Jun 26, 2015
Hizi Ndizo Athari Za Kuwa Na Maumivu Makali Kihisia.
Nakumbuka ni hivi karibuni
ambapo ilikuwa ni majira ya jioni na
nilirudi nyumbani tofauti na kawaida yangu. Siku hiyo niliamua kupitia jikoni
kama kituo change cha kwanza. Nilipoingia jikoni nilimwona binti ambaye huwa
tunakaa naye akiwa ameinamia kwenye beseni la kuoshea vyombo
hapo jikoni.
Nilimsemesha na aligeuka
kuniangalia bila kunijibu chochote. Mikono yake alikuwa ameiweka ndani ya
beseni kama kuficha kitu lakini hata nilipomwangalia nilihisi kama alikuwa
analia hivi. Nilipomsogelea na kutazama mikono yake, nilipatwa na mshtuko sana.
Alikuwa ameshika kisu na mkono wake wa kushoto ulikuwa ukitoka damu. Ilionesha
alikuwa amejikata.
Nilipomuuliza ni kwa nini
anafanya vile huku nikiwa nimetundikiwa, alinitazama tu huku machozi yakimtoka.
Siyo siri niliogopa sana. Baada ya tukio lile niliamua kumuulizia daktari kwa
ufafanuzi zaidi alionipa ndipo nilipojua
hasa kuhusu jambo lile ambalo lilipelekea binti yule kuweza kujiumiza.
Ilinibidi kwa kweli,
nimpeleke hospitali na tatizo nililokuja kuambiwa na daktri ni tatizizo linalotokana hasa na mtu kukata tamaa, kuchangiwa
na kuamua kujiadhibu kwa kujiumiza. Bila shaka tunajua kwamba, kukata tamaa
kunapozidi na mtu anapohisi kuwa maisha hayana maana, anaweza kujiuwa.
Nilijifunza yote hayo kutokana na tatizo alilokuwa nalo binti
yangu huyu. Kujiumiza huku kunaweza kuwa ni kwa kujikata mikono, miguu au
sehemu nyingine ya mwili. Wakati mwingine inaweza kuwa kwa kuvuta nywele ,
ung’ata kucha kwa nguvu, kujipiga au kujichubua au kukwaruza hata kidond
ambacho hata kilikuwa karibu kupona.
Ingawa siyo tatizo kubwa ,
kwani inakadiriwa ni mtu mmoja tu kila
mia moja anakabiliwa nalo, bado hii ni idadi kubwa ya kutosha. Ina maana kwaba
kwa hapa nchini kiasi cha watu 440,000 wanakabiliwa na tatizo hilo.
Pamoja na ukubwa wa tatizo
hilo kwa bahati mbaya hakuna mtaalamu ambaye hadi sasa amewahi kusema kwa hakika tatizo hilo linatokana na nini
hasa. Lakini angalau inafahamika kwamba ni juhudi ya anayejiadhibu kutaka
kujihisi ahueni ya kimaisha angalau kwa muda fulani.
Bila shaka tumewahi
kushuhudia au kusikia kuhusu watu wanaojikwangua, wanaojiumiza, wanaojibamiza
ukutani, wanaopanda mitini na kujiangusha ili wavunjike kwa kuamini kuwa
wanapata ahueni kwa kufanya hivyo. Kama tumewahi kushudia au kusikia, hii yote
ni sehemu ya tatizo hili.
Mara nyingi kujiadhibu huku
hufanywa kwa siri sana na wahusika. Kwa hiyo wakati mwingine inakuwa vigumu
kuona kuwa anajiadhibu, bali tunaweza
kuona matokeo yake. Mtu anaweza kuona kidonda kipya kwenye mwili wa mtu au
kuona nywele zimevurugwavurugwa ghafla tu ama dalili nyinginezo.
Kwa bahati mbaya, hawa watu
wanaojiumiza wenyewe, ni mara nyingi huwa hawajui ni kwanini wanajiumiza,
hujiumiza kwa sababu huhisi wakifanya hivyo watapata nafuu. Lakini nafuu ya
nini, huwa ni swali gumu kupatiwa majibu.
Bado hata hivyo, ukweli
unabaki kwamba, wanafanya hivyo kwa sababu wana maumivi kihisia. Kwa hali hiyo,
kama inatokea mtu anagundua kwamba, jamaa yake ameingia mahali ambapo anajiumiza
mwenyewe kwa njia yoyote, inabidi ajaribu kumsaidia akijua ni tatizo la
kihisia.
Nimeshawahi kusikia kuhusu
watu amao wamepelekwa kwa waganga wa asili kwa sababu ya tatizo hili. Kufika
huko wakaambiwa wana wana jini anatafuta damu na kuanza kutibiwa kwa kutaka
kumtoa jini huyo, hali ambayo iliwazidishia maumivu kihisia hadi wakaamua
kujiua. Kumbe ambacho hawakujua kujiumiza huko siyo majini wala nini bali hizo
ndizo athari za kuwa na maumivu makali ya kihisia.
Tatizo la mtu kujiumiza
mwenyewe kwa lengo la kupata nafuu, halihusiani na kulongwa au nguvu nyingine
za giza. Ni tatizo ambalo kisaikolojia linaelezeka kabisa. Ingekuwa
halijanipata, ningeweza kusema, huenda lina nguvu za giza ndani yake kama wengi
wanavyofikiri. Lakini nimelishuhudia moja kwa moja na nalijua vizuri.
Tunakutakia kila la kheri,
endelea kujifunza kila siku bila kuchoka kwa kupitia mtandao huu wa DIRA YAMAFANIKIO lakini hakikisha unawashirikisha wengine ili kuweza kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.