Aug 16, 2016
Mambo Ya Kuzingatia, Ili Kuifanya Akili Yako Ifanye Kazi Kwa Ufasaha Na Mafanikio Makubwa.
Naamini katika maisha, huwa inafika mahali
kila mtu anatamani akili yake ifanye kazi vizuri na imletee mafanikio makubwa.
Lakini hata hivyo, pamoja na matamanio hayo wengi bado huwa hawajui wafanye
nini au wachukue hatua zipi ili kuweza kuipa akili nguvu zaidi kila siku na
kufanya kazi kwa ufasaha.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, baada ya kufanya
utafiti kwa muda, walikuja kukaa chini na kuweka vigezo ambavyo kwa mtu akiviafuta
basi ni ni lazima akili yake iweze kufanya kazi vizuri zaidi na kwa mafanikio.
Moja ya vigezo walivyoviweka kama unataka akili yako ifanye kazi vizuri ni kama
hivi vifuatavyo:-
1. Chakula bora.
Ili akili yako iweze kufanya kazi vizuri sana,
inahitaji kwa kiasi kikubwa chakula bora, chenye virutubisho muhimu. Kwa mfano,
tafiti nyingi zilizofanywa kitaalamu zinaonyesha vyakula vya jamii ya samaki ni
muhimu sana katika kuipa akili yako afya ya kufanya kazi vizuri.
Hata hivyo utafiti huo haukuishia hapo tu,
unazidi kufafanua mara nyingi, watoto wanao tumia vyakula jamii ya samaki sana
huwa pia wana uwezekano wa kufanya vizuri hata darasani. Hivyo unaona, chakula
bora ni muhimu sana katika kuipa akili yako nguvu ya kufanya kazi vizuri.
2. Mazoezi.
Kati ya kitu rahisi ambacho hakiwezi
kukugharimu sana lakini ikiwa utakifanyia kazi na kitaifanya akili yako ifanye
kazi vizuri, ni mazoezi. Mazoezi yana uwezo mkubwa sana wa kuipa akili yako
nguvu kuliko. Wengi wanaofanya mazoezi, akili zao zipo vizuri.
Unaweza ukachukua jukumu leo la kuifanya akili
yako ikafanya kazi vizuri kwa kuamua kufanya mazoezi. Pengine unaanza kuwaza
unaanzia wapi? Kama ni hivyo usipate shida. Dakika 20 kwa siku iwe jioni au asubuhi
zinakutosha kabisa kuifanya akili yako ikawa na afya bora.
3. Fanya kazi za kujitolea.
Si kila wakati kazi unayofanya ni lazima ikupe
malipo. Kuna wakati kubali kujitolea kufanya kazi za jamii tena bure.
Unapofanya kazi kama hizi kikawaida kunakufanya ujisiie vizuri na mwisho wa
siku akili yako nayo inaanza kufunguka na kufanya kazi vyema hivyo hivyo.
Naona unashangaa katika hili, sikiliza. Wewe
ni matokeo ya jamii uliyopo. Kwa mujibu wa kanuni za maumbile ili uweze
kufanikiwa ni lazima uirudishie jamii yako kitu fulani kama shukrani. Sasa
mojawapo ya vitu hivyo, ndio kazi kama hizi angalau mara moja moja. Ukifanya hivyo
ujue kabisa akili itaanza kufanya kazi vyema.
4. Pata usingizi wa kutosha.
Pia usingizi wa kutosha kimetajwa kama ni
kigezo kimojawapo cha kuifanya akili yako kufanya kazi vizuri. Inasemakana
akili yako ili iweze kufanya kazi vizuri angalau unatakiwa kupata usingizi
usiopungua angalau saa nane kwa siku.
Najua hili unalijua vizuri, lakini je huwa
unalizingatia? Kama huwa ulizingatia sana, kuanzia sasa litilie mkazo na kuhakikisha
lazima akili yako inapumzika na kuipa nguvu ya kufanya kazi vizuri upya kwa
siku inayofuata. Ukifanya hivyo ni lazima akili yako ifanya kazi kwa ufasaha,
utake au sitake.
5. Jisomee kila siku.
Chakula bora peke yake hakitoshi kuipa akili
yako nguvu ya kufanya kazi kwa ufasaha. Kitu cha ziada ambacho kingine unatakiwa
kukiongeza ni kujisomea. Akili inayojisomea inakuwa ina nguvu sana ya kufikiria
na kufanya mambo kwa ubora.
Najua hili la kujisomea ni shida kwa wengi,
lakini hakuna namna nyingine ya kuifanya akili yako ikawa ina nguvu ya kuteda
kwa ubora, zaidi ya kujisomea. Unapojisomea unakuwa unaufikirisha ubngo na kuupa
changamoto na mwisho wa siku unajikuta umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa kumalizia makala haya, tambua hayo ndiyo
mmbo ya msingi ambayo yamezungumzwa na wataalamu kwamba yanaweza kuipa akili yako
nguvu ya kufanya kazi kwa ufasaha.
Chukua
hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia DIRA YA
MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.