Aug 2, 2016
Tabia Za Pesa.
Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini
wengine wana pesa na kwa nini wengine hawana pesa? Kwa nini wewe huna
pesa ulikosea wapi au unakosea wapi? Ungana nami mzee wa Nyundo nikuhabarishe.
Kama ambavyo binadamu wana tabia zao
zinazowaongoza na kuwafanya kuwa tofauti na wengine, pesa nayo ina tabia zake
na kanuni zake pia. Pesa ina sheria zake kuu nne:-
1. Namna ya kuitafuta na
kupatikana kwake.
2. Namna ya kuikuuza au
kuifanya ikue na kuongezeka.
3. Namna ya kuilinda iendelee
kuepo na kudumu.
4.Namna ya kuitumia pesa.
Kisaikolojia kila binadamu awaye
anajua namna ya kutafuta pesa na kutumia pesa. Ila tatizo na tofauti za hawa
binadamu ziko katika tabia na namna zingine mbili kuikuza na kuilinda pesa na
hapa ndipo hutokea tofauti kati ya wasionacho/masikini na walionacho/ matajiri.
Daaah mzee wa nyundo leo umetoa kali. Kama
umechungulia akili za watu vile. Jamani tuko pamoja au wengine nimewaacha njia panda
ya Himo? Yes, wataalamu wa mambo ya maisha ya mwanadamu na mafanikio wamebaini
katika tafiti zao kuwa KUNA UWEZEKANO WA KUPATA PESA KIRAHISI LAKINI NI NGUMU
SANA KUPATA UTAJIRI KIRAHISI.
Why this? Tulia nikupe siri za
mafanikio ya utajiri na mtu kupata pesa ni vitu viwili tofauti sana. Na hii
ndio maana mtu anaweza kuzaliwa katika familia ya kitajiri na akawa masikini
wakati kuna mtu mwingine kazaliwa familia ya kimaskini na leo hii ni Tajiri
mkubwa sana.
Mfano kwa Tanzania ni Bakhresa na
Mengi ni watu waliozaliwa katika familia duni lakini kwa kujua kwao na
kuzifanyia kazi tabia za pesa. Leo wamekuwa ni watu wa tofauti na kuwa
Matajiri. Hakuna njia ya mkato waliotumia kupata mafanikio waliyonayo.
Wamefuata sheria za pesa baada ya
kujua tabia za fedha. Nawe unaweza kuwa Tajiri ukiamua kubadili matumizi yako
ya pesa na kujua namna ya kuzifanya pesa zizae na kukua na pia kujua namna ya
kuilinda pesa. Nitaikuzaje pesa na kuilinda Kisuda? Nawe unanichanganya akili
yangu leo bro. Sikusomi kabisa. Daaah!!!
Kisaikolojia elimu zote hufundishwa
darasani ispokuwa elimu ya pesa pekee ndiyo haifundishwi darasani. Kivipi
tena? Mzee wa Nyundo leo umeamua kunichosha kichwa changu.
Elimu ya pesa hufundishwa pekee
mtaani hata vyuo vinavyofundisha biashara na uchumi havifundishi hii Kitu. Ni
mtaani pekee na kwa Kisuda mzee wa nyundo ndio mahali pekee unaweza kupata elimu
hii muhimu na ya kipekee. Kivipi jibu rahisi, kesho amka asubuhi kisha mwendee
tajiri mkubwa yeyote aliyeko mtaani kwako kamuuliza ni nini siri ya utajiri
wake na mafanikio yake?
Hakika 100% hakuna jibu la
maana atakalokupa zaidi ya kukuona kama mwanga na mchawi katika maisha
yake. Kwa nini hii hutokea? Hakuna anayetoa siri ya mafanikio yake ya
kipesa kwa hofu ya kuzidiwa na wewe.
Siri wanazijua ila kukwambia wewe ni
big no that's why Matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kusaga
rumba kila mwaka maisha ni yale yale no changes. Kila akijitahidi hapa na pale
anaishia kubadilisha mboga na nguo za sikukuu na mwaka mpya.
Nihitimishe somo langu kwa kukupatia
njia 5 za kuweza kufanya ili umiliki pesa na kuwa na uhuru wa kiuchumi au tajiri.
1.Weka AKIBA hii ni Kitu muhimu sana
katika hatua za kukamata pesa. Weka Akiba angalau 10% kwa kila pato lako. Bila
kujali ni kubwa au dogo kiasi gani tenga 10% kama AKIBA. Na kuna msemo moja
huwa napenda kuutumia katika maisha yangu. Usiweke AKIBA kiasi kinachobakia
baada ya matumizi Bali tumia kinachobakia Baada ya kuweka AKIBA yako ya 10%.
Shika hii Mimi imemisaidia kufika malengo yangu mengi sana.
2.Tafuta maarifa kwa kusoma vitabu na
kuhudhuria semina na mafunzo ya watu sahihi na wenye mawazo chanya.
3. Wekeza AKIBA yako katika miradi na
biashara zinazolipa baada ya kupata maarifa na kujiridhisha vyakutosha.
4. Dhibiti matumizi yako ya Pesa kwa
kuwa na Bajeti ya nini ununue na kwa nini ununue. tambua matumizi ya muhimu na
matumizi yako ya lazima. Yape kipaumbele matumizi ya lazima kuliko matumizi ya
muhimu hii nayo imenisaidia sana mmi Kisuda kutimiza malengo na ndoto
zangu Leo najivunia utambuzi huu katika matumizi kuhimu na ya lazima.
5. Kuwa na matumizi mazuri ya muda
wako. Watu wengi hawana matumizi sahihi ya muda wao. Sio ni lazima uwe na
ratiba itakayokuongoza katika siku yako. Kila binadamu ana masaa 24 lakini
wachache hufanikiwa na wengi hawafanikiwi. Hapa kuna siri moja kubwa sana.
~Matumizi sahihi ya masaa au muda wako wa ziada ndiyo huamua eidha
ufanikiwe au usifanikiwe. mzee wa nyundo umetisha sana Bro.
Siri ya wewe kuwa tajiri na kumiliki
pesa zingatia vitu hivyo ni lazima ufanikiwe. Ukishindwa itabidi ukatambikiwe
au ukaoge maji ya bahari.
Imeandikwa na mtaalamu wa masuala ya saikolojia na mafanikio SHARIFF
KISUDA. Fuatan naye katika ukurasa wake wa face book, Shariff Kisuda ujifunze
Siri za mafanikio kila siku.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.