Aug 29, 2016
Kama Unataka Kufanikiwa Ni lazima Uongozwe Na Jambo Hili Kwanza.
Kisaikolojia kila binadamu anaongozwa na nafsi mbili ambazo ni
hisia na Hoja .
Hisia ni hali ya utabiri isiyokuwa na uhakika wa jambo. Huenda
ikawa na ukweli au uongo. Mara nyingi hisia hutawaliwa na tamaa ya macho au
mwili. Hoja ni uhalisia wa jambo au mambo yanayoonekana kwa macho. Ni mambo
yenye uhalisia kimtazamo. Mtu yeyote anayeongozwa na hoja hufanikiwa kwa 100%
lakini mtu anayeongozwa na hisia au tamaa ni kama mcheza kamari, anaweza kupata
au kuliwa au kushindwa kabisa.
Hisia kama tulivyoona ni tabia ya kimaumbile aliyonayo mtu. Kila
mtu ana tamaa ya kupata mafanikio katika maisha yake. Hiyo ni hisia haina hoja
ya msingi katika kuleta mafanikio. Mafanikio ili yapatikane lazima iwepo hoja
ya msingi itakayo tawala katika maneno na vitendo vya mtu katika maisha
ya mtu. Kivipi kuwe na hoja za msingi?
Ukitaka mafanikio lazima ujenge hoja za msingi na zenye
mashiko. Ni lazima uwe tayari kuizishinda hisia za matamanio katika maisha.
Uamue kuifanya akili yako iongozwe na hoja badala ya kuongozwa na hisia.
HOJA ZA MSINGI ZITAKUSAIDIA KUFANIKIWA. |
Hoja humfanya mtu kuwa na uhakika wa kile anachokifanya. Kuwa na
‘data’ sahihi za kile anachofanya.
Humfanya mtu kufanya kila kitu kwa ufanisi MKUBWA.
Hoja humfanya mtu kujiamini na kuthamini kile anachofanya. Hoja
humpa heshima na kumfanya athaminike na jamii kutokana na kufanya vitu sahihi
na vyenye tija kwa jamii.
Hisia au tamaa humfanya mtu kufanya maamuzi yanayompelekea
kujuta baadae katika maisha take.
Hisia zikimtawala mtu hufanya vitu vya aibu na kumdhalilisha katika
jamii kama kuiba, kubaka, kulawiti, kusema uongo kwa manufaa binafsi, kula mali
ya haramu bila Hofu. Hisia zikimtawala mtu hukosa kujiamini na kujiona mwenye
mapungufu na kukosa ujasiri.
Katika kumalizia somo letu naomba kutoa angalizo kuwa kabla ya
kufanya maamuzi katika jambo lolote unalohitaji kufanya kwanza jiulize
unayotaka kufanya je, yanaongozwa na hisia au hoja? Kama yanaongozwa na hisia
au tamaa kamwe usifanye jambo hilo na kama jambo hilo linaongozwa na hoja
hakika lifanye maana litakufaa katika maisha yako.
Naomba tuishie hapa kwa leo tukutane muda ujao kwa ajili ya
kujifunza zaidi na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza kwa kina.
Tupo pamoja,
Shariff H. Kisuda (Mzee wa Nyundo)
Simu; 0715 079 993,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.