Jun 9, 2015
Dalili Saba Za Mtu Anayejitambua Katika Maisha Yake.
Kuna dalili zenye uwezo wa
kukusaidia kumbaini mtu anayejitambua katika maisha yake. Unapokosa dalili hizi
ujue kabisa kuwa bado hujafikia ngazi ya juu kabisa ya kujiweza kujitambua na
kuweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako. Ninapozungumzia mabadiliko
nikiwa na maana ni kuwa na uwezo wa kupanga malengo na kuyafanikisha na kuishi
kwa amani na furaha bila kutegemea mambo ya nje.
Huenda dalili hizi zinaweza
zikawa nyingi zaidi lakini kwa leo nitakutajia chache tu baadhi ambazo zitaweza
kukusaidia moja kwa moja. Ukiona una dalili hizi au jamaa yako ana dalili hizi,
huna budi kuanza kujua kwamba, uko kwenye kiwango cha juu cha kuweza kutumia
nguvu zako za ndani na kuweza kufikia mafanikio yoyote makubwa unayoyahitaji
katika maisha yako ya kila siku.
Kwanza, ni mtu anayepokea
mambo katika hali halisi. Haathiriwi na mazoea, bali kile kilichopo,
kinachopaswa kuona na kuchambuliwa, ndicho anachokipokea. Ina maana huchambua,
bila kujali mazingira au mazoea yanasema nini. Unapokuwa unaona mtu ana dalili
kama hiyo, elewa kabisa mtu huyo
anajitambua katika maisha yake.
Pili, ni mtu anayejikubali
yeye kama yeye, hataki wala hatamani kuwa kama wengine. Ameridhika na
kukubaliana na alivyo na maisha yake yalivyo. Lakini pia ni mtu anayekubali
wengine kama walivyo na kutokutaka wengine wawe kama yeye. Vilevile ni mtu
anayekubaliana na maumbile na uhalisia wake katika maisha yake.
Tatu, ni mtu ambaye hahitaji
sana usiri na faragha. Mtu anayejitambua huzidi sana kujiondoa kwenye hali ya
kuhitaji faragha sana kama ndiyo jambo la lazima. Kwa kujitambua, mtu huwa huru
zaidi na hakuna jambo ambalo linaweza kuhitaji faragha. Kama yapo ni machache
sana ambayo ni ya maana na sio kila jambo ni usiri na faragha.
Nne, ni mtu ambaye huridhika
na kutambua mchango wa mwingine au wengine na kukubaliana na yale yenye
kumtokea. Kwa hali hiyo ni mtu ambaye hahemkwi. Majibu yake kwa mambo
yanayomtokea yametulia sana, hasa kwenye suala la hisia zake. Anayejitambua
hudhibiti hisia, na siyo hisia kumdhibiti yeye.
Tano, ni mtu ambaye hayuko
tayari kuwa mtiifu, ni mtu ambaye hayuko tayari kuwa mtiifu tu bila kujua
sababu. Kama ni kufuata jambo, hajiulizi maswali mengi sana kabla hajaamua. Hii
ina maana kwamba, haendeshwi na mazoea, bali hutumia tafakari kwanza.
Sita, ni mtu mwenye uwezo wa
kujibainisha na binadamu mwingine. Aliyejitambua
huamini kwamba, kile ambacho kinamfurahisha yeye, kinaweza kumfurahisha
binadamu mwingine hivyohivyo kama alivyo yeye kilimvyomfurahisha.
Saba, ni mtu ambaye anapata
uwezo mkubwa wa ubongo, mawazo ya kufanikisha na kufanya hali iwe bora zaidi.
Kwa hiyo, ni mtu ambaye ana uwezo wa kubuni na kufanya mabadiliko mahali. Siyo
mabadiliko ya kuleta fedha tu, bali mabadiliko ya kuwafanya binadamu wengine
kujisikia vizuri.
Kwa kifupi, hizo ndizo
dalili ambazo mtu anayejitambua anaweza kuwa nazo katika maisha na kuzitumi
kuweza kuleta mabadiliko chanya katika maisha yake na jamii kwa ujumla.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.