Jun 17, 2015
Mambo 5 Unayoyapoteza Katika Maisha Yako Kwa Sababu Ya Kuwa Na Hofu.
Kuwa na hofu ni kitu ambacho
kila binadamu anacho, lakini kwa bahati mbaya hofu hizi zimekuwa zikiwatesa na
kuwaumiza wengi zaidi. Hili limekuwa likitokea hivyo, kutokana na wengi wetu kuwa
na hofu zilizopitiliza zaidi.
Je unajua ni madhara kiasi
gani ambayo unaweza ukayapata katika maisha yako kutokana na wewe kuwa na hofu
nyingi? Kwa haraka haraka naomba nikutajie mambo unayoweza kuyapoteza katika
maisha yako ikiwa tu wewe utakuwa mtu wa hofu sana.
1. Hofu
inakupotezea mipango na malengo yako.
Hofu unazokuwa nazo katika
maisha yako, mara nyingi huwa ni rahisi kuweza kukupotezea mipango na malengo
yako uliyojiwekea. Hii huwa inatokea kwa
sababu unapokuwa una hofu zaidi unakuwa unajikuta unashindwa kufuata malengo
yako uliyojiwekea kwa usahihi. Na hilo huwa linatokea pengine kwa sababu ya
kuogopa ukubwa wa malengo uliyojiwekea.
Watu wengi kutokana
kutawaliwa na hofu nyingi katika maisha yao, wamejikuta wakiwa ni watu wa
kushindwa kutimiza karibu malengo yao muhimu ambayo wanajiwekea. Kiukweli ukiwa
na hofu nyingi, tambua kabisa kuwa utaharibu mambo yako mengi katika maisha
yako. Hivyo basi ni muhimu kuweza kumudu hofu ulizonazo ili kufanikiwa.
2.
Hofu inakupotezea ujasiri.
Unaweza ukawa jasiri na
kuweza kusimamia maisha yako kweli, lakini unapokuwa una hofu kwa bahati mbaya
huo ujasiri huwa huwa unatoweka. Hiki ndicho kitu kimojawapo ambacho hofu
huweza kutupotezea katika maisha yetu. Tambua kuwa kwa kadri unavyozidi kuwa na
hofu ule ujasiri na ushujaa wote hutoweka. Huwezi kuwa shujaa wa kweli kama
ndani yako umejawa na hofu nyingi.
Kama haunielewi kwa hili
sana, tuchukulie kwa mfano umeajiriwa iwe na serikali au kampuni fulani. Wakati
huohuo kuna madai au haki fulani unazozidai kwenye eneo hilo unalolifanyia
kazi. Ikiwa ndani yako utakuwa na hofu za kufikiri kuwa kwa kudai kwako haki
zako unaweza kufukuzwa kazi uwe na uhakika, huwezi kufanya mabadiliko. Kwanini?
Ni kwa sababu hofu inakuwa imekupotezea ule ujasiri bila ya wewe kujijua.
3.
Hofu inakupotezea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
Elewa kuwa, hakuna maamuzi
yoyote ya maana ambayo unaweza ukayafanya ikiwa ndani mwako una hofu nyingi. Maamuzi
yote mara nyingi utakayoyafanya wakati una hofu yatakuwa yana nia ya kukufanya
uikimbie hofu hiyo inayokukabili. Hivyo kwa maana hiyo hayawezi kuwa maamuzi
sahihi kwako zaidi ya kujilazimisha ili kwako upate unafuu fulani wa kutoka
kwenye hofu.
Jaribu kufikiri kidogo
katika maisha yako juu ya maamuzi ambayo umewahi kuyachukua ambayo yalikuwa ni
ya hofu zaidi. Utakuja kugundua kuwa maamuzi uliyoyafanya hayakuwa yako na si
hivyo tu pia hayakuwa sahihi kwako kwa asilimia zote. Bali ni maamuzi ambayo
uliyafanya kutokana na hofu zako. Kutokana na hofu hizo ulipoteza uwezo wa kufanya
maamuzi sahihi.
4.
Hofu inakupotezea fursa nyingi.
Ni rahisi sana kumkuta mtu
akifanya kazi ileile hata kwa miaka ishirini bila kuiboresha na kwa bahati
mbaya kazi hiyo inaweza kuwa haimsaidii sana hata yeye katika maisha yake. Hiki
ni kitu ambacho nimekiona sana kwa maisha ya wengi wakiwa palepale bila kusogea
kutokana na kuwa ving’ang’azi wa kazi ambazo hazina tija kwao eti kwa sabau ya
mazoea, hivyo ni ngumu sana kwao kuweza kuzibadilisha.
Unapokuja kuchunguza kwa
nini inakuwa hivyo kwao, jibu ni rahisi tu hofu walizonazo. Kutokana na hofu
zao wanaogopa ikiwa wataacha kazi au watabadilsha biashara maisha yao
yatakuwaje? Ni watu ambao hawana uhakika wa njia mpya, hivyo ni bora wabaki
hapo walipo. Katika maisha yako hakuna kitu kibaya kama kupoteza fursa kubwa
kwa sababuya hofu ulizonazo. Jifunze kuzikabili na zidi kusonga mbele.
5.
Hofu inakupotezea furaha na amani ya kweli.
Hakuna utakachoweza
kukifurahia katika maisha yako ikiwa
wewe umetawaliwa na hofu nyingi. Kikubwa utakachokuwa ukiwaza tu hizo hofu zako
na mwisho wa siku utajikuta ile amani ya kweli ndani yako imetoweka kabisa.
Unaweza ukawa shahidi kwa hili kwa kukumbuka zaidi kupitia maisha yako binafsi
kuwa kipindi ambacho upo ama ulikuwa na hofu nyingi ni lazima ulikuwa ukikosa
ile furaha ya kweli.
Si wewe tu jaribu angalia
watu wote iwe jirani zako ama marafiki zako ambao hawana furaha sana. Ukija
kuwaangalia sana watu hao kinachowafanya wawe hivyo mara nyingi ndani mwao wanakuwa wana hofu
nyingi zaidi. Hofu hizo huweza kuwapelekea washindwe kujiamini, kujiaona kama
vile hawafai na zaidi ya yote furaha wanayokuwa nayo pia huweza kutoweka kabisa
katika maisha yao. Hiyo yote inakuja kwa sababu ya hofu.
Kumbuka, unao uwezo wa
kufanya mabadiliko katika maisha yako kila siku ikiwa utaamua hivyo. Hata hofu
zako ulizonazo unaweza kuzibadilisha na kuishi maisha ya ushindi unayoyataka
yawe kwako. Hayo ndiyo mambo muhimu utakayoyapoteza ikiwa utazidi kukumbatia
hofu.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea mtandao huu wa DIRA YAMAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.