Aug 19, 2016
Hatua Muhimu Za Kukusaidia Kutoka Kwenye Madeni.
Wapo
watu wengi ambao huwa hawafikiri sana kwamba, kujiingiza kwenye madeni mengi ni
kitu cha hatari. Watu hawa huja kugundua kwamba wapo kwenye hatari hiyo mara baada
ya madeni hayo kuwalemea sababu ya wingi wake.
Kutokana
na madeni hayo kuwa mengi, na kushindwa kuyalipa, hapo sasa ndio majuto na
kilio huanza kutanda. Na wengi huanza kujilaumu kwa nini walikopa mikopo mingi,
mikopo ambayo kama inawatesa kwa sasa, kutokana na kushindwa kuilipa.
Najua
umeshawahi kukutana na watu ambao wana mizigo mingi na mikubwa ya madeni. Inawezakana
watu hawa walikuwa jirani zako, ndugu au pengine hata wewe mwenyewe. Je,
ulishawahi kujiuliza inapokutokea hali kama hii ni kitu gani unachotakiwa
kufanya?
Leo
kupitia makala haya, twende kwa pamoja kujifunza hatua muhimu za kukusaidia
kutoka kwenye madeni.
1. Weka mipango imara.
Hatua
ya kwanza itakayokusaidia kutoka kwenye madeni yako, ni kule kuamua kuweka
mipango imara ya kukutoa kwenye madeni yako uliyonayo. Utaweza kulifanikisha
hili vizuri, ikiwa utakaa chini na kupitia kiwango cha pesa unachotumia,
ukilinganisha na kile kinachoingia.
Weka mipango imara ya kutoka kwenye deni ulilonalo. |
Kwa
mfano, inawezekana kabisa upo kwenye madeni kwa sababu unatumia pesa nyingi
hovyo. Kwa hali hiyo hukupelekea matumizi yazidi kipato na kukufanya kukopa. Hivyo,
hakuna namna nyingine zaidi ya kuweka mipango imara ya kubana matumizi na
kuweza kuondokana na madeni.
2. Tafuta chanzo kingine cha pesa.
Njia
nyingine nzuri ya kuweza kuondokana na madeni uliyonayo ni kutafuta chanzo
kingine cha pesa. Acha kung’ang’ania kuwa na chanzo kimoja cha pesa, hiyo
inaweza ikawa ni hatari sana kwako katika harakati za kujikwamua kutoka kwenye
madeni.
Kwa
mfano, kama umeajiriwa tafuta namna yoyote ile uwekeze kwenye hiyo biashara. Halikadhalika,
kama umejiajri kwa kufanya biashara yako mwenyewe, jitahidi baada ya muda uwe
na biashara nyingine. Kwa kufanya hivi itakusaidia kuweza kutoka kwenye madeni.
3. Punguza matumizi yasiyo ya lazima.
Mbali
na kuweka mipango imara na kutafuta chanzo kingine cha pesa, pia unaweza kutoka
kwenye deni ulilonalo kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Wengi wetu mara
nyingi huwa ni watu wa matumizi mengi pasipo kutarajia.
Unawezaje
kutoka kwenye matumizi yasiyo ya lazima? Kwanza, unaweza kuepuka matumizi
yasiyo ya lazima kwa kuepuka kununua vitu visivyo vya lazima sana kwako. Pili, ni kuwa makini na
kila pesa inayotoka kwa kuiwekea kumbukumbu. Kwa hatua hiyo, inaweza kuwa msaada
kwako kukutoa kwenye madeni.
4. Anza kulipa madeni makubwa.
Kama
madeni uliyonayo ni mengi, ni vizuri kuya orodhesha madeni yako na kuanza
kuyalipa madeni yale makubwa. Kwa kuchukua hatua hiyo utajikuta mahali, umeweza
kuuotoa mzigo wa madeni ambao ulikuwa unakusumbua kwa muda mrefu.
Kwa
kuhitimisha makala haya, naomba niseme hivi; mikopo ni mizuri ikiwa itatumia
vizuri kwa malengo maalumu. Endapo utaitumia vibaya inaweza ikawa ni mzigo
mkubwa na kugeuka kuwa deni.
Kama
mkopo uliouchukua umekuwa deni, tafadhari hizo ni baadhi ya hatua ambazo unaweza
kuzitumia kutoka kwenye madeni uliyonayo. Lililo kubwa kwako, fanyia kazi hicho
ulichojifunza na chukua hatua.
Nikutakie
siku njema na kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Chukua hatua sitahiki za
kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com
kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Blog;
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.