google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 5, 2016

Mambo Ya Kufanya Unaposhindwa Kutimiza Malengo Yako Kwa Wakati.

No comments :
Kuna wakati huwa tunajisikia vibaya na kujihisi kama kukata tamaa, kutokana na hali ya kushindwa kutimiza malengo yetu kwa muda muafaka tuliojiwekea.
Najua ni kitu ambacho wakati huwa kinauma hasa pale unapoona malengo yako hayatimii upesi kama unavyotaka iwe. Je, ni kitu gani unachotakiwa kufanya hasa unaona malengo yako hayajatimia kwa muda muafaka?
1. Weka mipango yako upya.
Kama mbinu ambazo umezitumia kufanikisha malengo yako hazijakusaidia kufikia malengo yako kwa wakati, panga malengo yako tena upya. Acha kujiona umepoteza sana, weka malengo yako upya na jaribu tena na tena na tena.
2. Kuwa king’ang’anizi.
Pale malengo yako yanaposhindwa kutimia kwa wakati jaribu kuwa king’ang’azi. Usije ukaingia katika hali ya kukakata tamaa, kwa sababu hali ya kukata tamaa haiwezi kukusaidia sana zaidi ya kukukwamisha tena.
Panga malengo yako upya.
3. Hamasika na mafanikio ya wengine.
Hata kama mambo yako yamekuwa magumu na malengo yako yameshindwa kutimia kwa wakati, ili kurudi kwenye mstari jaribu kutumia njia ya kuhamasika kwa kuangalia mafanikio ya watu wengine.  
4. Angalia changamoto zilizokuzuia.
Pia ni kweli umeshindwa kufika pale ulipotaka kufika kwa wakati, sasa ni vyema ukaangalia changamoto zile zilizokuzuia kufanikiwa. Ukishazitambua changamoto hizo zinafanyie kazi mara moja na kisha songa mbele.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.