Sep 30, 2021
Njia Pekee Itakayokufanya Ukawa Hodari Ni Hii…
Jiulize unataka kuwa hodari katika jambo lipi? Ukishapata jambo hili ambalo unataka kuwa hodari, anza utekelezaji wa kulifanya jambo hilo kila siku na kwa juhudi zote. Usijaribu kufanya na halafu ukaacha, hautaweza kuujenga uhodari kwa namna hiyo.
Sep 29, 2021
Sababu Nne (4) Kwa Nini Maisha Yanazidi Kuwa Magumu Kwa Wengine.
Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la watu linalalamika kwamba maisha yamekewa magumu. Kwa sababu hii pia watu wengi wamekuwa wakikata tamaa na kuona maisha hayafai ni bora waishi hivyo hivyo ilimradi siku ziende.Sep 28, 2021
Mambo Ya kuzingatia Ukitaka Kufanikiwa Katika Masuala Ya Kifedha.
Somo la fedha ni la muhimu sana kwa kila mmoja wetu, hii ni kwa sababu tunashindwa kupata au kudumu katika mafanikio yetu kifedha hii ni kwasababu wengi wetu hutuna uelewa wa kutosha katika suala la kipesa.Sep 27, 2021
Silaha Kubwa Ya kufikia Mafanikio Yako Ni Hii.
Kati ya kitu muhimu sana cha kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Kati ya silaha kubwa ya kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Unapokuwa na akili ya utulivu inakusaidia kuona mambo mengi, na kufanikisha mambo mengi pia.
Si rahisi sana kuweza kufanikiwa sana kama akili yako haijatulia. Unatakiwa ujue, silaha yako kubwa ya mafanikio ni matumizi ya akili yako na wala si bahati au muujiza kama uwazavyo.
Akili yako ina uwezo wa kukupa matokeo makubwa sana kama imetulia, hapa inaweza ikakupa majibu mazuri na ikaleta matokeo ya kushangaza ambayo huwezi kuyaamini.
Hivyo, unatakiwa kila wakati kuchagua mazingira tulivu yatakayoifanya akili yako ifanye kazi kwa utulivu. Unatakiwa kuishi na watu sahihi, wasio na makelele kwako.
Lakini si hivyo tu, unatakiwa kuishi na mke au mume sahihi kwako asiye na makelele. Unatakiwa kuishi na mwenzi wako ambae anaifanya akili yako itulie na isiwe ya vurugu.
Amani ya akili, utulivu wa akili, ndio chanzo cha mafanikio makubwa yote na yakutisha. Hakuna ambae aliyefanikiwa huku akili yake ikiwa haijatulia, mtu huyo hayupo.
Waangalie vizuri watu waliofanikiwa, utajifunza kitu kimoja kwao ni watu ambao akili zao zimetulia. Unasema nimejuaje, angalia jinsi wanavyoongea, wanaongea kwa utulivu mkubwa sana, hiyo ni ishara akili zao zimetulia.
Ili kufukia mafanikio yako makubwa, haina haja na maana kuishi na watu au katika eneo ambalo linakunyima utulivu wa akili. Jiulize, ya nini kuishi na mpenzi ambaye anaifanya akili yako isitulie na kuanza kumwaza yeye. Tafuta utulivu wa akili utaona matokeo yake makubwa jinsi utakavyo yapata.
Unapokuwa na utulivu wa akili inakusaidia sana wewe kupangilia mambo na mikakati yako kwa ukamilifu, tofauti na ambavyo ukikosa utulivu akili yako haiwezi kuwaza kitu cha maana na kukupa matokeo makubwa.
Zingatia sana, utulivu wa akili, ni silaha ya kwanza katika kufikia mafanikio yako. Kila siku, jitahidi, utafute eneo lilotulia na tafakari maisha yako, na utaona matokeo mazuri yakija kwa upande wako.
