Aug 17, 2016
Vitu Ambavyo Wengi Hujutia Sana Wanapofika Uzeeni.
Naamini
wote tunajua tunazaliwa, tunakua na ipo siku tutakuja fikia uzeeni. Hivyo kila
mtu kwa kujua hilo, hujitahidi sana kuishi maisha ambayo hatakuja kuyajutia kwa
hapo baadae akifika uzeeni. Kwa kifupi, kila mtu anapenda uzee wake uwe mzuri
ambao hauna lawama.
Hakuna
ambaye anapenda aje achekwe na watoto au wajukuu zake eti kwa kutotimiza
majukumu fulani. Kila mtu anapenda watoto au wajukuu zake wamsifie kwamba kweli
babu enzi za ujana wako ulifanya makubwa.
Hilo ndilo kila mtu analolitamani litokee katika uzee wake.
Lakini
hata hivyo kwa wengi waliofikia uzeeni kile wanachokitamani kiwe, huwa
hawakipata kwa sababu kadhaa. Hujikuta wakiishi maisha ya kujuta sana. Majuto
hayo hutokana hasa na mambo ambayo waliyafanya wakiwa vijana na kupelekea
pengine maisha yao kuwa magumu.
Sitaki
uwe miongoni mwa watu ambao wakifika uzeeni uje ujute kwa kulia sana. Leo
nanawa mikono kwa kukuonyesha vitu vya msingi ambavyo wengi huvijutia sana kila
wanapofika uzeeni. Sasa basi, vitu hivyo ambavyo wengi huvijutia sana hasa
wanapofikia uzeeni ni kama hivi vifuatavyo;-.
1.
“Kwa nini nilipoteza muda sana?”
Kati
ya jambo la wazi ambalo wengi waliofikia uzeeni wanalojutia ni kule kupoteza
muda. Huwa ni watu wa mawazo sana kutokana na lawama ambazo wanazipata kutoka
kwa jamii, watoto au wajukuu zao.
Mara
nyingi lawama hizi huelekezwa ni kwa nini maisha yao yako hivyo. Maswali kama
babu ulikuwa wapi wakati wnzako wanawekeza huulizwa sana. kwa hali kama hiyo
suala la kupoteza muda hujutiwa sana na wengi wakiwa uzeeni.
Wengi hujuta sana kwa kupoteza muda wao. |
2.
“Kwa nini sikuwekeza mapema?”
Si
kupoteza muda tu ambapo wengi wanapofikia uzeeni hujutia. Ila wakati mwingine
wanajuta kwa nini hawakuwekeza mapema wakati wa ujana wao. Hujiuliza maswali
mengi kwa nini hawakununua mashamba, hawakujenga nyumba, au kwanini hawakufanya
uwekezaji wa maana?
Hayo
yote huibuka mara baada ya kujiona wao wapo mikono mitupu na hawana nguvu tena.
Kilio, sononeko na majuto yanakuwa makubwa sana, hali ambayo inaweza kupelekea
kupata magonjwa yasiyotarajiwa kama shinikizo la damu.
3.
“Kwa nini sikuishi kwa kufuata ndoto zangu?”
Hili
pia huwa ni jambo linaloleta majuto hasa kwa wengi wanaopofikia uzeeni. Kitu
ambacho hujiuliza kila wakati kwa nini waliishi maisha ya kutimiza ndoto za
watu wengine, badala ya kukaa chini na kutimiza ndoto zao. Hapa huwaza sana je,
kipindi hicho walikuwa wamerogwa.
Hapa
walio fikia uzeeni hujiona wana hatia na makosa makubwa sana ambayo waliyafanya
wakiwa ujanani. Ukweli wote huo wanakuja kuujua baada ya kugundua kumbe hakuna
hata kitu cha maana walichokifanikisha duniani zaidi ya kufanikisha ndoto za wengine
na kusahau za kwao.
4.
“ Kwa nini sikuwasaidia wengi kutimiza ndoto zao?”
Pia
hufika mahali wale waliofikia uzeeni hutambua kwamba upo umuhimu mkubwa sana wa
kuisaidia jamii, hata kwa kidogo walichonacho. Lakini kila wakiangalia hakuna
msaada wa maana walioutoa. Hapo sasa ndipo huanza kuumia na kuwaza mengi.
Kiuhalisia,
huwa ni kipindi kigumu sana. Hapo ndipo unapoona wanajaribu kutoa angalau
msaada lakini inakuwa inashindikana kwa sababu pengine hawakujiweka vizuri
kiuchumi. Majuto ya kutokuwasaidia wengine huwaumiza sana pia.
5.
“Kwa nini sikujituma sana? ”
Wapo
wengine ambao hujita na kujilaumu kwa sababu ya kuona kwamba walitakiwa
kujituma sana hadi kufanikiwa. Sasa wanaona hawajafanikiwa na wanajua wazi hilo
ni kosa lao. Kila wakati wanapata shida na kujiuliza kwa nini hawakujituma sana
ili kujenga maisha mazuri zaidi.
Ikiwa
kweli una kiu kubwa ya kutaka uzee wako uonekana wa maana, basi unalazimika
kujituma sana kwenye kila jambo unalolifanya. Ikiwa hutajituma na kuweka
misingi imara wakati ukijana, sahau kuwana mafanikio uzeeni na zaidi utalamikiwa
na kujutia uzee wako wako wote.
6.
“ Kwa nini sikuishi na familia yangu kwa upendo?”
Haya
ni majuto huwa yapo wale wazee ambao kila wakikumbuka waliishi na familia kwa
migogoro mibgi sana. pi hali hiyo ilipelekea hata kutengana na kujikuta
wakiziacha familia zao zikiteseka.
Sasa
inapofika kipindi chha uzeeni hujikuta wakijuta na kujilaumu ni kwanini hayo
yote yalitokea. Ni kwa nini hawakuweza kuaysuluhisha mapema na kusababisha
mgogoro ambao unawasumbua hapo wakiwa uzeeni.
Kwa
kawaida unapokuwa kuwa kijana unaweza ukafanya makosa mengi na ukayachukulia
kawaida. Lakini inapofika uzeeni ndio unaanza kuelewa kwa nini ulikosea kufanya
hivyo.
Maisha
yako yapo mkononi mwako, kama bado una nguvu, jifunze kuwajibika ili baadae
usije ukajuta kwenye maisha yako ya uzeeni. Ukiangalia kwa ufupi hayo ndio
baadhi ya mambo ambayo wengi hujutia wakifikia uzeeni mwao.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.