Aug 10, 2016
Hii Ndiyo Dozi Sahihi Ya Maisha Yako Ya Mafanikio.
Mara
kadhaa unatakuwa umekuwa shahidi kwa namna moja ama nyinyine kwa kuona ya
kwamba mtu akiumwa ni lazima atafute matibabu ili aweze kupona ugonjwa ambao unamsumbua.
Hivyo
hivyo mtu huyo akipewa dawa anatakiwa
kuzitumia katika utaratibu ambao unaeleweka ili aweze kupona, utaratibu huo
ndio ambao huitwa dozi, dozi hiyo lazima mtu aifuate ili aweze kupona na endapo
atatumia kinyume na alivyoelekezwa na
mtalamu upo uwezakano mkubwa kuweza hudhurika zaidi au kupoteza maisha.
Kama
ilivyo kwa mgonjwa ili aweze kupona na kuimarika vizuri katika afya yake hana
budi mgonjwa huyo kuweza kufuata
utaratibu wa kutumia dozi ili aweze kupona.
Hata
kwenye safari yako ya mafanikio ndivyo ilivyo, unahitaji kupata dozi, dozi
ambayo ina misingi na utaratibu wake wa kuitumia. Wengi wetu tunamani kupata
mafanikio kwa haraka zaidi, huku tukisahau ya kwamba mafanikio ni hatua kwa
maana ya kwamba ni lazima tumalize dozi ndipo tupate mafanikio hayo.
Hivyo
nakusihi uweze kufuatana nami ili uweze kujua namna ya kuweza kupata dozi ya
mafanikio yako, pia suala si kupata dozi tu, bali uzitumie katika maisha yako, na si
kuzitumia tu bali uzitumie ili upone
ugonjwa wa dhiki, shida na taabu za
kimaisha ili uweze kupata mafanikio yako.
Vile
vile nisisitize kwa kusema ya kwamba ili uweze kufika ambapo unataka ya kwenda
kwa maana ya kupata mafanikio huna budi ya kuamini na kuwa mvumilivu na mbunifu
wa hali ya juu sana.
Ifuatayo ndiyo dozi sahihi ya safari
yako ya mafanikio.
1. Angalia matumizi yako ya muda
katika kutekeleza malengo yako.
Ipo
haja leo ya kujua mambo ambayo yatakusaidia kuweza kutimiza malengo yako. Watu
wengi huwa tunakosea sana hasa katika kujali na kuzingatia muda wa kutekeza
mambo yetu.
Kwa
mfano watu wengi licha ya kuwa na malengo huwa hatuweki ni kwa muda gani ndoto
yako itakuwa imekamilika. Mfano ili uweze kufanikiwa na kutimiza malengo yako,
kwa mfano unataka kuwa mfanyabiashara fulani ni lazima ujue ni muda gani utakuwa umetiza jambo lako. Hii ni muhimu sana
kuzingatia.
Hata
hivyo kuwa na maono ya muda (time limit)kwa kila jambo lako itakusaidia kuweza
kujua ni kwa namna gani utakuwa umetiza lengo lako. Hivyo nakusihi kwa kila jambo lako ambalo unatamani kulifanya
kwa hapo baadae ni lazima uwe umelipanga ni baada ya muda gani lengo hilo litakuwa limekamilika. Pia mara
kadhaa endelea kukumbuka msemo ule mtamu wenye kukutia hamasa ya kwamba ni
‘muda ni mali’ hivyo huna budi kulizingatia hilo.
2.
Jifunze kutoka kwa watu walifanikiwa
huku na wewe ukitumia njia ambazo ni za tofauti.
Mara
kadhaa tumekuwa ni watu kulamika sana hasa pale ambapo tumefeli kwenye jambo
fulani. Kulalamika huku mara kadhaa nimegundua ni kwa sababu kuu moja ya kwamba tumejifunza kwa watu ambao wamefeli.
Lakini
kufanya hivi mara kadhaa hutupa picha ya kwamba hata sisi hatuwezi hii ni
kutokana mtu fulani alifeli. Kufeli kwa mtu
mwingine katika jambo lake kwa asilimia kadhaa hutengeneza hofu ndani
yetu, hofu hiyo ni ile hofu ambayo utajiona ya kwamba hauwezi.
Hata
hivyo kama unataka kupata mafanikio jambo la kuzingatia ni kwamba unatakiwa
kupata ushauri kwa watu sahihi ambao wamekwisha fanikiwa kufanya hivi
inakusaidia kwani wao wana taarifa sahihi kuhusiana na jambo hilo.
Kwa
mfano unataka kufanya biashara ya kuuza chipsi ukiomba ushauri kwa mtu ambaye
anauza mkaa, muuza mkaa huyo atakwambia biashara hiyo ina hasara sana, lakini
sababu hizo sio za kweli kwa sababu hana taarifa sahihi, hivyo kama unataka
kuuza chipsi ni lazima uweze kumfuata mtu ambaye amefanikiwa katika biashara
hiyo kwani mtu huyo anazo taarifa kamili juu ya biashara hiyo.
Hivyo
nakusihi ili uweze kupata mafanikio huna budi kuayazingatia hayo kwa hali ya
juu sana, hasa katika suala la utekelezaji, kufanya hivyo kutukufanya uweze
kuwa mshindi wa maisha yako. Endelea kufuatana nami katika safu hii kila
wakati.
“Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra
sahihi” kwa kuendelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ndimi; afisa mipango Benson Chonya
Blogu;
dirayamafanikio.plogspot.com
Email;
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.