Unatakiwa ujue, silaha kubwa katika kufikia mafanikio yako ni
utulivu wa akili. Ukituliza akili zako, utafanya mambo makubwa sana na ya
kushangaza wengi na pia wengi hawataamini je, kweli ni wewe. Kumbe siri, ipo
kwenye kutuliza akili, basi.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 26, 2021
Chagua Mwendo Upi Unakusaidia Kufanikiwa.
Kuna wakati unaweza ukakamilisha mambo mengi sana, kama utaamua kwenda kwa taratibu. Unatakiwa usikimbize mambo yako, ila unatakiwa kwenda taratibu na kufanya kwa uhakika na ufanisi mkubwa wenye faida.
Kwa mfano, kama kuna majukumu ambayo unayafanya kila siku, basi, majukumu hayo yafanye kwa utaratibu, kwa utulivu mkubwa na utajikuta unakamilisha mambo mengi ambayo hukutegemea.
Kuna watu wanafikiri ili kukamilisha mambo mengi unatakiwa kwenda kwa haraka zaidi, kitu ambacho si kweli. Unaweza kwenda taratibu na ukakamilisha mambo mengi, unaweza kwenda haraka halafu ukaharibu.
Ni wajibu wako unatakiwa ujue ni wakati upi unatakiwa uende taratibu na wakati upi unatakiwa uende haraka. Si kila wakati wa kwenda kwa haraka ikiwa utafanya hivyo huwezi kukamilisha mambo mengi zaidi unajiharibia wewe.
Kama nilivyosema, kwenda haraka hakuwezi kukusaidia kukamilisha mambo mengi kwa sababu, akili yako inakuwa haijatulia yaani inayumba yumba. Kama akili yako inayumba hivyo, kufanikisha mambo mengi ni ndoto.
Unatakiwa kila wakati kujiuliza, hapo ulipo ni wakati wa kwenda haraka au wakati wa kwenda kwa kasi. Kisha ukishapata majibu, fanya uamuzi sahihi. Maisha sio mashindano na wengine, angalia mwendo wako.
Hapa ndio upo ule umuhimu wa kuchagua mwendo upi unakusaidia kukamilisha mambo mengi. Je, mwendo wa kasi au mwendo wa taratibu, lakini kaa ukijua kila mwendo una sehemu yake.
Suala hili, lipo kama vile unavyoendesha gari. Si kila wakati unatakiwa kukimbiza gari, yapo mazingira yake. Na kwenye maisha iko hivyo hivyo, kuna wakati wa kwenda kwa haraka na wakati wa kwenda taratibu.
Kufanikiwa kwako kunategemea sana uchaguzi wako wa mwendo upi
uutumie na katika eneo lipi. Fanyia kazi hili, na utaona matokeo makubwa kwa
upande wako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 25, 2021
Mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kufanya uwekezaji.
Ipo hivi unapofanya uwekezaji katika jambo lolote unatakiwa
kuelewa kwamba hakuna faida utakayoipata papo hapo. Bali uwekezaji huchukua
muda fulani mpaka uje uone uwekezaji wa jambo hilo.
Wengi
wanapoambia wawekeze katika jambo fulani hukurupuka katika kuwekeza mwisho wa
siku hujikuta wanapata hasara au kutokuona faida ya uwekezaji waliofanya.
Kitu
pekee ninachopaswa kukumbusha ni kwamba unapotaka kuwekeza katika jambo fulani,
unatakiwa kuzingatia mambo haya machache;
·
Uwekezaji unakutaka uweze kulielewa jambo unalotaka kuliwekeza kwa
undani zaidi.
·
Faida ya uwekezaji huchelewa sana kuonekana.
·
Uwekezaji huitaji uvumilivu mkubwa ndani yake.
·
Uwekezaji unahitaji umakini wa hali ya juu ili kuepukana kupata
hasara ya jambo husika.
Hivyo ni
vyema ukayazingatia hayo machache kati ya mengi kabla hujaamua kuwekeza katika
jambo lolote lile ulitakalo.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya.
