Jun 11, 2015
Njia 4 Za Kuondoa Mfadhaiko Wa Mawazo.
Mawazo ni jambo la kawaida
kwa binadamu, huwa inategemea mawazo hayo ni ya namna gani. Wataalamu wa
saikolojia wanasema kuna njia mbalimbali za kuweza kuondoa mfadhaiko wa mawazo ambazo
ukiweza kuzitumia zitakuweka huru zaidi na kuweza kuishi maisha ya furaha ambayo
unayahitaji katika maisha yako.
1.Kuwa
na mawazo chanya.
Njia ya kuongea wewe
mwenyewe ni moja ya suluhisho la kuweza kuondoa mfadhaiko wa mawazo. Kuna wakati
inatokea unaongea mwenyewe kwa sauti au moyoni kuwa nitafanya hiki au kile. Mtazamo
chanya utakusaidia sana kurudi katika hali yako ya kawaida na kuweza kabisa
kujiweka sawa.
Hivyo unashauriwa kujifunza
kubadilisha mawazo hasi kuwa chanya. Kwa mfano unaweza kujisemea nitafanya hivi
au nitafanya vizuri zaidi ya hivi hata kama unaona mambo yanakwenda vibaya. Kwa
kuwa na mtazamo chanya kutakusaidia sana wewe kutoa mfadhaiko katika maisha
yako.
2.
Tafuta unafuu.
Mara nyingi ukiwa na
mfadhaiko wa mawazo hukufanya ujisikie vibaya, hivyo unatakiwa utafute kitu
ambcho kutakuletea shinikizo la mawazo. Hivyo basi, unashauriwa kutumia muda
usiopungua dakika 15 kwa kufanya vitu vifuatavyo kuwasilina na marafiki kwa
kutuma meseji au kusoma vitabu, magazeti na majarida.
Vilevile sikiliza muziki,
andika vitu ambavyo unatakiwa kufanya katika maisha yako. Kwa kufanya hivyo
utakuwa unajitafutia unafuu wewe mwenyewe, hali itakayoweza kukufanya sasa
uweze kujihisi kuondoka kabisa katika huo mfadhaiko wa kimawazo unaokutesa.
3.
Tumia njia za dharura.
Kuhesabu moja hadi kumi,
vuta pumzi kwa ndani kwa nguvu mara tatu au tano, jiondoe kabisa katika mfadhaiko
huo kwa kusema moyoni nitafanya baadae, nenda katembee. Usiogope kusema
samahani kama umekosea lakini pia weka kengele ya kukumbusha kwa dakika 10
kabla ya kujihadhari kuchelewa kuamka asubuhi.
Nyingine jiulize niyafanyaje
matatizo makubwa na kuyafanya kuwa
madogo, jibu simu mara moja kwa siku, jibu barua pepe au barua, epuka kufanya
vitu vingi sana kwa wakati mmoja. Kama ni kuendesha gari endesha kati kati ya
barabara ambayo haina vurugu sana.
4.
Kupumzika.
Kumpumzika ni zaidi ya kukaa
na kuangalia kipindi katika runinga. Ili kuondoa mfadhaiko unaotakiwa kupumzika
ufanye hii kitu ndani ya akili na mwili wako. Wakati wa kupumzika kuna michezo mbalimbali
kama yoga ambayo unaweza kuifanya na kutafakari kwa kina zaidi kile unachoona
kinakupa mfadhaiko.
Katika hili tunaona watu
wengi hulifanyia kazi na kufunza mfano kitendo cha kuvuta pumzi kwa ndani inaweza
ikawa ni njia nzuri ya kuweza kujipumzisha hasa ukiwa nyumbani.
Tunakutakia kila la kheri katika
safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.