Aug 30, 2016
Mambo Ambayo Watu Wenye Mafanikio Huyafanya Sana ‘Wikiendi’.
Kimsingi,
ipo tofauti kubwa sana kati ya watu waliofanikiwa na watu ambao hawajafanikiwa,
husani katika suala zima la matumizi ya siku za mapumziko hasa wikiendi.
Mara
nyingi watu waliofanikiwa huzitumia wikendi zao kwa manufaa zaidi ukilinganisha
na wale ambao hawajafanikiwa. Kutokana na matumizi haya ya muda huo wa
mapumziko ndio wakati mwingine huweza kuleta utofauti hata wa mafanikio.
Hebu
tuangalie watu wenye mafanikio huzitumiaje ‘wikiendi’
zao;-
1. Kuamka asubuhi na mapema.
Mara
nyingi watu wenye mafanikio, ratiba yao ya kuamka ipo pale pale bila kujali
kwwamba ni siku ya kawaida au ‘wikiendi’. Siku zote hujitahidi sana kuweza
kuamka asubuhi na mapema.
Hufanya
hivi kwa sababu wanatambua muda ni wathamani sana. Hivyo, hawako tayari
kupoteza muda kwa chochote zaidi ya kuamka mapema na kuanza kuwekeza kwenye
muda huo ili uwape faida.
2. Kujisomea.
Kati
ya kitu amabacho watu wenye mafanikio huhakikisha wanakifanya wikiendi ni
kujisomea. Kupitia kujisomea huko hujifunza mambo mengi ambayo yanawasaidia
katika kukua kimafanikio na kupambana na changamoto za maisha.
3. Kutafakari juu ya maisha.
Watu
wenye mafanikio katika wikiendi zao hawaishii kujisomea tu, bali wakati
mwingine kutafakari sana juu ya maisha yao. Hutumia muda huo kujiuliza wapi
walipotoka, wapi walipo na wapi wanapokwenda. Maswali hayo huwasidia kupiga
hatua nyingine kubwa ya kusonga mbele.
4. Kufurahia maisha na familia.
Pia
wikiendi kwa watu wenye mafanikio huzitumia sana kuwa pamoja na familia zao. Ni
wakati ambao hupenda kucheza na kwenda maeneo tofauti na nyumbani kama ‘beach’ au mbuga za wanyama, kufurahia
maisha na familia zao.
5.
Kuweka mipango sawa ya wiki lijalo.
Mara nyingi watu wenye mafanikio huzitumia
wikiendi zao, kwa kupanga mipango mipya ya wiki lijalo. Hapa hukaa chini na
kujiuliza ni mikakati gani ambayo wataichukua ili kufanya wiki lijalo liwe bora
na la manufaa zaidi.
6. Kufunga
mawasiliano yasiyo ya muhimu.
Hiyo haitoshi watu wenye mafanikio ‘wikiendi’ zao huwa hawapendi sana kuwa
na masiliano mengi kama ilivyo siku za kawaida. Kama ni simu wakati mwingine
huzifunga au huwa hawapendi kuwasiliana sana na wengine katika kipidi hiki
kifupi cha mapumziko.
7.
Kutoa shukrani.
Shukrani ni jambo lingine la pekee ambalo watu
wenye mafanikio hulifanya kwenye siku za mapumzikio. Ni kipindi ambacho huweza
kuishukuru jamii kwa kwa namna tofauti mfano kutoa zawadi au kutembelea
wagonjwa na mengineyo.
Kwa kifupi hayo ndiyo mambo machache ambayo
watu wengi wenye mafanikio huyafanya sana katika siku zao za mapumziko ya wiki.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.