Aug 18, 2016
Mawazo Muhimu Unayotakiwa Kuwa Nayo Ili Kukuza Biashara Yako.
Biashara
shaka naongea na wewe katika siku hii ya leo ukiwa kwenye biashara yako au
pengine ukitarajia kuanza biashara hivi punde. Kama uko kwenye biashara,
pengine naongea na wewe ukiwa kwenye harakati za kutafuta wazo bora litakalo kusaidia
kukuza biashara yako na kuwa ya mafanikio makubwa.
Kama
uko kwenye hali ya kutafuta wazo bora litakalokusaidia kukuza biashara kwa
kusoma makala haya itakusaidia sana. Ieleweke kwamba kuanzisha biashara na kuikuza
biashara hadi ukaiona inaleta matunda ni vitu viwili tofauti. Wengi hujitahidi
sana kuanzisha biashara lakini linapokuja suala la kukuza, hushindwa kwa sababu ya kukosa mawazo muhimu.
Kwa
namna yoyote ile, mfanyabiashara anahitaji kuwa na mawazo muhimu yatakayomsaidia
kukuza biashara yake wakati wote. Haijalishi
udogo au ukubwa wa biashara husika, lakini mawazo bora ni nguzo muhimu ya
kuifanya biashara ikaendelea mbele na kutoa mafanikio makubwa.
Leo
kupitia makala haya hebu tuangalie mambo gani muhimu unayatakiwa kuwa nayo ili
kukuza biashara yako.
1. Tanua soko lako.
Biashara
yako itaweza kukua ikiwa utakuwa una wazo la kutanua soko lako kila wakati. Kwa
mfano, kama umekuwa ukiuza bidhaa zako ndani ya mtaa mmoja, ni vyema ukafikiri
namna ya kuzipeleka na mtaa wa pili. Kwa wazo hilo litakusaidia sana kukuza biashara yako kwa viwango vya juu.
Jenga mtandao wa kukuza biashara yako. |
2. Pata maarifa ya biashara.
Kila
wakati inabidi ujifunze kuunoa ubongo wako na kujifunza sana juu ya biashara
unayoifanya. Maarifa ni muhimu sana katika kuikuza biashara yako, vinginevyo
biashara hiyo ni lazima itadondoka. Hivyo, unatakiwa kujisomea vitabu au kuhudhuria
semina mbalimbali za kibiashara ili kufanikisha hilo.
3. Toa huduma za ziada.
Unaweza
ukaifanya biashara yako ikakuwa na kuwa ya mafanikio ikiwa utajifunza kutoa
huduma za ziada. Kwa mfano, unaweza ukawapa wateja wako zawadi ndogo ndogo kila
wanaponunua bidhaa. Hilo litawasaidia kuwavuta na kujikuta ukikuza biashara
yako siku hadi siku.
4. Tengeneza mtandao wa kibiashara.
Huwezi
ukasema unakuza biashara yako na kusahau kukuza mtandao wako wa kibiashara. Ni lazima
kujitengenezea ‘netwek’ na
wafanyabiashara wenzako ya kukusaidia kukufanikisha. Hilo litakusaidia katika
kutatua changamoto na wakati mwingine hata kukuza bidhaa kwa urahisi.
5. Boresha bidhaa zako.
Mwisho,
ili uweze kukuza biashara yako, kwa vyovyote vile unalazimika kuboresha bidhaa
zako. Kila bidhaa unayoitoa ni lazima iwe ya viwango vya juu. Kwa hali hiyo
itapelekea utapata wateja wengi kila kukicha
na kusababisha biashara yako kuweza kukua.
Ikumbukwe
kwamba kutanua soko, kupata maarifa ya kibiashara, kutoa huduma za ziada, kutengeneza
mtandao na kuboresha bidhaa kila wakati, ni moja ya mawazo muhimu ambayo
unatakiwa kuwa nayo kila siku ili kukuza biashara yako.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku. Ila hakikisha unawashirikisha wengine waweze kujifunza zaidi.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.