Jun 10, 2015
Ili uweze Kufanikiwa, Una Haja Ya Kujifunza Zaidi Juu Ya Kitu Hiki Katika Maisha Yako.
Je, unaweza kuandika orodha
ya tabia zako zote? Kama unaweza kuziandika zitenge katika makundi mawili.
Kundi moja liwe la zile ambazo zinakusaidia na zenye manufaa kwako hata kwa wengine na kundi la pili ni zile
ambazo hazina maana na hata zinawauzi na kuwakera watu wengine
sana.
Kama utafanya zoezi hili kwa
uaminifu huku ukiamini hakuna atakayeiona orodha yako , kuna mambo mawili
huenda ambayo utafikiria kuyafanya. Kwanza, utasikitika kugundua kuwa baadhi ya
tabia zako mbaya ni zile ambazo ungependelea kuziacha haraka ili kuboresha utu
wako. Jambo la pili ambalo litakujia katika fikra zako ni kuongeza orodha ya
tabia zako nzuri.
Unapoongeza tabia nzuri ni
lazima utambue haziwezi kuwa kuwa tabia zako kwa kuziandika tu katika orodha.
Katika zoezi hili watu wengi wenye akili timamu hupendelea kuwa na tabia nzuri
nyingi zaidi. Ni watu wachache tu ambao huweza kufikiria kuongeza tabia
zisizofaa.
Katika makala hii tutajadili
jinsi mtu anavyoweza kujifunza tabia mpya na namna anavyoweza kuziacha tabia
zisizo nzuri. Hata hivyo, tunapozungumzia tabia huna budi kukumbuka kuwa
zinajumuisha tabia zinazojengeka katika akili ya mtu. Wala hatukusudii zile
tabia zinazoingia katika kundi la vitendo hisia kama vile mtu kusikia njaa
anapokaa muda mrefu bila kula chakula.
Lakini unapopata mawazo ya
kuongeza tabia nzuri ina maana unatambua umuhimu wa tabia katika maisha yako ya
kila siku. Hebu fikiria baadhi ya tabia ulizonazo. Asubuhi unaamka mapema,
unaoga na kupiga mswaki na kuvaa nguo na viatu. Pengine kabla ya kutoka
kitandani unaweza kufungua redio au televisheni ili kupata taarifa za habari.
Baada ya kujitayarisha unajipatia kifungua kinywa na kuondoka nyumbani kuelekea
kazini. Hizi ni baadhi ya tabia ulizojizoeza tangu ulipokuwa mtoto.
Mtu una tabia hizi
tulizozitaja na nyingine nyingi ambazo zote kwa pamoja hufanya maisha yako kuwa
mazuri nay a furaha. Kwa kawaida mtu hujikuta ana tabia nyingi na utaratibu wa
maisha ambazo zimemwingia na kumvaa zenyewe na pengine bila kufanya juhudi ya
kuzipata ama kuzifikiria.
Tabia zote hizo zinaweza kuwa
kama vile ucheshi na kuzungumza vyema na watu, kuheshimu wanaokuzidi umri na
kustahi wadogo, ukarimu na huruma kwa watu, uadilifu, staha, uaminifu na
nyingine nyingi.jambo muhimu katika maisha ni kuzidumisha na kuboresha zaidi.
Kudhibiti mfumo wa kupata
tabia tukumbuke kuwa kwa kufanya mazoea fulani tunaweza kusitukia tumebadili
baadhi ya tabia. Inabidi tuwe makini kuepuka kujifunza tabia mbaya. Hii ni kwa
sababu tabia mbaya hutupotezea wakati na kutufanya tushindwe kupata mafanikio
katika maisha. Aidha ni dhahiri kuwa zipo tabia zinazoboresha mienendo yetu na
kutufanye tupate mafanikio makubwa katika maisha.
Kumbuka kuwa kwa vile
umeshakwisha kuwa mtu mzima juhudi za kuunda tabia mpya ambazo zitafanya maisha
yako yawe mepesi zinakutegemea wewe
mwenyewe. Ulipokuwa ungali mdogo misuli na mfumo wako wa neva za hisia ulikuwa
haujakomaa kiasi cha kukuwezesha kukabiliana na mazingira na kujenga tabia zote
ambazo ni muhimu kwa maisha yako.
Wakati ule kila hatua ya
maendeleo ya kupata tabia mpya ilitegemea mafunzo kutoka kwa wazazi, walimu na
watu wengine waliokuzidi umri. Maadhali sasa umekua, wewe mwenyewe unaweza
kufahamu sababu za kujenga tabia mpya. Ili kuunda tabia mpya unahitaji kuwa na
dhamira na utashi wa dhati.
Licha ya utashi mkubwa jambo
la pili ni kuandaa utaratibu thabiti utakaokufanya uitende tabia hiyo mara kwa
mara ili uweze kujenga mazoea ya
kujiridhisha kuwa una chokifanya kitasaidia kuimarisha hiyo tabia.
