Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, November 4, 2015

Mambo 12 Ambayo Ni Lazima Uyafanye Katika Maisha Yako.

No comments :
Kwa kawaida kila mtu ana kanuni, taratibu au ambazo amejiwekea na kuishi nazo. Kanuni hizi zinaweza zikawa ni za kupanga au bahati mbaya lakini zipo. Ndio maana utakuta mtu yule maisha anayoishi yanatofautiana kwa kiasi kikubwa sana na mtu mwingine.
Lakini hata hivyo pamoja na kanuni au sheria hizo kuweza kutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine, huwa yapo mambo ya lazima ambayo kila mtu analazimika kuyafanya katika maisha yake. Haya ni mambo ya lazima ambayo unatakiwa uyafanye siku zote na mara kwa mara katika maisha yako:-
1. Jifunze kuwa mtoaji kuliko mpokeaji.
2. Onyesha heshima kwa kila mtu.
3. Linda maneno yako sana. Acha kuongea ongea hovyo.
4. Fanya mambo yako kwa ubora kila siku.
5. Kuwa na muda wa kuwasikiliza wengine.

DIRA YA MAFANIKIO
WAPE MOYO WENGINE PALE WANAPOKATA TAMAA.
6. Wape wengine moyo pale wanapokata tamaa.
7. Unapokosea, sema samahani kwa yule unayemkosea.
8. Kuwa mkarimu.
9. Jifunze kujisamehe wewe na kuwasamehe wengine.
10. Mara nyingi jifunze kuwa mtu wa shukrani katika maisha yako.  
11. Jenga, tabia ya kujifunza kila siku.
12. Kuwa king’ang’anizi wa maisha yako mpaka ufanikiwe.
Hizo ndizo kanuni rahisi tu, ambazo unaweza ukaishi nazo katika maisha yako na kuishi maisha ya ushindi na amani.
Nakutakia siku njema na maisha ya amani yawe kwako na endelea kujifunza kupitia DIRA YAMAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment