hiyo yote hutokea hivyo kwa sababu wanakuwa wamekosa maarifa  ya kukuza biashara zao kwa namna moja au nyingine.
Kwa kusoma makala haya inakusaidia kujua mbinu zitakazo kusaidia kama wewe ni mfanyabiashara mdogo kuweza kukuza mtaji wako taratibu na kufika mahali na wewe ukawa na biashara yako kubwa kama wengine unavyowaona.  
Je, mbinu hizo ni zipi? Fuatana nami mwanzo hadi mwisho kuweza kuzijua mbinu hizo na kuzifanyia kazi.
1. Jitume sana.
Inawezekana biashara yako ikawa ni kuuza matunda. Pia inawezekana biashara yako ikawa ni ya uchuuzi yaani kutoa badhaa eneo moja na kuzipeleka eneo lingine kuziuza.
Sasa unapokuwa na biashara ndogo kama za namna hii, ili uweze kufanikiwa ni lazima ufanye kazi kwa bidii sana na kujituma kwa nguvu zote bila kuchoka.

Kuwa mbunifu.
Ikiwa hautafanya hivyo ni lazima hautapiga hatua na biashara yako itakufa. Unajua ni kwa nini itakufa? Ni kwa sababu katika kipindi hiki biashara yako inapokuwa ndogo inataka uangalizi wa hali ya juu sana ili iweze kukua.
Hivyo, utalazimika kujituma sana na kufanya kila aina ya jitahada ambazo zitapelekea kuifanya biashara yako ikaweza kukua na kufika mahali ikajitegemea yenyewe.
2. Kuwa mbunifu.
Mbali na kujituma kapindi ambacho unakuwa una biashara ndogo, jitahidi uwe mbunifu. Unapokuwa mbunifu inakusidia sana kugundua ni kitu gani ambacho wateja wako wanataka au ni kipi ambacho hawataki. Hiyo ni njia bora sana itakayokusaidia kuboresha pale kwenye mapungufu na itakusaidia sana pia kuweza kuikuza biashara yako.
3. Sikiliza malalamiko ya wateja.
Ni vyema pia ukawa ni mtu wa busara kuweza kusikiliza kile ambacho wateja wako wanakisema katika kipindi hiki cha kukuza biashara yako. Hiyo itakusaidia kutimiza  matakwa yao na itakupelekea kuwa na wateja wengi ambao watasaidia kuifanya biashara yako ikue.
4. Tafuta msaada.
Katika kipindi cha kukuza bishara yako na kuifanya iwe kubwa, acha kujaribu kuishi kama kisiwa. Tafuta msaada wa ushauri kwa wale waliofanikiwa wakusaidie kimawazo wao walifanya nini hadi wakafikia huko waliko sasa.
5. Punguza utegemezi kwenye biashara yako.
Pia unapokuwa unaikuza biashara yako acha kutegemea sana pesa unayoipata kwenye biashara yako ndiyo iendeshee maisha yako. Jaribu kuwa na pesa nyingine, vinginevyo bila kufanya hivyo unaweza ukaua kila kitu bila kujijua.
6. Jifunze kukuza mtaji.
Kwa namna yoyote ili biashara yako ikue na ikafika mahali inajitegemea unalazimika sana  kujifunza mbinu za kukuza mataji wako. Hilo ni somo ambalo unatakiwa ulizingatie sanaa na kujiuliza kila wakati ni nini kifanyike ili mtaji uweze kukua.
kwa kifupi, hayo ndiyo baadhi ya mambo machache yanayoweza  kukusaidia kuweza kukuza bishara yako kama unaanzia chini.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
0713048035.


No comments :

Post a Comment