Kanuni za kujifunza tabia
mpya, kujenga tabia mpya na kujifunza kitu kipya ni kitu muhimu san asana kwako.
Maana ya kujifunza ni nini? Kujifunza ni kujipatia mwelekeo fulani kikamilifu
katika mfumo wa neva ya ufahamu. Hivyo kujipatia tabia mpya ni kujifunza kwa
kufuata kwa kanuni kuu mbili zifuatazo
- Kwanza kuwa na matakwa thabiti ya kujifunza.
- Pili kuandaa mpango au utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ya kutenda tabia hiyo mpaka uimudu kuitekeleza kwa usahihi.
Hebu tutumie mfano ufuatao
ili kuelewa jinsi ya kutumia kanuni hizi:-
Kulikuwa na mtu aliyekuwa
akifanya kazi katika mji na akiishi katika kijiji cha mbali. Hivyo kila siku
asubuhi alikuwa akiondoka nyumbani na kutembea kuelekea kazini. Na jioni
hivyohivyo akipata taabu kwa kutembea kurudi nyumbani. Alikuwa amechelewa
kufika kazini asubuhi na jioni pia alichelewa kurudi nyumbani.
Wakati huohuo kulikuwa na
jirani yake aliyekuwa akitumia baiskeli kwenda kazini na kurudi nyumbani. Jambo
hili lilimfanya Yule jirani yake ajiulize afanye nini kwa kuwa alikuwa hajui
kuendesha baiskeli. Hata hivyo alikiri moyoni kuwa ingekuwa vyema kiasi gani
kama angeweza kwenda na kurudi kazini kwa baiskeli kama wenzake.
Kama ungekuwa wewe ungefanya
nini? Hapana shaka ungeamua kufanya kama
jirani yake kutumia baiskeli. Hivyo utakuwa na hunabudi kujifunza kuendesha
baiskeli. Hii ni hatua ya kujifunza tabia mpya ya kuendesha baiskeli, hatua ya
kwanza katika dhamira ya kujifunza tabia hii mpya itakuwa ni kujizatiti katika utashi wako.
Hatua ya pili utaanza
kujifunza jinsi ya kukaa juu ya baiskeli kwa uwiano ulio uzito sawa ili
usiegemee upande moja na kukufanya ukaangika. Kisha utaanza kujifunzakuendesha
baiskeli. Hatua ya tatu itakuwa ni kuweza kutambua kuwa ili uweze kuendesha
baiskeli huna budi kufanya mazoezi.
Hivyo, utalazimika kupanga
muda na kufanya mazoezi ili kuuzoesha mfumo wako wa neva uwe umejifunza na
kukuwezesha kuimudu tabia hii mpya.hata katika mafanikio, ili uweze kufanikiwa
ni lazima ujifunza juu ya tabia bora za mafanikio zitakazoweza kukufanikisha. Utaweza
pia kujifunza tabia mbaya kwa kufuata pia hatua kama hizi.
Kanuni za kuacha tabia mbaya
kama vile mtu anavyoweza kujifunza tabia mpya pia kuna njia ya kupangua na
kutuplia mbali tabia usiyoipenda. Hapana shaka unaelewa jinsi mtu anavyosahau
haraka jambo analolijua anapoliacha kabisa kulitenda kwa muda. Hii ndiyo njia
unayoweza kuituumia ili kuacha tabia ambayo hupendi kuendelea nayo.
Tunaposema tabia mbaya tuna maana
ule mwenendo ulionao unaowaudhi watu wengine na kuwafanya wapoteze imani na
upendo kwako au ile tabia ambayo inaweza kukuathiri afya yako. Unapokusudia kuiacha
taba mbaya unaweza kufuata tabia zifuatazo:-
Kwanza, uwe na nia au utashi
thabiti wa kuiacha kabisa tabia hiyo. Pili, jiaminishe katika nafsi yako na
ujidhihirise kikamilifu na uamuzi wako kwa nini uumeamua kuiacha hiyo tabia na tatu, fanya mazoezi ya kuacha
kuifanya hiyo utabia na hakikisha imetoka kabisa katika mfumo wako wa neva.
Hitimisho.
Tabia ndiyo inayomtofautisha
binadamu na mnyama. Hivyo, kadri mtu aavyokuwa na tabia njema ndivyo kadri
anvyouimarisha ubinadamu wake na mafanikio kwa ujumla. Kila mtu anawajibika
kuhakikisha anaimarisha utu wake kwa kuongeza tabia bora na kuacha tabia mbaya
kama makala hii ilivyotufunza.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YAMAFANIKIO kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO
PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
MAKALA HII IMEANDIKWA NA ABEID SAKARA,
DAR ES SALAAM.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.