Oct 20, 2016
Mfumo Unaotengeneza Maisha Yako.
Upo
mfumo unaotengeneza maisha yako na kuyafanya yawe hivyo kama yalivyo. Hapo ulipo upo
hivyo kimaisha si kwa bahati mbaya, mkosi au laana kama ambavyo unajifikiria
kila wakati, bali upo hivyo ni kwa sababu ya mfumo.
Kwa
bahati mbaya au nzuri mfumo huu mara
nyingi unautengeneza wewe iwe kwa kujua au kutokujua. Habari njema kubwa kwako ni kwamba, kwa vyovyote vile iwavyo, mfumo huo unao uwezo wa kuutawala hata kama
umejitengenezea mfumo mbovu.
Mfumo
huu ambao ninauzungumzia hapa na ambao unatengeneza maisha yako upo kwenye
mawazo yako. Mawazo yako ni kila kitu ikiwa utajua namna ya kuyatawala na kuyatumia
vizuri ili yakupe mafanikio.
Tatizo
kubwa la sasa ni kwamba, ulimwengu umejazwa na watu wengi ambao hawajui jinsi
ya kutawala mawazo yao. Kwa sababu hiyo
hujikuta ni watu wa kuishi tu kwa kupoteza muda bila ya kuwa na mafanikio
makubwa.
Kila wakati fikiria kile unachokitaka kwenye maisha yako. |
Na
kitendo cha kutokutawala mawazo yao kinasababishwa na watu wengi kushindwa
kuelewa kile kinachoweza kutawala maisha yao. Nikiwa na maana ule mfumo ambao
unaweza ukatawala maisha ya mtu.
Mfumo
huu unaotengeneza maisha yako umefundishwa tokea miaka mingi sana na
umefundishwa pia karibu na dini zote. Kwa
mfano tukisoma bibilia mithali 23;07 inatuambia “maana aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo…”
Andiko
hilo linatuthibitishia na kutuonyesha kwamba mfumo unaoendesha maisha ya
binadamu upo kwanza kwenye mawazo yake. Kipi unachokifikiri? Kipi unachoendelea
kukiwaza kila wakati hicho ndicho kinaunda maisha yako.
Wanasaikolojia
pia wanatufundisha kwamba kila mtu ana kitu anachokiwaza au kile anachokiweka akilini
kwa muda mrefu. Kitu hicho ambacho
kinakuwa kipo akilini au picha ambazo unaziweka ndizo zinazo tengeneza maisha
yako.
Ukichunguza
utaelewa hicho kinachozungumzwa kipo na tunakiishi. Hiyo ikiwa na maana mfumo
unaoendesha maisha ya mwanadamu upo kwenye kile anachokifikira kia wakati.
Hakuna ubishi juu ya hili, ushahidi upo karibu kila kona.
Kwa
mfano tunaona, watu maskini wanaendelea kuwa maskini zaidi kwa sababu ya mawazo
au picha zile wanazoziweka kwenye akili zao. Kila wanachokiwaza au kikiona ni
umaskini na mwisho wa siku huushia kuupata huo umaskini.
Pia
watu matajiri wanaendelea kuwa matajii zaidi, lakini hiyo yote inatokana na
kile wanachokiwaza kwa muda mrefu. Watu hawa kila wakati huwaza mafanikio,
hivyo kwa sababu hiyo huvuta mafanikio na utajiri maishani mwao.
Kama
kila wakati unaona umaskini, ni wazi utakuwa maskini. Kama kila wakati unawaza
utajiri na kuweka picha za utajirii nalo hilo utalifanikisha bila shida yoyote.
Mfumo unaotengeneza maisha yako yawe ya kushindwa au mafanikio haudanganyi,
unakupa kile unachokizingatia akilini mwako.
Kwa
kuwa mfumo huu upo, kila mmoja wetu anatakiwa kujua namna ya kujifunza kutumia
na katawala mawazo yake kwa ufasaha ili yaweze kumpa mafanikio makubwa.
Lakini
ikiwa endapo utaacha mawazo yako yakutawale, hutaweza kufanikiwa zaidi utabaki na
utaendelea kuishi maisha ya kuwasindikiza wengine kwenye maisha na utashangaa huoni
mafanikio yoyote yale.
Ili
sasa uanze kuufaidi mfumo unaoutengeneza maisha yako na ukafikia mafanikio
makubwa kama wengine, kila wakati unatakiwa kuwaza kile unachokitaka. Acha
kuwaza na kinyume unachokitaka.
Jaza
picha za kule unakokwenda. Jaza picha za kile unachotaka kukifanikisha. Jaza picha
za kiwango cha pesa unachokitaka mwaka huu. Ukifanya hivyo kila wakati huku
ukichukua hatua za utendaji UTAFANIKIWA.
Kwa
kifupi hivyo, ndivyo ambavyo mfumo unaotengeneza maisha yako jinsi unavyofanya
kazi. Kumbuka kila wakati hakuna bahati, muujiza wala mkosi katika maisha bali
upo mfumo unaotengeneza maisha yako.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda
pia kuchukua fursa hii kukukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga
tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha
ikifuatia na jina lako kwenda 0713 04 80 35
ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.