0757-909942
Sep 24, 2021
Jinsi Ya Kupata Wazo Bora La Biashara.
Tafuta wazo sahihi la kukufanikisha. |
Sep 23, 2021
Vizuizi Katika Maisha Yako, Vipo Kwa Ajili Ya Kukuandaa Na Jambo Hili.
Vizuizi katika maisha, huwa havipo kwa ajili ya kukuzuia wewe eti ushindwe kufanikiwa. Vizuizi katika maisha huwa vipo kwa ajili ya kukuandaa uwe bora kwenye mafanikio yako.
Piga picha, ingekuwa vipi mtoto wa miaka 10 angekuwa yupo chuo Kikuu, hiyo isingekuwa na maana yoyote. Elimu yake ingeonekana bure na kukosa ule uthamani mkubwa.
Lakini, vizuizi vya miaka takribani 14 ya kupitia shule ya msingi, sekondari, kufanya majaribio, hivyo vyote vinamkomaza na kumfanya aione digrii ya chuo Kikuu ni ya thamani.
Piga picha pia, kama mafanikio unayoyataka yangekuwa rahisi tu, pasipo kupitia changomoto au vizuizi vyovyote vile, hayo mafanikio naamini yasingekuwa na raha kubwa zaidi.
Kuna wakati unaweza ukawa unalaumu sana kutokana na vizuizi unavyokutana navyo, lakini ukiangalia vinakukomaza na kukufanya ukawa bora kwenye mafanikio yako.
Unapokutana na vizuizi, ni wakati wako wa kujifunza maisha yanasema nini juu yako na si wakati wa kulaumu. Jifunze kitu kutokana na vizuizi hivyo. Usikae kizembe jifunze kitu.
Acha kuona vizuizi ni kama tatizo kwako, ona vizuizi ni kama njia ya kuweza kukukomaza wewe na kukufanya ukawa bora. Utafanikiwa sana kama vizuizi vyako utaviona kwa jicho hilo.
Kama unapitia kwenye changamoto kubwa, kaa ukijua unaandaliwa, unakomazwa hasa kwa kule unakoenda. Unajengewa misuri ya ukomavu itakayokufanya ufanikiwe.
Shukuru kama unakutana na changamoto. Shukuru kwa sababu ndio
saa ya kukomazwa. Unatakiwa kukumbuka, vizuizi havipo kwa ajili ya kukuzuia
bali kukuandaa kuwa bora.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 22, 2021
Ujasiri Unaohitajika Katika Kusaka Mafanikio Yako.
Tunaaminishwa ya kwamba mnyama mwenye ngozi ngumu kuliko wote huenda ikawa ni mamba, japo hakuna uthibitisho kamili juu ya hilo. Uwezo wa mnyama mwenye ngozi ngumu ni mnyama mwenye uwezo wa kuvumilia mengi ikiwemo uwepo wa jua kali wakati wa kingazi.
Kama ilivyo kwa mnyama mamba basi hata sisi tunaambiwa ili tuwe na ngozi ngumu katika kufanya mambo mbalimbali, hii ikiwa na maana ya kwamba tunapaswa kuvulimia kila changamoto ambazo zitakuwa zinajitokeza kwenye kukamilisha mambo mbalimbali.
Ni muhimu kuwa na ngozi ngumu kwa sababu wengi wetu tumekuwa ni watu wa kukata tamaa sana, hasa pale zinapojitokeza changamoto mbalimbali kwenye mambo tuyafanyayo.
Ila ukweli ambao napaswa kukumbusha siku ya leo ni kwamba pamoja na changamoto zote zinazojitokeza kwenye mambo mbalimbali tunakumbushwa ya kwamba tunapaswa kuwa wavumilivu kwani mvumilivu ndiye ambaye atakula mbivu, au kwa maneno mengine anayevulia ndiye atakayefanikiwa zaidi.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Ndimi,
Afisa Mipango Benson Chonya
0757909942
Sep 20, 2021
Nguvu Ya Changamoto.
