Feb 28, 2018
Wanaoficha Pete Za Ndoa Hawajui Kupenda.
Unapomkuta
mwanamke au mwanaume ambaye yuko kwenye ndoa, amevua au huwa anavua pete yake
ya ndoa mara kwa mara na kuiweka kwenye mkoba wake au mfukoni, utasemaje?
Ni
lazima kuna namna ambayo utamfikiria mtu huyo. Je, utamfikiria kwamba ni malaya,
haridhiswi na ndoa yake, au hampendi mumewe au mkewe?
Hapa
nitajaribu kutoa maelezo ambayo, yatakufanya usihisi vibaya kwa kile ambacho,
umekuwa ukikifikiria kuhusu mwanamke au mwanaume wa aina hiyo.
Imeelezwa
kwamba, wale wanawake au wanaume ambao, huficha pete zao za ndoa, ni watu ambao
hawana uwezo wa kulea watoto, yaani huwa wanawapuuza sana watoto wao.
Kwa
kulinganisha, inaelezwa kwamba, wale wanawake au wanaume wenye kuvua au kupenda
kuvua pete zao za ndoa na kuziweka mikobani, huwa wanawapuuza watoto wao kuliko
wale ambao, huvaa pete zao muda wote.
Weka wazi pete yako ni ishara ya upendo. |
Lakini
pia, inaelezwa kwamba wale wanawake au wanaume wenye sura za kuvutia au nzuri
sana wanapokuwa na tabia hii ya kuficha pete zao za ndoa, huwa ni wazazi
wasioweza hata chembe kulea watoto wao, yaani wanakuwa ni wazazi aambao, ni
watekelezaji sana, wasiojali kabisa kuhusu watoto wao.
Katika
moja ya tafiti zake mwanasaikokoljia Andrew Harell wa chuo kikuu cha Alberta nchini Canada, anasema kwamba, hili sio
suala la kubahatisha, kwani amelifanyia utafiti kwa wengi, kwa muda mrefu na
katika mazingira tofauti.
Mwanasaikolojia
huyo anazidi kudai kwamba, hata linapokuja suala la kuangalia na kutunza
wagonjwa, wale watu wanaoficha pete zao za ndoa, hawana uwezo wa kuwatunza
wagonjwa ukilinganisha na wale wenye kuvaa pete.
Inaelezwa
kwamba, kuvua pete ya harusi na kuificha ni ishara kwamba, mwenye pete hiyo
hana hisia au uwezo wa kujifunga na ndoa yake au familia yake. Kwa kukosa sifa
hizo, ni wazi mtu huyo hawawezi kujifunga na watu wengine wenye kuhitaji msaada
wake wa kihisia kama vile wagonjwa.
Kuvua
au kuficha pete ya ndoa, kunahesabiwa kama ni dalili ya mtu kutaka kuanzisha
uhusiano mpya nje ya ndoa yake. Haja hiyo inapotimizwa, uwezekano ni mkubwa kwa
mwanaume au mwanamke kupunguza upendo au kujali familia yake, akiwemo mke au
mume au watoto. Kwa hali hiyo, kuficha pete ni dalili ya kutokujali na
kushindwa kujifunga kwenye uhusiano.
Wakati
huo huo taarifa za kitafiti zinaonyesha kwamba, wazazi wenye kuvua pete huwa
hawatoi uangalifu mkubwa kwa watoto wao wenye sura mbaya, ukilinganisha na ule
wanaoutoa kwa watoto wao wenye sura za kuvutia au wazuri.
Katika
moja ya tafiti zilizowahi kufanywa, zilihusisha
wazazi na watunza watoto walioenda na watoto hao kwenye supermarkert. Ilionekana
kwamba, wale watoto wasiopendeza, waliachwa kwa umbali mkubwa bila wazazi wao
kujali, wakati wale watoto wenye kuvutia, wazazi au walezi walikuwa nao karibu
sana.
Tafiti
zote hizo zinajaribu kuonyesha upo uhusiano mkubwa sana kati ya kitendo cha kuvua pete
na suala zima la kujali. Je, hali hiyo kwako ikoje? Huu ni utafiti tu, wewe je,
unasemaje?
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku. Pia chukua jukumu la
kumshirikisha mwingine, ili aweze kujifunza na kunufaika na masomo yanayotolewa
humu.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA ESTHER ZACHARIAH,
DAR ES SALAAM.
MAWASILIANO; esterzacharia73@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.