Jun 29, 2015
Kama Unataka Kuishi Maisha Ya Furaha Na Mafanikio? Hakikisha Unafanya Uchaguzi Huu Katika Maisha Yako.
Maisha
uliyonayo yanaweza yakawa mazuri sana ama mabaya kutokana na aina ya uchaguzi
unaofanya juu ya maisha yako kila siku. Mara nyingi uchaguzi tunaofanya katika
maisha yetu ndiyo huwa unaamua zaidi maisha yetu yaweje. Kama uchaguzi
unaofanya ni mbaya, ni wazi maisha yako yatakuwa mabaya na kama uchaguzi wako
ni mzuri basi maisha yako yatakuwa mazuri hivyohivyo hakuna atakayezuia hilo.
Kwa
kuwa uchaguzi wowote tunaofanya katika maisha yetu unakuwa una athari ni vizuri
tukawa makini kidogo na uchaguzi wa mambo tunayofanya kila siku. Nikiwa na
maana kuwa inatakiwa tujue kama kuna jambo tunalifanya ni muhimu kutambua lina
athari zipi kwetu. Kama tumeamua kufanya kitu fulani tuanze kwa kutafakari
matokeo yake kwanza. Hivyo ndivo tunavyotakiwa kufanya ili kuwa na uchaguzi
sahihi katika maisha yetu.
Kwa
uchaguzi sahihi tutazidi kufanya maisha yetu kuwa bora siku hadi siku.
Ikumbukwe pia kila kunapokucha tunanya aina nyingi sana za chaguzi ambazo
zinaamua hatima ya maisha yetu. Mara nyingi huwa ni watu wa kuchagua mavazi,
nguo za kuvaa, njia na mambo mengineyo mengi. Sasa ikiwa tunachagua mambo haya,
kwanini tusiwe na uchaguzi juu ya maisha yetu? Je, unajua ni aina gani ya
uchaguzi sahihi tunaotakiwa kuufanya katika maisha yetu ili kufanikiwa zaidi?
1. Chagua kuishi sasa.
Hii
ndiyo siri ya wewe kuweza kufurahia maisha yako. Hautaweza kufurahia maisha
yako na kuyaona katika uzuri wake halisi ikiwa unaishi kwa fikra sana za siku ziliyopita
ama siku za nyuma zaidi. Kwa kuishi kwako sasa, kuishi kwa kutokuwa na hofu
sana juu ya kesho yako, hapo utakuwa unafanya uchaguzi sahihi utakao weza
kubadilisha maisha yako na kuwa ya furaha na yenye mafanikio kwako pia.
2. Chagua kuishi maisha yasiyokuumiza.
Acha
kuishi maisha ya kuumiza utaumia sana. Ili kufanikwa kwa hili, jifunze kutokuyachukulia
mambo kwa ujumla ili usiweze kuumia zaidi. Ikiwa mtu atakwambia wewe ni mbaya,
hufai hiyo yote inaweza ikawa sawa kulingana na mtazamo wake. Hapo lakini wewe
usije ukachukulia huo ndiyo ukweli na kuanza kuumia na kujiona kweli hufai.
Fuata ukweli ulio ndani yako kuhusu wewe na siyo vinginevyo.
3. Chagua kuishi maisha ya ukarimu.
Haijalishi
mtu amekufanyia nini katika maisha yako kitu kikubwa cha kujifunza nikuwa
mkarimu kwa wetu wengine. Unapokuwa mkarimu unakuwa unaishi maisha ya utulivu
ambayo mara nyingi yanakuwa hayana msuguano zaidina wengine katika maisha yako.
Kwa kuishi maisha hayo yatakusaidia kukupa furaha na nguvu ya kufanikiwa. Hivi
ndivyo unavyotakiwa kuishi na kuwa hivyo.
4. Chagua kuishi kwa kufanya mambo yako
kwa uchache.
Ikiwa
utajifunza kumudu tabia hii basi utaweza kuishi maisha safi ya furaha ambayo
wewe mwenyewe utakuwa ni wazi unayafurahia kwa vyovyote vile iwavyo. Jifunze katika
maisha yako kuongea kidogo na kuwa msikilizaji sana. Jifunze pia kula chakula
kiasi ili kukujengea afya bora zaidi. Mambo mengi jaribu kuyafanya kwa kiasi
hiyo itakuwa ni siri mojawapo ya kuweza kukupeleka kwenye mafanikio.
5. Chagua kufanya mambo mapya.
Hautaweza
kufanikiwa kama utakuwa unafanya mambo yaleyale siku zote. Ili kuweza
kufanikiwa unalazimika kuchagua kufanya mambo mapya ambayo hujayazoea. Katika
kufanya mambo mapya ni lazima kujitoa mhanga na kukabiliana na kila aina ya
changamoto ili kuweza kufanikiwa, vinginevyo itakuwa ni ngumu sana kuweza kumudu
kuleta mafanikio tunayoyataka katika maisha yetu.
Tunakutakia kila la
kheri katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO
kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA
MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.