Kuna wakati unajikuta upo kwenye siku ambayo una vitu vingi sana vya kufanya, lakini cha ajabu huwa ni siku ambayo pia unaweza kukamilisha mambo mengi ambayo hukutarajia.
Pia kuna siku ambayo unajikuta una vitu vichache vya kufanya, lakini huwa ni siku ambayo hukamilishi mambo mengi pia. Unashangaa unajikuta, mambo mengi hujafanya.
Hiyo inamaanisha nini, kila unapokuwa kwenye changamoto, akili yako inakuwa na nguvu na uwezo wa kufanya mambo mengi na kufanya kazi vizuri na ufasaha mkubwa.
Unatakiwa ujue, changamoto unazokutana nazo, zinakuwa zina uwezo mkubwa wa kuamsha akili yako na kuifanya ifanye kazi kwa njia ya maajabu na kuleta majibu ya kushangaza.
Hivyo, fundisho kubwa hapa ni kwamba, hutakiwi kuogopa changamoto, kwani changamoto zinakukomaza na kukusaidia kukamilisha mambo mengi. Changamoto ni msaada kwako.
Kila unapokutana na changamoto, jiulize, utawezaje kufanya na kupata majibu sahihi. Hakuna kinachoshindikana kila kitu kinawezekana hata ukiwa kwenye changamoto.
Ipo nguvu kubwa sana ndani ya changamoto, kama utaelewa vizuri. Yale ambayo ulikuwa huwezi kuyafanya unaweza kuyafanya ukiwa kwenye changamoto kubwa na za kutisha.
Kuanzia leo, acha kuhuzunika unapokutana na changamoto, jifunze
juu ya changamoto hizo. Kazi ni kwako, weka akilini changamoto wakati wote ni
msaada kwako, zitakuimarisha na kukufanikisha.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 19, 2021
Hii Isiwe Sababu Ya kukuzuia Kufanikiwa...
Kuna watu hawafanikiwi kwa sababu, wanafanya kazi zao nusu nusu na zinaishia kati, hawafiki mwisho kule wanakotakiwa kufika. Watu kama hawa kufanikiwa ni ngumu.
Kwa mfano, ilitakiwa watu hao wafanye kazi zao zianze kuwalipa, kwa sababu hawafiki mwisho yaani wanaishia kati, basi hujikuta wafikii yale mafanikio yanayotakiwa.
Utakuta mtu ni mwimbaji mzuri sana, lakini hafanikiwi, kwa sababu, hajaweza kurekodi, hafanikiwi kwa sababu hajaweza kujiweka wazi akajulikana na kusaidiwa na watu wengine.
Pia utakuta mtu ni mwandishi mzuri sana, lakini anakuwa hafanikiwi kwa sababu, mtu huyo anakuwa bado hajachapa kazi zake zikaonekana, hivyo kazi zake zinakuwa ni nusu hazijafika mwisho wa kumpa faida.
Wapo watu wa aina hii wengi, utakuta wengine wanafanya kilimo, lakini hawaweki ule ubora unaotakiwa ili wafanikiwe. Kwa kuishia kwao kati inaleta shida sana kwao na kuwazuia kufanikiwa.
Ili kufanikiwa kwa chochote kile unachokifanya, unatakiwa kufanya kitu hicho mpaka mwisho. Hutakiwi kuishia katikati, utakuwa unajipoteza wewe kwa kupoteza muda na nguvu zako bure.
Kwa chochote ukifanyacho, kifanye hadi mwisho na ukione kinakupa mafanikio makubwa. Hapo ndipo ilipo siri ya mafanikio yako, yaani kufika mwisho. Kama hufiki mwisho, itakuwa kazi sana kwako kufanikiwa.
Kufanya kazi nusu nusu na kushindwa kufika mwisho isiwe hata sababu ya kukuzuia kufanikiwa. Kwa chochote ukifanyacho, nenda mazima mazima, hakuna kufanya kazi nusu nusu, hutafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 18, 2021
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuipa Akili Yako Ushawishi Na Ikupe Mafanikio.
