Aug 1, 2016
Kwanini Siku ya Jumatatu Huitwa "BLUE MONDAY"?
Mara
kadhaa nadhani utakuwa umewahi kusikia mtu anakuuliza ya kwamba blue monday kwa
upande wako ikoje? Bila hata kujua kuwa blue monday humanisha nini mara kadhaa
umekuwa ukijibu ya kwamba blue monday yako ipo poa. Ila kimisingi hauna haja ya
kujibu hivyo endapo haufahamu maana yake . Basi kaa sawa ili nikuleze kwa kina
maana ya hii siku.
Blue monday hutengenezwa kuanzia siku ya ijumaa, jumamosi na jumapili. Siku hizi tatu huitwa ‘weekend’ kwa kimombo kwa maana ya kwamba wiki imeisha. Siku hizi huitwa ni siku ya matumizi ya pesa na kula bata, Hata hivyo siku hizi za tatu huitwa ni siku za matumizi zaidi kuliko kuuingiza pesa.

Hapa ndipo lile somo la nidhamu ya pesa hupita
kushoto kwa kila baadhi yetu. Unajua ni kwanini siku hizi tatu hutengeneza
"blue Monday" hii ni kwasabau ya hapa huwa hakuna matumizi sahihi ya
kifedha. Hapa ndipo panatufanya ya kwamba tusijue ni yapi ni matumizi ya lazima
na yapi ni si matumizi ya lazima kwa kila fedha ambayo tunaitumia.
Hivyo jambo la msingi ili kuibadili blue Monday ili kuwa ni siku njema kwako huna budi kufanya yafutayo;
Mosi ni kwamba panga malengo yako katika mtiririko ambao unaeleweka, mtiririko huo uwe katika mfumo wa kujua ni masaa yapi ni uzalishaji Mali, pia ni masaa mangapi ni maalumu kwa ajili ya kupumzika.
Kwani maisha ya binadamu yanaendeshwa kwa
asilimia kubwa kwa ratiba ambayo mtu huenda akawa amejipangia au kupangiwa
katika kufanya jambo fulani. Hata hivyo tukumbuke ya kwamba matumizi sahihi ya
muda ni chachu ya kupata kile ambacho unachokihitaji. Jambo la msingi la
kujiuliza ni kwamba unatumia vipi muda wako.
Pili jambo la kuzingatia ili kuamka siku hii ya blue Monday ukiwa hauna mawazo sana. Unatakiwa kuwa na bajeti yako ambayo itakusaidia kukuongoza kwa namna moja ama nyingine. Bajeti hii ndiyo ambayo itakupa mwongozo na mstakabadhi wa matumizi yako ya fedha. Bajeti ya Matumizi hayo itakuonyesha kabisa ni asilimia ngapi ya fedha inatakiwa itumike katika siku hizo za mapumziko, ili kuepuka na mawazo yasiyokuwa na lazima. Ifanye siku yoyote katika katika wiki iwe ni siku ambayo ina manufaa kwako na wengne.
Pia nikusihii sana ewe mdau na msomaji wa makala haya ni kwamba unatikiwa kufanya vitu vyako kwa malengo, malengo hayo ndio yatakayokufanya uweze kuona nuru ya maisha yako ni wapi ni wapi ambapo unaelekea?
Ndimi Mjenzi Wa Taifa kupitia Uandishi (MTU); Afisa Mipango Benson Chonya.
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Blogu. dirayamafanikio.blogspot. com

Blogu. dirayamafanikio.blogspot.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.