Wataalamu wengi wa mafanikio wanasisitiza sana umuhimu wa kupitia malengo yako kila siku ili iwe rahisi kwako kuweza kuyatimiza. Unajua ni kwa nini hili linasisitizwa sana? Umeshawahi kujiuliza kwa nini?
Hiyo yote ni kuufanya ubongo wako uamini kwamba malengo yako yanawezekana. Hiyo iko hivyo pia kwa sababu kabla hujafikisha miaka mitano unakuwa umekataliwa mara 40,000 kwa vitu tofauti na ni mara 5000 tu ndio unakuwa umekubaliwa.
Mpaka hapo unaona kama umekataliwa mara nyingi hivyo, tafsiri yake ni rahisi kuona kila kitu hakiwezekani. Ili mambo hayo yawezekane sasa, inabidi uushawishi ubongo wako kuamini kwamba inawezekana.
Kumbuka mafanikio yanaanza na sisi wenyewe kwanza, yaani zile imani tulizonazo ndani mwetu, ndizo zinajenga mafanikio. Hivyo unatakiwa kujilisha vitu chanya na kujiaminisha kwamba inawezekana kwa lolote lile kwako, pitia malengo yako kila siku utafanikiwa.
Hakuna namna utakayoweza kuifanya akili yako iamini kuwa
utafanikiwa zaidi ya kuandika malengo yako na kuyapitia kila siku. Ukifanya
zoezi hilo kila siku la kuyapitia malengo yako, utaipa akili yako ushawishi
mkubwa sana na utafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 17, 2021
Usipotumia Mambo Haya Vizuri, Utakwama.
Unatakiwa kutumia kila ulichonacho kwa uhakika na vizuri kabisa. Acha kujidanganya kwamba unataka mafanikio makubwa wakati hata ile misingi ya kutengeneza mafanikio makubwa unaiharibu hovyo hovyo.
Haiwezekani eti unasema unataka mafanikio makubwa wakati unatumia muda, pesa na nguvu zako hovyo, ambapo vitu hivyo kwa pamoja vingekusaidia kufikia mafanikio makubwa kama ungevitumia vizuri na kwa busara.
Pesa unazozipata hazijiamulii zenyewe kwamba ‘sasa mimi pesa ninakwenda kununua kitu hiki au kile.’ Wewe ndie mwenye jukumu la kupanga pesa zako zitumike wapi na kwa sababu ipi.
Sasa kama hiyo iko hivyo, kwa nini unafanya maamuzi mabovu ambayo yanakupotezea pesa nyingi na kwa kiasi kikubwa? Kuwa makini sana na matendo yako ili yasikupotezee pesa ambayo ni moja rasilimali muhimu kukusaidia kufanikiwa.
Hapo ulipo najua una pesa za kiasi fulani hata kama ni ndogo, najua una muda na nguvu fulani, sasa kwa nini hivi vitu usivitumie kwa uangalifu ili viweze kukusaidia kukupa mafanikio makubwa na badala ya kuvipoteza tu kiholela.
Watu matajiri, wanajua namna ya kutunza pesa zao vizuri, kwa nini wewe usiwe miongoni mwao? Huna pesa si kwa sababu pesa zinakukimbia bali ni kutokana na matendo yako yanayofukuza pesa.
Kitu cha kufanya jiulize, ni hatua zipi utaweza kuzichukua ili kuweza kulinda rasilimali zako za kukusaidia kufanikiwa ambazo ni pesa, muda na nguvu zako. Kama hujui tafuta watu wenye mafanikio kisha wafatilie.
Kama utatumia muda, nguvu na pesa zako vizuri, utafanikiwa.
Usipotumia mambo hayo vizuri, nakuhakikishia itafika utakwama na hautaweza
kupiga hatua kubwa. Muda wako, pesa zako na nguvu zako, ni vitu vya msingi sana
katika mafanikio yako.